Breaking News

Your Ad Spot

Oct 8, 2014

FIKA YAJA NA MPANGO WA 'FIKA NA FINKA'

 Mkuu wa Huduma za Kibenki wa FINCA,Bwa.Gershom Mpangala akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),kuhusiana na taasisi hiyo ya Kifedha kuzindua kampeni yake mpya  iliyojulikana kwa jina la Fika na Finca,kampeni inayolenga kuwafikia Watanzania wote kupitia huduma za kibenki na kuwasaidia kutimiza malengo ya kimaendeleo waliyojiwekea,Mkutano huo umefanyika kwenye moja ya Ofisi zao zilizopo Mwembechai Jijini Dar.Pichani kati Kaimu Afisa Mwendeshaji Mkuu wa FINCA Tanzania ,Bwan.Daniel Mhin pamoja na Meneja tawi la Magomeni Bwa.Cassian Clovis
Pichani kati ni Kaimu Afisa Mwendeshaji Mkuu wa FINCA Tanzania ,Bwan.Daniel Mhina akifafanua zaidi kuhusiana na Faida za akaunti za akiba za Finca kuwa ni nyingi,ikiwa ni pamoja na urahisi wa kufungua na kuendesha akaunti,taratibu za kufungua akaunti zina mahitaji madogo,kutoa na kuweka pesa bure kwenye matawi yote nchini na usalama wa fedha za mteja kupitia mfumo wa bayometriki unaotumiwa na benki hiyo.Bwan Daniel alisema kuwa kupitia matawi ya FINCA inahudumia wateja zaidi ya 120000 ambao wanahudumiwa na zaidi ya wafanyakazi 700 nchini. pichani shoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki wa FINCA,Bwa.Gershom Mpangala pamoja na Meneja tawi la Magomeni Bwa.Cassian Clovis.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa FINCA uliofanyika jijini Dar leo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages