Breaking News

Your Ad Spot

Oct 8, 2014

KINANA ATINGISHA KILOLO LEO, AMPANDISHA JUKWAANI KIONGOZI WA CHADEMA AELEZE ALIVYOSIMAMIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Profesa Peter Msola, alipowasili eneo la Kilolo Minadani, na kufanyiwa mapokezi, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM, katika jimbo hilo, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo, Oktoba 8, 2014. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Seti Mwamoto
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na mwenyeji wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, Seth Mwamoto baada ya kuwasili katika jimbo la Kilolo wilayani humo leo, 
 Vijana waliojiajiri katika kikundi cha Muungano cha ufyatuaji matofali katika jimbo la Kilolo, wilayani Kilolo mkoani Iringa wakiwa kazini alipowatembelea Kinana leo, Oktoba 8, 2014. Zaidi ya vijana 40 wamo katika muungano huo.
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Seki Kasuga (kushoto) akifuatilia matukio Kinana alipotembelea Umoja wa wajasiariamali wa kikundi cha kufyatua matofali kwa teknolojia ya kisasa katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo mkoani Iringa leo 
 Kinana akizungumza na vijana hao kabla ya kushiriki ufyatuaji matofali. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye anayefuatana na Kinana kwenye ziara hiyo ya mkoa wa Iringa
 Kinana akisisitiza jambo alipozungumza na vijana wa kikundi hicho kabla ya kushiriki ufyatuaji matofali. Kinana alizitaka mamlaka zinazohusika kuwapatia vijana hao eneo lenye maji ya uhakika kwa ajili ya ufyatuaji matofali, baada ya kumweleza kuwa pamoja na kuufurahia mradi huo wa ufyatuaji matofali lakini wanakumbana na changamoto ya kukosa maji kwa kuwa eneo wanalofanyia mradi huo halina maji.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali akiwa na Prof. Peter Msola (kushoto), alipotembelea mradi wa vijana wajasiriamali wa kikundi cha ufyatuaji matufali kwa teknolojia ya kisasa katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo mkoani Iringa, leo

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua alipotembelea mradi wa vijana wajasiriamali wa kikundi cha ufyatuaji matufali kwa teknolojia ya kisasa katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo mkoani Iringa, leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofal, alipotembelea mradi wa vijana wajasiriamali wa kikundi cha ufyatuaji matufali kwa teknolojia ya kisasa katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo mkoani Iringa, leo
 Katibu Mkuu wa CCM akipanga matofali baada ya kushiriki ufyatuaji wa matoli kwenye mradi huo wa vijana wa Kilolo 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi kwenye Halmashauri ya Kilolo, pamoja naye Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita

BAADAYE KINANA ALIENDA KUCHAPA KAZI IHIMBO
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye viwanja vya zahanati ya Kijiji cha Utengule kata ya Ihimbo, kabla ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo, kwenye jimbo la Kilolo, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye viwanja vya zahanati hiyo ya Kijiji cha Utengule
 Wananchi wakisoma utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyofanywa na Mbunge wa Kilolo Profesa Peter Msolwa, Kinana alipowasili kwenye zahanati hiyo
 Mbunge wa Kilolo Profesa Msola akieleza alivyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Utengule kwa tiketi ya Chadema, Parcras  Mkakatu akisikiliza maelekezo ya Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Utengule (Chadema), Parcras  Mkakatu akijieleza kwa Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Utengule (Chadema), Parcras  Mkakatu akijieleza kwa Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
 Wazee wa Kihehe wakimpamba Kinana kwa mavazi rasmi ya keshima ya kabila hilo katika kijiji cha  Utengule, baada ya kuhutubia wananchi kwenyeviwanja vya zahanati ya Kijiji hicho
 Kisha wazee hao wakampa mkuki kukamilisha heshima hiyo
 Kinana akishuka jukwaani baada ya kuwashukuru wananchi kwa wazee hao kumpa heshima ya uchifu
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi wa Kiijiji cha Utengule baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Zahanati ya Kijiji hicho leo,Oktoba 8, 2014. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages