.

RAIS JAKAYA KIKWETE AREJEA NCHINI LEO KUTOKA KATIKA MATIBABU NCHINI MAREKANI

Nov 29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Rais Bw. Morris Mbena baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Said Mecky Saidk, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwammunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014. Wengine kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu na Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Kamishna Jenerali, John Minja.
 Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimlaki Rais Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi hayo, kwenye Uwanja wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo
 Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya viongozi waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
 Mama Maria Nyerere akizungumza na Mama Salma Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya Rais Kikwete (kulia), kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha na mwanaye Khalifa Jakaya Kikwete wakati alipowasili Ikulu leo akitokea nchini Marekani kwa matibabu.

AJALI YA HELKOPTA DAR ES SALAAM, YAUA MARUBANI WANE

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar, Ilala jijini Dar es Salaam.GPL(P.T) Read more...

ZITO ALIPULIWA NA RAFIKI YAKE KIPENZI, LUSINDE PESA ZA ESCROW NAE YUMO

Hii ndiyo barua iliyoandikwa na zito kwa ajili ya kukopa fedha hizo za Escrow kumpeleka mama yake india kutibiwa. Barua hii iliyo na vithibitisho kadhaa pamoja na kopi ya leseni ya aliyetumwa iliwasilishwa na Mbunge Lusinde Bungeni na kusomwa kisha kuikabidhi meza kuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Lusinde akichangia wakati wa mjadala huo ukiendelea Bungeni jana jioni huku akionyesha barua hiyo inayomhusisha Zito katika kashfa hiyo.
Lusinde akiendelea kuchangia huku akiwavunja mbavu wabunge kwa vijembe vyake.
Mbunge Kafulila, akichangia kujaribu kuthibitisha ukweli wa sakata hilo.
Kafulila akiendelea kumwaga nondo.
Mbunge, Joshua Nassari, akisimama kuomba mwongozo, jambo lililomfanya mwenyekiti wa kikao hicho, Zungu kuingilia kati na kupiga marufuku wabunge kuomba mwongozo wakati mmoja wao akiendelea kuchangia, kutokana na kuchelewesha muda.
Sehemu ya wabunge waliohudhuria kikao hicho cha jana jioni. 

KINANA ASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA NANGURUWE.

Nov 28, 2014


 Wananachi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Mtwara Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Kinana akizungumza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kibaoni, Mtwara Vijijini leo.

 Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Katika Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya Mtwara Vijijini

 Mzee Ismail Lumbeya (95), akisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Nanguruwe

Mnara wa Kumbukumbu ya Mwanajeshi wa Tanzania , Hamad Mzee aliyeuawa na ndege ya kivita ya wareno baada ya kuzitungua ndege mbili za kivita mwaka  1972 katika Kijiji cha Kitaya mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakati wa mapambano ya kuikomboa Msumbiji

 Kinana akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu shujaa Hamad Mzee katika Kijiji cha Kitaya, Mtwara Vijijini

 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Kitaya

 Ngoma ya asili ikitumbuiza wakati wa mkutano huo

 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo

Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Kinana akipanda katika moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwa makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini katika mkutano wa hadhara wa katika Kata ya Kitaya.

Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama wapya wa chama hicho katika mkutano huo
 Watoto wakiwa na vipeperushi vya picha ya Kinana wakati wa mapokezi yake katika Kijiji cha Kibaoni

 Kinana akikunjua bendera wakati wa uzinduzi wa Tawi la CCM la Vijana akatika Kijiji cha Nanyamba

 Kinana akitoka kukagua mradi wa maji katika Kata ya Nanyamba Mtwara Vijijini

 Vijana wakicheza ngoma ya madudu katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Nanyamba Kinana akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe kinachotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya Mtwara Vijijini

Kinana akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe

MAXCOM AFRIKA YATIMIZA MIAKA MITANO, YABADILI MUONEKANO WA HUDUMA YAO YA MAX MALIPO

 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya  MaxCom Africa, inayotoa huduma za Max Malipo,  Juma Rajabu  na Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula wakikata utepe kuzindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo, katika hafla iliyokutanisha uongozi wa kampuni hiyo ya Jukwaa la Wahariri, leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akizindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo itakavyokuwa sasa kwenye ofisi za mawaakala wake.
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula, kuashiria kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa la Wahariri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa Mwakilishi wa Manispaa ya Ilala Mashauri Saidii, kuashiria kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa la Wahariri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya MaxCom Africa, Juma Rajabu akishikana mkono na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevile Meena baada ya kutangaza kulichangia Jukwaa hilo sh. milioni 5
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya  MaxCom Africa, Juma Rajabu (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mwishoni mwa mazungumzo yaliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kushoto ni Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevile Meena
 Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, Juma Rajabu akizungumza na wahariri Serena hotel 
 Ofisa Mkuu wa Operesheni, wa Maxcom Africa, Ahmed Rusasi akieleza huduma za Max Malipo zitolewazo na kampuni hiyo, wakati wa kikao hicho na wadau katika hoteli ya Serena jijini DSar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MaxCom Afrika akiwa ameketi meza kuu na wadau
 Baadhi ya viongozi wa Maxcom Afrika katika hafla hiyo
 Wadau kutoka Jukwaa la Wahariri
 Wadau kutoka Jukwaa la Wahariri
 Wadau kutoika jukwaa la wahariri
Baadhi ya waalikwa kutoka Jukwaa la wahariri wakipata chakula cha mchana ambacho kilitoplewa kwa wote katika hotelo ya Serena jijini Dar es Salaam, baada ya uongozi wa MaxCom Afrika kumaliza mazungumzo yao na wadau katika kuadhimisha miaka mitano ya kampuni hiyo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
ยช