.

CHADEMA IRINGA WAPELEKANA POLISI, NI MWENYEKITI WA MKOA NA WA WILAYA WA CHAMA HICHO

Dec 31, 2014


Na Matukiodaima Blog
HALI  ya  kisiasa  ndani ya  chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)  mkoa wa Iringa si shwari  baada ya mwenyekiti wake mkoa  wa Iringa Mustapher Msowela  kumfikisha polisi  mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Iringa mjini, Frank Nyalusi

Nyalusi  ambae  pia ni  diwani  wa kata ya Mvinjeni jimbo la Iringa mjini juzi alitiwa nguvuni na  jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
 
Nyalusi aliyeshitakiwa katika kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa jana, anatuhumiwa kumtusi mwenyekiti wake huyo wa mkoa kupitia mitandao ya simu; matusi yanayoendelea kuchunguzwa na jeshi hilo.
Nyalusi amekamatwa kwa tuhuma hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya kudaiwa kutoa tuhuma za uongo kwa lengo la kujipatia umaarufu dhidi ya mfanyabiashara maarufu wa mjini Iringa, Salim Asas ambaye pia ni Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa.
 
Katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Chadema Desemba 21 kwenye uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni alitoa tuhuma zinazowahusisha vijana watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina kwamba walitumwa na Asas kwenda kumuua.
 
Asas kwa kupitia kwa wakili wake, Alfred Kingwe amekanusha tuhuma hizo alizoziita ni za kipuuzi ambazo haziwezi kubebeka hata kwa mzani mdogo wa kupimia madini.
 
Ili kumsafisha mteja wake, Kingwe alisema ndani ya siku 14 toka akabidhiwe hati ya madai (Demand Note), Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika eneo lile lile alilotolea tuhuma hizo na kuzikanusha vinginevyo atafikishwa mahakamani.
 
Akizungumza na wanahabari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema;  “Kuhusu tukio la kumtukana mwenyekiti wake wa mkoa, Nyalusi alikamatwa jana mara baada ya Msowela kuwasilisha malalamiko yake polisi, akahojiwa na kuachiwa baada ya kukamilisha taratibu za dhamana.”
 
Alisema jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza tukio hilo la kijinai na endapo litathibitika kuwa la kweli, Nyalusi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mivinjeni mjini Iringa atafikishwa mahakamani.
 
Kuhusu tukio linalomuhusisha na Asas, Kamanda Mungi alisema jeshi la Polisi limefanya mahojiano ya awali na wahusika hao.
 
“Jambo hili lipo, tunachunguza; yapo maneno Nyalusi ameyatamka kwenye mkutano wao wa hadhara kwamba ametishiwa kuuawa, ametumiwa watu watatu kwenda kumuua wakiwa na visu. Kumtishia mtu ni kosa la jinai na kumtuma mtu kwenda kumdhuru mtu mwingine ni kosa la jinai, kwahiyo tunachunguza” alisema.
 
Alisema katika mazingira ya uwazi, Polisi inachunguza suala hilo ili kujua Nyalusi alitishiwa katika mazingira gani; alitishiwa na nani na kwanini hakwenda kutoa taarifa hiyo Polisi na kufungua kesi ili Polisi iwakamate wahusika na kulinda maisha yake.
 
“Lakini tunajaribu kuangalia kama hakutishiwa na ametamka vile katika mkutano wa hadhara, lengo lake lilikuwa ni nini na kama anajua madhara yake kwa jamii iliyosikia taarifa hiyo ni yepi,” alisema.
 
Alisema kama itabainika taarifa zilizotolewa na Nyalusi ni za uongo, sheria itachukua mkondo wake na kama itadhihiri ni za kweli sheria pia itachukua mkondo wake.

WAZO MTAMBUKA KWENDA KWA RAIS KIKWETE

NAKUSHAURI RAIS WANGU KIKWETE, MUACHE MUHONGO AMALIZE KIBARUA CHAKE
Rais Kikwete
Said Mwishehe
PANAPO majaaliwa ya Mungu, kesho tunaungana na mataifa mengine duniani kusheherekea mwaka mpya wa 2015.

Hivyo, kwa hesabu za kalenda ya mwaka 2014, leo hii tunamaliza muda uliobaki kabla ya kuingia mwaka 2015.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuendelea kutupa pumzi yake. Ametujaalia afya njema. Hili ni jambo la kushukuru.

Pia nitumie nafasi hii kutoa pole kwa ndugu, rafiki na jamii zetu ambao leo hii hatunao tena. Wametangulia mbele za haki.

Hiyo inatokana na mapenzi yake muumba wa mbingu na ardhi. Tuwaombee dua njema huko waliko.Mbele zao, nyuma zetu.

Wakati tunakaribia kuingia mwaka 2015, nitumie nafasi hii kuowambea wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Imani yangu Mungu atawaponya na kuwarejesha kwenye afya njema na hatimaye kuendele na ujenzi wa taifa.

Wakati tunajiandaa kuupokea mwaka mpya, kuna mambo mengi ambayo yametokea kwenye mwaka huu wa 2014.

Yapo ambayo yametunufaisha kama taifa lakini wakati huo huo yapo ambayo yametufedhehesha.

Mwaka 2014 ulikuwa mwaka wa matukio mengi katika nyanja mbalimbali. Nikiri kuna mambo ya kujivunia na kuna mambo ya hovyo ambayo yametokea kwenye taifa hili ambalo linaendelea na juhudi za kusaka maendeleo yake.

Sote ni mashahidi Watanzania kwa nafasi zao mbalimbali wameendelea na ujenzi wa taifa leo. Wameendelea kudumisha umoja na mshikamano wao.

Wameendelea kuungana kupigania maisha yao. Ni watu ambao hawataki kukataa tamaa. Wanafanya kila juhudi kuhakikisha taifa linasonga mbele.

Nikiri kauli ambayo inaliumiza taifa hili ni kuendelea kuimba wimbo wa "Sisi maskini". Wimbo ambao kwangu mimi unaniumiza kichwa. Sitaki hata kuusikia. Sitaki kuusikia kwasababu ni sehemu ya adui wetu wa maendeleo yetu.

Sisi maskini ni kauli ambayo imetukwamisha kwa miaka mingi sasa. Hata mwaka huu wa 2014, kauli ya sisi maskini imeturudisha nyuma.

Kujiita kila siku maskini ndio matokeo yake tunashinda kuishi maisha ya kuendelea kuomba misaada. Kisa tu nchi yetu eti maskini.

Kwangu naamini sisi si maskini ila huenda tunakosa mipango na usimamizi mzuri wa kufikia malengo yetu.hili ndilo tatizo ambalo linatusumbua kwa miaka mingi.

Mwaka 2015 ni mwaka wa kubadili mitazamo na fikra zetu. Tukitumia vema rasilimali zetu, tutapiga hatua. Kila kitu tunacho.tunachotakiwa ni mipango na usimamizi mzuri. Tuache akili za kuwa tegemezi kwa kila jambo.

Inashangaza tunapokuwa na msitu mkubwa wa misitu kama ule wa Sao hili Iringa halafu kijiti cha kusafishia meno kinatoka China. Ama kweli!

Inasikitisha kuona imefika mahali eti kila kitu lazima kitoke nje. Kasumba hii inatokana na yale yale ambayo wengi yametutawala kwenye akili zetu kuwa lazima tuwe tegemezi.

Hatupaswi kuwa na akili hiyo kwa mwaka 2015. Ni mwaka wa kutafakari kama taifa nini tufanye ili tusonge mbele.

Kwa bahati mbaya tumekuwa na kundi kubwa ambalo linatumia muda mwingi kupiga soga vijiweni kwa ajenda ambazo hazina mashiko ya kimaendeleo. Ni rahisi kusikia watu wanajadili nani kavaa nini. Fulani analula nini?

Wanaojadili tunapigaje hatua kama taifa ni wa chache. Hata hao tunaowategemea kutupigania wamekuwa wa kuishi kwa matukio. Likija tukio hili wamo, likija lingine wamo.Mafundi wa kuongoa kuliko kutenda.

Inasikitisha sana.Tumeyaona hayo mwaka 2014.Si vizuri yakajirudia tena mwaka 2015. Kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa, ndio kosa. Tusimamie kama nchi tuangalie maisha yetu. Tumetoka wapi na tunakwenda wapi.

Tukisoma vitabu vya historia tunaambia Tanzania na China zilianza harakati za kusaka maendeleo mwaka mmoja. Nenda leo China kaingalie.

Hatufanani nayo kwa namna yoyote ile.Watu tulianza nao kwenye harakati za kutafuta maendeleo, eti leo tunawapigia magoti kuwaomba msaada.

Wachina wameijenga nchi yao.Wameamua kusimama kidete kuhakikisha taifa lao linapiga hatua na kuwa lenye nguvu duniani.  Sishangai Marekani inapokwenda kuomba misaada ya kifedha China.

Kwetu sisi maendeleo yetu yamekuwa ya mwendo wa kinyonga. Wananchi wamekata tamaa ya maisha. Kila kukicha wanasema afadhali ya jana. Ndio maisha ambayo tumeamua kuishi.

Imefika mahali Wachina wameamua kuja nchini kwetu na kufanya kazi ambazo tumeshindwa kuzifanya. Nenda Kariakoo jijini Dar es Salaam, Wachina wanauza maua.Wanauza karanga.

Inasikitisha inapofika mahali hata karanga tunashindwa kuuza. Tunasibiri Wachina waje wauze. Halafu tumebaki kupiga kelele tu.Tumefika mahali pabaya.

Sifa ya taifa kupiga hatua za maendeleo linahitaji kuwa na siasa safi, utawala bora, ardhi na watu.

Nikiri tunaweza kuwa tumekosa siasa safi na uongozi bora lakini tuna ardhi ya kutosha na watu. Kwa bahati mbaya watu wapo lakini kasi ya maendeleo haiendani na idadi yetu.

Kitendo cha kukosa siasa safi imefika mahali, wanasiasa wengi wametugeuza kama vile kichwa na mwendawazimu. Wanatuongopea watakavyo.

Wanajua hatuna tunaloweza kulifanya. Hakika mwaka 2014, licha ya kufanya mambo ya maendeleo, yapo ambayo tunapaswa kujiepusha nayo mwaka 2015.

Msomaji wa safu hii, baada ya kutoa maelezo hayo ambayo kwangu mimi kwa siku ya leo ni kama utangulizi sasa nije kwenye ajenda yangu ya Jumatano ya leo.

Ajenda yenyewe ni hili sakata la Escrow.Sakata ambalo limekuwa gumzo kwenye kila kona ya nchi yetu. Limekuwa likizungumza na kila mtu. Kama hulizungumzi wewe basi analizungumza mwenzio.

Sakata la Escrow limetikisa nchi yetu kwa sehemu kubwa. Sote tunafahamu mjadala huo wa Escrow unatokana na utata wa fedha wa sh. bilioni 306 zilizopo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, wajanja kuamua kuzichukua.

Wanasiasa wa kada mbalimbali wamekuwa wakilizungumza hilo kwa kina. Wamekuwa wakipambana kwa hoja. Wamekuwa wakijadili na kuelezea umma kuhusu fedha hizo.

Nikiri mwaka 2014, mjadala wa Escrow kwangu mimi naona ulikuwa ni mjadala uliochokuwa sehemu kubwa ya mazungumzo kuliko mijadala mingine.

Ni kweli kulikuwa na mjadala kuhusu Katiba mpya lakini ujio wa sakata la Escrow umefunika kabisa mazungumzo ya Katiba inayopendekezwa.

Kwa kuwa hata wanasiasa wetu nao wanaishi kwa matukio. Wengi wao wameachana na ajenda ya Katiba mpya ambayo wananchi wanahitaji kuelimisha licha ya wao wenyewe kujisomea Katiba inayopendekezwa kabla ya kufanya uamuzi kwa kupiga kura ya ndio au hapa.

Leo hii ili mwanasiasa aonekane amezungumza jambo la maana basi anaamini akizungumzia Escrow ndio nyota ya siasa inasafishika.

Sina tatizo na wanasiasa ambao wamelizungumzia sakata hilo hadi hapa lilipofikia. Tunajua Bunge limetoa maazimio nane kwa Serikali.

Maazimio ambayo kwa sehemu kubwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inatakiwa kuamua kwa kuchukua hatua dhidi ya wanaohusishwa na uchotaji fedha wa Escrow.

Ndio maana aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema ameamua kuachia ngazi.

Uamuzi huo unatokana na ukweli kwamba ushauri wake kisheria hakueleweka. Jaji Werema anasema amechafua hali ya hewa.

Pia tunafahamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi naye amsimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi. Kisa sakata hilo hilo la Escrow.

Nani ambaye hafamu kama aliyekuwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka naye ametemwa kwenye baraza la mawaziri.

Kilichomuondoa ni kupokea fedha za Escrow.Prof. Tibajuka aliwekewa kwenya akaunti yake binafsi sh. bilioni 1.6.

Wakati mjadala huo unaendelea, hakuna mwanasiasa ambaye ameweza kupata ujasiri wa kuliambia taifa fedha hizo ni za umma au si za umma. Nani mwenye fedha hizo?.

Ujasiri ambao wanasiasa wetu walio wengi wanao hadi sasa ni kwamba sh. bilioni 306 za Escrow ni za umma. Wamesema hivyo wakiwa bungeni na wanaendelea kusema hivyo nje ya Bunge.

Kwangu mimi na hata kwa Watanzania wengine, nimefurahishwa na hotuba ya Rais Kikwete.Hotuba ambayo aliitoa Desemba 22 mwaka huu. Alikuwa anazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kama kiongozi wa nchi ameonesha kulifahamu vema suala hilo. Akatumia nafasi hiyo kuelezea historia nzima ya sakata la Escrow.

Akaeleza namna ambavyo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na IPTL walivyokuwa wanalipa.

Pia, akaeleza namna ambavyo akaunti ya Tegeta Escrow iliovyofunguliwa hadi hatua ya IPTL na wanahisa wenzake kuuziana hisa na kisha kufunga akaunti ya Tegeta Escrow na kuchukua fedha zilizomo.

Rais Kikwete baada ya kutoa maelezo mengi ya kueleweka pengine kuliko yale yaliyokuwa yanatolewa na wanasiasa walio wengi akatumia nafasi hiyo kuwahakikishia Watanzania kuwa fedha hizo ni za IPTL.

Rais Kikwete katika hotuba yake alisema"Fedha hizo ni za IPTL maana ni malipo ambayo yalikuwa yanalipwa kutoka Tanesco ambazo ni tozo la uwekezaji, lakini toafuti yake fedha zilikuwa zinawekwa kwenye akaunti maalumu".

Kimsingi hotuba ya rais imejibu swali la msingi ambalo Watanzania wengi walikosa kulisikia.Pamoja na kusema fedha hizo ni za IPTL bado akauthibitisha umma kuna kodi ya Serikali ndani yake.

Hivyo tunapoumaliza mwaka 2014, naamini rais amesema kile ambacho wengi tulipaswa kukisikia.Akasisitiza uchunguzi ufanyike na kisha sheria ichukue mkondo wake.

Akaagiza mamlaka zinazohusika na uchunguzi zitakapokamlisha taarifa , yeye atakuwa na uamuzi wa kufanya.

Baada ya kulifafanua kwa kina suala hilo, rais akatumia nafasi hiyo kuweka wazi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amemuweka kiporo.

Bwana we! kauli hiyo ya Prof.Muhongo kuwekwa kiporo imeamsha hasira za wanasiasa hasa za wapinzani.

Wametoa matamko ya kumtaka Rais Kikwete kumuwajibisha Prof.Muhongo kwa kumuondoa kwenye nafasi hiyo.

Wengine wametangaza kufanya maandamano nchi nzima.Najiuliza sababu za  msingi za kufanya maandamano hayo.

Najiuliza hivi wanaotaka Prof.Muhongo aondolewe kwenye nafasi hiyo ni kweli wanashinikiza kwa maslahi ya Taifa au kwa maslahi binafsi.

Hapa kuna siri kubwa, ambayo wenye kumshinikiza rais amuondoe Prof.Muhongo kwenye nafasi ya uwaziri wanaijua. Nani ambaye hajui kazi ambayo imefanywa na Prof.Muhongo kwenye wizara hiyo.

Amefanya mambo makubwa kwa maslahi ya nchi.Waziri Muhongo kwa usimamizi wake mzuri umeme umekwenda kwenye vijiji mbalimbali vya nchi yetu.

Nimezunguka wilaya za nchi hii 129 hadi sasa.Naiona kazi ambayo Prof.Muhongo ameifanya katika nishati ya umeme.

Nani ambaye hajui umuhimu wa nishati ya umeme kwa wananchi. Misimamo yake katika wizara hiyo imefanikisha ujenzi wa bomba la gesi.Angekuwa Waziri legelege , bomba la gesi kutoka Mtwara kuja(kwenda) Dar es Salaam lisingejengwa.

Alijua anasimamia maslahi ya taifa.Pia najua kwenye eneo la gesi amekasirisha wengi.Wapo ambao hawataki hata kumsikia.Leo si wakati wake kuzungumzia hilo.

Wanasiasa wanataka rais amuondoe Prof.Muhongo, hivi waziri mwingine ambaye atakwenda kwenye wizara hiyo na kukaa kwa miezi nane iliyobaki ya utawala wa rais Kikwete anakwenda kufanya jambo gani kubwa.

Kuna dhambi gani Waziri Muhongo akiachwa amalizie muda ambao Rais Kikwete ameubakisha.

Kwa kuwa tunaingia mwaka 2015, ni bora niseme ukweli maana utaniweka huru.Naamini sioni sababu ya kumuondoa Waziri Muhongo Wizara ya Nishati na Madini.

Tangu amekuwa Waziri wa Nishati na Madini Waziri Muhongo amefanya kazi kubwa na nzuri.Hata hao ambao leo wanamuandama wanajua.

Nikiri najua, haya ninayoeleza kuna watu nawakera lakini ni bora niwe huru kwenye kile ninachoamini.

Kauli ya Mwishehe, kaushauri Rais wangu, Rais Jakaya Kikwete , nakuomba umuache Waziri Muhongo amalizie kazi anayoifanya kwenye wizara hiyo.Binafsi sioni mahali ambapo Waziri Muhongo amechukua fedha za Escrow.

Sioni mahali ambapo Waziri Muhongo ameshauri fedha zitoke. Waziri Muhongo msimamo wake unajulikana wazi kuhusu fedha hizo.

Kwa bahati mbaya wanasiasa wetu wameng'ang'ania tu kumtaka rais amuondoe Muhongo badala ya kutoa suluhu ya nini kifanyike ili hayo ambayo yanatokea na kusababisha taifa kushindwa kuchukua kodi yake yasijirudie.

Wanasiasa wanashindana kuita vyombo vya habari kumshinikiza rais kumuondoa Waziri Muhongo.

Naamini na ndio ukweli wanafanya hivyo si kwasababu ya maslahi ya taifa , bali wanafanya hivyo kwa msuko mwingine. Ipo siku nitausema.Kwenye hili nitasimamia ukweli.

Kwenye siasa za Tanzania kuna mambo huwa yanakera sana. Moja ya mambo yanayokera ni pale mtu anaposimama kujifanya anapigania maslahi ya taifa kumbe, kichwani kwake anawaza tofauti.

Kuna wakati huwa najiuliza kwanini , wanashinikiza Prof. Muhongo aondolewe. Nawaza weee , lakini napata majibu tofauti tofauti. Moja ya jibu ambalo huwa nalipata ni kwamba wanaogombea urais nao wana yao kwenye hilo.

Tena si wa CCM tu, bali hata wa upinzani. Wanaona sakata la Escrow ni karata ya mwisho ya kufanikisha malengo yao.

Wengine wanaamini kupitia sakata hilo itakuwa njia rahisi ya kuiangusha Serikali ya Rais Kikwete bungeni.

Hivyo, kila mmoja analiangalia kivyake na si kweli wote wanaopigania hilo ni kwa ajili ya maslahi ya taifa. Ingekuwa ni maslahi ya taifa wangetuambia kwenye sh. bilioni 306 za Escrow za umma ziko sh. ngapi?

Nimalizie kwa kueleza tunaingia mwaka 2015, tudumishe upendo, umoja na mshikamano wetu. Najua wapo ambao watakaosema nimetumwa. Sijatumwa. Sitajali.

Kubwa zaidi kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake kwa kile anachokiamini anaweza kuchangia alau kidogo hasa kwa kuzingatia mwaka 2014 umebakisha saa chache tu wa uhai wake.

Karibu mwaka 2015, nitumie nafasi hii kuwataka mafanikio mema kwenye mwaka wa uchaguzi wanasiasa wote. Mwaka ambao kila anayetaka kugombea udiwani, ubunge au urais anarudi kuomba kura kwetu.

Nawaheshimu wanasiasa wote na wa vyama vyote. Kwenye ukweli nipo pamoja nanyi na kwenye uongo nitakuwa kando yenu.

Tuwasiliane 0713833822

SHEIKH SHARIF AZUA MAPYA YA URAIS 2015, ASEMA TANZANIA ATAKAYEPATIKANA NI ALIYEFANYAKAZI NJE YA NCHI KWA MUDA MWINGI

Sheikh Shariff Matongo  akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)kuhusu  ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.

NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII, DAR
Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo.

Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo katika uchaguzi ujao wa Tanzania kupatikana Rais ambaye ni kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.

Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa  ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na  na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh  alisema ndoto nyingine  kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata mafanikio  makubwa kwa mwaka utaoanza kesho.

Vijana wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana ihivyo wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa  itapita lakini kutakuwa na vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.

‘’Ndoto yangu  niliopoteshwa sikukaanyo peke yangu niliweza kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa wa Abuu Dhabi,Mufti wa Nigeria  na wengine wote wanakaniambia suala hilo nisikaaye nalo nishirikishe na watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff Matongo.

Sheikh Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.

Alisema ndoto hizo ni lazima kuweza kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa watu wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.

SAA 24 ZA BURUDANI DAR LIVE KUFUNGUA MWAKA 2015

Dec 29, 2014

RAIS WA TFF JAMAL MALINZI APOKEA JEZI KUTOKA KAMPUNI YA PROIN KWAAJILI YA MASHINDANO YA WOMEN TAIFA CUP.

Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza(kushoto) akimkabidhi Jezi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kwaajili ya Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa Women Cup yanayotarajiwa kutimbua vumbi tarehe 1 January 2015.
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Mkurugenzi wa makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza amkabidhi jezi Rais wa TFF, Mh Jamal Malinzi kwaajili ya michuano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa Women Cup ambayo yanatarajiwa kutimua Vumbi tarehe 1 Januari 2015 huku Mechi ya Uzinduzi ikiwakutanisha timu kutoka Mwanza na Musoma mechi ambayo itapigwa katika Dimba la CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
Kampuni ya Proin Ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya ambayo yanatarijiwa kutimua Vumbi Mnamo tarehe 1 Januari 2015. Proin Imeamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la Kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake ambapo baadae wachezaji bora wataweza kuingia katika Timu ya Taifa ya Wanawake.
Vilevile Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mh Jamal Malinzi amewataka pia makampuni mengine Kujitokeza katika Kudhamini Mashindano haya yanayotarajiwa kuanza tarehe 1 Januari 2015 kwa lengo la Kuweza kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake huku pia wakipata fursa ya Kujitangaza kibiashara kwasababu mpira wa miguu ni mchezo ambao unapendwa sana na watu wengi hivyo ni dhahiri kabisa Kuwa Makampuni mengi yakidhamini mashindano haya yataweza kufikia malengo yao kwa kujitangaza.
KAWAIDA Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza(kushoto) akimkabidhi Jezi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kwaajili ya Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa Women Cup yanayotarajiwa kutimbua vumbi tarehe 1 January 2015. Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog Mkurugenzi wa makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza amkabidhi jezi Rais wa TFF, Mh Jamal Malinzi kwaajili ya michuano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa Women Cup ambayo yanatarajiwa kutimua Vumbi tarehe 1 Januari 2015 huku Mechi ya Uzinduzi ikiwakutanisha timu kutoka Mwanza na Musoma mechi ambayo itapigwa katika Dimba la CCM Kirumba, Jijini Mwanza. Kampuni ya Proin Ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya ambayo yanatarijiwa kutimua Vumbi Mnamo tarehe 1 Januari 2015. Proin Imeamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la Kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake ambapo baadae wachezaji bora wataweza kuingia katika Timu ya Taifa ya Wanawake. Vilevile Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mh Jamal Malinzi amewataka pia makampuni mengine Kujitokeza katika Kudhamini Mashindano haya yanayotarajiwa kuanza tarehe 1 Januari 2015 kwa lengo la Kuweza kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake huku pia wakipata fursa ya Kujitangaza kibiashara kwasababu mpira wa miguu ni mchezo ambao unapendwa sana na watu wengi hivyo ni dhahiri kabisa Kuwa Makampuni mengi yakidhamini mashindano haya yataweza kufikia malengo yao kwa kujitangaza.

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WAWEKA HISTORIA DAR LIVE


(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)
UNGANA NASI KATIKA FACEBOOKTWITTER , INSTAGRAM , YOUTUBE

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

Dec 28, 2014

theNkoromo Blog, Singida
Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu

Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.

Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.

HABARI KATIKA PICHA, NYALANDU AKITANGAZA KUWANIA URAIS LEO.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo theNkoromo Blog)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
 Mwimbaji wa muziki wa Injili, Frola Nkone akiimba kutumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Mhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
Wasanii wa kikundi cha Makomandoo cha mjini Singida wakitumuiza wakati wa mkutano huo
Wadau wakifurahia burudani wakati wa mkutano huo wa Nyalandu
 Steve Nyerere ambaye ni Msanii na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.
KABLA YA MKUTANO
Nyalandu na Mkewe Faraja Kota wakiingia kwenye Kanisa la KKKT  Usharika wa Ilongelo kwa ajili ya ibada maalum. Pamona nao ni watoto wao Sera na Christopher kabla ya kwenda Uwanjani kutangaza azma yake ya kuwania Urais 2015
Nyalandu na Faraja Kota wakiwa na watoto wao Sera na Christopher katika kanisa hilo 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro  Nyalandu akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo leo
Waziri Nyalandu akiwa na watoto wake wakati wa ibada maalum iliyofanyilka leo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo Jimbo la Singida Kaskazini
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akitoa sadaka wakati wa ibada maalum iliyofanyika leo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo
Mke wa NYalandu, Faraja Kota akipita baada ya kutoa sadaka kwenye kanisa hilo la KKKT Usharika wa Ilongelo
Mwimbaji wa nyimbo za Injili lkatika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa la FPCT  katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
Waumini wakiwa katika kanisa la FPCT wakati wa ibada maalum aliyohudhuria Nyalandu leo
Nyalandu na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada maalum leo asubuhi. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog.

DC MOMBA AWATAKA WAFANYABIASHARA TUNDUMA WASIOGOPE MIKOPO

Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma. Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo TundumaMkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma. Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la TundumaBaadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma. Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo TundumaBaadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo. Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo

NYALANDU KUFANYA TAMASHA KUBWA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUTIMIZA MIAKA 15 YA UBUNGE WAKE

Dec 27, 2014

*Zaidi ya watu 20,000 kuhudhuria
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, Desemba 28, 2014 (kesho J’pili) atafanya mkutano mkubwa kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi wa Singida Vijijini na Watanzania wote kwa kutimiza miaka 15 ya ubunge.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mbunge huyo, Elia Diga, imesema kuwa mkutano huo ambao utaambatana na burudani mbalimbali, utafanyika katika Kata ya Ilongero na utahudhuriwa na viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa dini zote na wananchi zaidi ya 20,000 kutoka kata zote zinazounda jimbo hilo na zile za jirani.

Katika mkutano huo, Nyalandu atahutubia wananchi pamoja na kueleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi chote cha miaka 15.

Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana mpaka sasa, Nyalandu pia ataeleza wananchi mwelekeo mpya wa jimbo hilo na mahali anapopenda lifike.

Viongozi wote wa CCM Wilaya ya Singida wakiongozwa na mwenyekiti wake, watahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba fupi kwa wananchi.

Wasanii nyota wanaotamba nchini wakiongozwa na kundi la Makomandoo, Rose Muhando, Christina Shusho, H-Baba, Mchekeshaji Steve Nyerere na Bendi ya New Life Bandi watakuwepo kukonga nyoyo.

Pia kutakuwepo na vikundi  mbalimbali vya ngoma za asili vikiwemo Njagmba, Ilongero Group na vingine vingi vitakuwepo kutoa burudani.

NAIBU WAZIRI MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI TAMASHA LA UPENDO WA MAMA DAR

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza.


Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.

Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha.

Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi.

"...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi.

Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa.

Aisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao.

Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali.

Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.

TAMASHA LA KRISMAS LAACHA HISTORIA MJINI IRINGA LICHA YA MVUA KUBWA

1Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akimtunza Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini DRC Congo wakati akiima kwenye tamasha la Krismasi lililofamyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wakiwemo Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Bony Mwaiteje, Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo, Solomon Mukubwa, Edson Mwasabwite Joshua Mlelwa, Ambwene Mwasongwe, Tumaini Njole, Emmanuel Mgogo na wengine wengi, hata hivyo mvua kubwa iliyonyesha mkoani Iringa imewafanya mashabiki wengi kutojitokeza katika tamasha hilo, Kundi zima la wanamuziki hao limekonga nyoyo za mashabiki mjini Iringa na linatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Songea mkoani Ruvuma ambapo tamasha kama hilo litafanyika Desemba 29 kwenye uwanja wa majimaji.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA) 2Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akicheza wakati mwimbaji Faraja Ntaboba akiimba kushoto ni mwimbaji Upendo Kilahiro akishiriki kucheza. 4Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba mbele ya mashabiki wake katika tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 5Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba mbele ya mashabiki wake katika tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 6Tumaini Njole na kundi lake wakitumbuiza kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 7Tumaini Njole akitumbuiza kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 8Baadhi ya mashabiki wakicheza muziki wakati wa tamasha hilo. 9Mwibaji Upendo Kilahiro akiimba jukwaani. 10Mwibaji Upendo Kilahiro akiimba jukwaani. 11Emmanuel Mgogo akifanya vitu vyake. 12Martha Mwaipaja akiimba kulia ni mwibaji Bony Mwapiteje. 13Mwibaji Joshua Mlelwa akionyesha uwezo wake jukwaani. 14Alex Msama kushoto akiwa na John Melele 15Waimbaji Ambwene Mwasongwe na Solomon Mkukubwa wakiongoza waimbaji wenzao jukwaani wakati alipokuwa wakiimba kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 16Upendo Nkone akiimba mbele ya mashabiki wake
.17
Upendo Nkone kulia na Tumaini Njole wakicheza jukwaani.
19Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WAWEKA HISTORIA DAR LIVE

Dec 26, 2014
Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Diamond akiwachombeza mashabiki.

Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.

Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.

Mfalme Mzee Yusuf on da stage.

Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.

Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.

Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.

Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.

Platnumz akizidi kufanya yake stejini.

Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.

Diamond na Idris wakifanya yao stejini.

Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.

Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.

Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.

Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.

Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.

Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.

Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.

...Sebene time.

Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.

NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.

Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.

Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.

Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.

Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.

Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.

Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.

Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.

Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA. Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani. M(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)
ยช