Breaking News

Your Ad Spot

Oct 3, 2014

KINANA ATINGA TANGA MJINI KWA KISHINDO NDEREMO NA HEKAHEKA VYATAWALA KILA KONA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa katika Kivuko cha mv Pangani, wakitokea wilaya ya Pangani kwenda wilaya ya Tanga mjini leo asubuhi, Oktoba 3, 2014
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakishuka kwenye kivuko hicho wakati wakitoka Pangani kwenda Tanga mjini leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aksalimia wananchi baada ya kutoka Pangani wakiwa njiani kwenda wilaya ya Tanga mjini. Kulia ni Mbunge wa Pangani, Salehe Pamba na Katibu wa NEC, Itikari na Uenezi, Nape Nnauye
 Nape akisalimiana na wananchi baada ya yeye na Kinana kushuka kutoka katika Kivuko cha mv Pangani
 Kinana akizungumza na wananchi baada ya kushuka kutoka kivuko cha mv Pangani akiwa njiani kwenda wilaya ya Tanga mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimia wananchi alipowasili Kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini kuendelea na ziara yake katika mkoa wa Tanga leo
Wananchi wa Marungu, wilaya ya Tanga mjini wakimshangilia Kinana alipowasili katika eneo hilo leo
 Aliyekuwa waziri wa Uchukuzi, Mbunge wa Tanga, Omary Nundu akisalimia wananchi katika Kijiji cha Marungu baada ya kuwasili eneo hilo akiwa na Kinana
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Halima Tendegu akisalimia wananchi, Marungu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupaua Ofisi ya CCM, Kata ya Marungu wilaya ya Tanga, leo akaiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kukagua uhai wa Chama katika mkoa wa Tanga.
 Kinana akisalimiana na mkazi wa Kata ya Marungu, Justine Lampert
 Kinana akiwasalimia wauguzi wa zahanati ya Kata ya  Tangasisi alipofika kuzindua Wodi ya Kinamama
 Vijana wa Tangasisi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, alipozungumza na wananchi katika kata hiyo ya Tangasisi leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkazi wa Kata ya Tangasisi Athumani Mzigo, wakati alipotoa kadi hizo kwa wanachama wapya wa mfuko huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wodi ya Kinamama zahanati ya Kijiji cha Machui, kata ya Tangasisi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Tanga, leo.
Omari Nundu akishiriki ujenzi wa wodi hiyo, kuhusu akisimamiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana leo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Tendegu. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages