Breaking News

Your Ad Spot

Oct 9, 2014

BENKI YA CBA YATANUKA HUDUMA ZA M-PAWA

DSC_0055Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo akizungumza wakati kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wao kwa kuichagua CBA pamoja na kuwapongeza wafanyakazi wa benki yake kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja wao katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye tawi la CBA Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru na Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa (aliyesimama kushoto).(Picha na Zainul Mzige).
DSC_0001Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo (aliyekaa kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wa benki ya CBA ambapo watatumia wiki hii kusikiliza nini wateja wao wanataka. Waliosimama kutoka kulia ni Meneja wa tawi la CBA Kariakoo, Vicky Munishi, Boniface Kiwia kutoka makao makuu ya CBA, Tanzania, Rehema Mashayo kutoka makao makuu wa benki ya CBA Tanzania. na kushoto ni Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa.
Na Mwandishi wetu
HUDUMA ya M-PAWA inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianzishwe.
Pamoja na fedha hizo huduma hiyo imewezesha kuwepo na amana za shilingi bilioni 6 kutoka kwa wateja laki 7 ambao wanapata huduma ya M-Pawa.
Taarifa hiyo ya mafanikio imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Julius Mcharo akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika Kariakoo.
Mcharo alisema huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na Vodacom imepata muitikio kutokana na watanzania kuweza kufungua akaunti za huduma hiyo mahali popote pale walipo kwa kutumia mtandao.
Alisema huduma hiyo ambayo pia inawezesha kupatikana kwa mikopo na kupokea na kulipa huduma mbalimbali kwa m-pesa imerahisisha maisha ya wananchi wengi na kusema kwamba itaendelea kuboreshwa na kutanuliwa.
Akizungumzia wiki ya huduma kwa wateja alisema kwamba watendaji wote wa benki hiyo wanakwenda katika matawi yapatayo 11 nchini kote kutoa huduma kwa karibu zaidi na wateja wao kwa lengo la kufahamu changamoto zao.
Alisema changamoto hizo zitawawezesha kutambua mahitaji halisi ya wateja na kutengeneza bidhaa zinazolingana na mahitaji yao.
DSC_0080Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wakitangaza rasmi kuzindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja watakayoitumia kusikiliza changamoto wanazokutana nazo wateja wao.
Alisema benki hiyo ambayo ina matawi matano Dar es salaam na mengine yakitawanyika katika miji ya Mtwara, Mbeya,Arusha, Tunduma imejitanua katika kutoa huduma kwa kutumia teknolojia hasa kwa kuwa na huduma za kibenki kwa njia ya mtandao.
Alisema kupitia njia ya mtandao wateja wao wanaweza kupata mikopo na hata kulipa huduma mbalimbali.
Aliwashukuru wateja na wafanyakazi kwa kuwezesha ndoto za wengi kutimia kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo na kuwataka waendelee kutumia CBA katika kuchupa mbele kimaendeleo.
Baadhi ya wateja waliohojiwa katika uzinduzi huo walikiri kufurahishwa na huduma za benki hiyo hasa kutokana na kutokuwa na foleni na kujali wateja wao.
Charles Mlawa alisema kwamba wamefurahishwa sana na uwapo wa tawi la CBA Kariakoo kwani limefanya waweze kuwa na uhakika na utumaji wa fedha kwa wadau wao ili kupata bidhaa zinazotakiwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages