.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI ASISITIZA UTENDAJI KAZI WENYE TIJA

Dec 31, 2015

JH1
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016. Baraza hilo limefanyika Desemba 31, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
JH2
Askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza wakati akitoa hotuba yake kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2016.
JH3
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa timamu kumpokea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akiwasili tayari kwa kulihutubia Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2016.
JH4
Maafisa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi aliyoitoa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
…………………………………………………………………………………………………
Na Lucas Mboje, Dar es Salaam
WATUMISHI wa Jeshi la Magereza wametakiwa kuzingatia utendaji kazi wenye tija mahala pa kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea(Business as usual).
Rai hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini, Dar es Salaam.
Jenerali Minja amewaagiza Watumishi wote wa Jeshi hilo kuhakikisha kuwa wanawajibika kwenye maeneo yao ya kazi ili kufikia ufanisi uliotarajiwa pamoja na kutumia vizuri rasilimali za Ofisi kwa manufaa yaliyokusudiwa.
“Utekelezaji wenu wa kazi za kila siku lazima uwe na tija na uendane sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ili kufikia ufanisi unaotarajiwa”. Alisema Jenerali Minja.
Aidha Jenerali Minja amezungumzia baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa Mwaka 2015 ambayo ni pamoja na kukamilika kwa Sera ya Taifa ya Magereza ambayo italiwezesha Jeshi hilo kutekeleza mpango wake wa Maboresho ya maeneo mbalimbali, kusainiwa kwa Mkataba  na Kampuni ya Poly Teknology ya China itakayojenga nyumba 9,500 za Makazi ya Maafisa na Askari, kusainiwa kwa Mkataba wa Magari 9,05 na Kampuni ya Ashok Leyland ambapo magari hayo yanatarajiwa kupokelea mapema mwakani.
Mafanikio mengine ni pamoja na Usajili wa kudumu wa Chuo cha Urekebishaji ambapo Chuo hicho kitatoa elimu stahiki ya Urekebishaji itakayotambulika ndani na nje ya Nchi, Jeshi la Magereza limepeleka Maafisa wake kwenye shughuli za Ulinzi wa Amani kwenye nchi mbalimbali zenye migogoro, Jeshi limeingia ubia na Wawekezaji mbalimbali katika miradi ya Kilimo, uchimbaji madini ya chokaa, ujenzi wa maduka makubwa(shopping Malls) katika Mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro ambapo miradi hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Jeshi.
Vilevile Jeshi limefanikiwa kuandaa Maandiko mbalimbali ikiwemo andiko la kujitosheleza kwa chakula na miradi minane ambayo miradi hiyo ikiwezeshwa inaweza kuongeza thamani za mali zinazozalishwa na Jeshi hilo.
Aidha Jenerali Minja alieleza changamoto mbalimbali ambazo Jeshi hilo linakabilianazo ambazo ni ufinyu wa bajeti, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiri, ukosefu wa zana za kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kuathiri Uzalishaji, tatizo la miundombinu ya magereza na msongamano magerezani hali inayopelekea kwa kiasi fulani kuathiri utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja ametoa Salaam za kheri ya Mwaka mpya 2016 kwa Watumishi wote wa Jeshi hilo na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala uendeshaji wa Jeshi la Magereza.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYELITI WA BARAZALA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMEDSHEIN, ATOA RISALA YA KUUKARIBI MWAKA WA 2016

4efab04e-03f8-4760-9e14-104ccf23e617
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitowa Salamu za kuukaribisha Mwaka Mpya 2016 kwa Wananchi wa Zanzibar Ikulu Zanzibar leo 31/12/2015. (Picha na Ikulu Zanzibar)

SAMATA AJIUNGA NA KRC GENK, KLABU AMBAYO ILICHEZEWA NA MASTAA HAO MAARUFU

December 30 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri wa kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta amekiri kuwa katika harakati za mwisho za kwenda kucheza soka barani katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Samatta ambaye December 30 alikiri kuwa bado hajasaini na Genk kama inavyoripotiwa ila mambo yanaenda vizuri, kama Samatta akifanikiwa kujiunga na klabu ya KRC Geng ya Ubelgiji, atakuwa katika headlines za wakali kadhaa waliowahi kuichezea timu hiyo na sasa wanatamba katika Ligi kubwa barani Ulaya. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee list ya mastaa 4 ambao wamewahi kupitia katika klabu anayokwenda Samatta.
1-  Thibaut Courtois huyu ni golikipa wa Chelsea alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2011 akitokea klabu ya KRC Genk aliyodumu nayo kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 ndio aliamua kutimkia Chelsea.
afp-532661467-e1408807653653
Thibaut Courtois
2- Kevin De Bruyne kwa sasa ni moja kati ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi kuingia katika klabu ya Man City akitokea Vfl Wolfsburg ya Ujerumani. De Bruyne aliwahi kuchezea klabu ya Genk kuanzia mwaka 2008-2012. Baada ya hapo alijiunga na Chelsea ila mwaka 2014 ndio akauzwa na klabu ya Chelsea kwenda Vfl Wolfsburg.
2BCF932900000578-3216120-The_club_s_record_signing_will_be_expecting_to_become_a_mainstay-a-45_1440951185575
Kevin De Bruyne
3-  Christian Benteke ni staa wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye asili ya Kongo. Benteke aliwahi kucheza klabu ya KRC Genk ya kwao Ubelgiji hadi mwaka 2012 klabu ya Aston Villa ya Uingereza ilipoamua kumsajili na mwaka 2015 kumuuza kwenda Liverpool.
1437625706_276577
Christian Benteke
4- Jelle Vossen huyu amecheza Genk kwa muda mrefu zaidi ya wachezaji wengine niliowataja hapo juu, Jelle Vossen amecheza klabu ya KRC Genk kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2015 ndio aliamua kujiunga na klabu Jelle Club Brugge ya huko huko Ubelgiji, ambayo pia ilishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Vossen
Jelle Vossen

NHIF WAIANZA 2016 KWA KUBORESHA HUDUMA ZAO

REN1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael Mhando akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam(Hawapo Pichani).
REN2
Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa Umma na Utafiti Rehani Athumani akiongea na Waandishi  wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu maboresho katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
REN3
Waandishi wa Habari wakifatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na  Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Leo Jijini Dar es salaam
Picha na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
……………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unategemea kuboresha baadhi ya huduma zao ifikapo 2016 ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hizo kwa wananchi.
Akiyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu Michael Mhando amezitaja baadhi ya huduma ambazo wana mpango wa kuziboresha kwa mwaka 2016  zikiwemo za kuongeza huduma ya matibabu ya moyo kwa kutumia bima ya NHIF,kutoa mikopo ya dawa,kurekebisha mfumo wa ulipaji wa baadhi ya huduma pia kubadili gharama za huduma ambazo zinalipwa kwa watoa huduma ili kuendana na hali halisi ya mfumuko wa bei.
‘’mimi binafsi nimefurahishwa na agizo la Mheshimiwa Rais  kutengeneza maduka ya dawa kila Hospitali ya Mkoa na nitakua tayari kushirikiana nao kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi’’alisema Mhando.
Naye Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa Umma na Utafiti Rehani Athumani amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili zikiwemo za kukosekana kwa dawa katika hospitali husika pamoja na tabia ya baadhi ya wanachama kugushi baadhi ya nyaraka wakati wa usajili.
Aidha,Bw. Rehani Athumani ametaja hatua itakayochukuliwa ili kudhibiti ubora wa huduma zitolewazo na mfuko huo kuwa ni kufanya ukaguzi wa kushtukiza ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama ‘Medical surveillance’ katika vituo vya matibabu ili kuona ubora wa huduma wanazotoa kwa wananchi.
Katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utahakikisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watoa huduma ambao wataongeza bei za huduma kwa wanachama wa mfuko huo na maboresho hayo  hayataathiri kiwango cha michango kinachotolewa na wanachama.

TTCL YATOWA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA VITUO VYA YATIKA DAR ES SALAAM

 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi Mlezi wa Watoto na Vijana, Stella Mwambenja wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya watoto wa kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa chakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016 kwa vituo vitatu vya watoto yatima  Dar es Salaam. Kulia ni Mlezi wa Watoto na Vijana wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede, Stella Mwambenja. 
Mmoja wa watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede cha Buguruni Malapa Dar es Salaam akitoa shukrani kwa kampuni ya TTCL baada ya kukabidhiwa msaada huo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amanda Luhanga (kulia) wakipewa historia fupi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge kwa Ofisa Mfawidhi, Ojuku Mgezi (katikati) kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge.
Sehemu ya makazi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge
Sehemu ya msaada ukishushwa kwenye Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas  (kulia) akizungumza na watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada Mlezi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. TTCL imetoa msaada wa mifuko ya Unga, Sukari, Mchele, Maharage na Mafuta ya Kupikia kwa vituo vitatu tofauti vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (katikati)  kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Temeke cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016.

KUWAIT YAMPONGEZA NAIBU WAZIRI DKT. SUSAN KOLIMBA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini,  Nassem Ibrahim Al Najib alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pongezi kwa Dkt. Kolimba kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Dec 31, 2015Balozi Al Najib akimkabidhi  Dkt. Kolimba salamu za pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa KuwaitSehemu ya ujumbe kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo kati ya  Dkt. Kolimba na Balozi wa Kuwait hapa nchini (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Batholomeo Jungu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Tahir Bakari, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri.Picha ya pamoja

WIZARA YA ELIMU YASISITIZA NI MARUFUKU KUONGEZA ADA SHULE BINAFSI KOTE NCHINI, PROFESA NDALICHAKO AAPA "KUFA NA MTU"

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojiana Elimu ya Juu, Profesa Joyce Ndalichako, ameaapa kula sahani moja na wamiliki wa shule za sekondari na msongi za watu binafsi kuongeza ada lakini mbaya zaidi kuongeza "cha juu", yaani michango ya maendeleo na majengo. "Hivi uliombaje usajili wa shule wakati huna majengo, sitaki kusikia hii kitu inaitwa michango ya majengo au maendeleo" kwenye shule za binafsi na hili nitalifanyia kazi mimi binafsi." aliapa Profesa Ndalichako muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa wa Uwaziri wa Elimu, Sayansi, Teknolijia na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Profesa Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Braza la Taifa la Mitihani, alisema, shule zote zinaziomilikiwa na serikali hazitatoza ada wala michango ya aina yoyote kwa wanafunzi wa kuanzia shule za awali hadi kidato cha nne kuanzia mwaka wa masomo 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Progesa Joyce Ndalichako
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
 
Coat of arms of Tanzania.png

KATAZO LA KUONGEZA ADA KWA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI KWA MWAKA WA MASOMO 2016
 
Waraka wa Elimu Na. 4 wa Mwaka 2008 uliweka viwango vya ada vinavyotozwa katika shule za Msingi na Sekondari za Serikali na zile zisizo za serikali. Ada iliyowekwa kwa shule za kutwa zisizo za serikali ni Tsh. 150,000/= na shule za bweni Tsh. 380,000/= kwa mwaka kwa kila mwanafunzi. Aidha waraka huo ulielekeza kwamba ongezeko lolote la ada lazima lipate kibali cha Kamishna wa Elimu kabla ya kuanza kutumika.  
Hata hivyo imegundulika kuna baadhi ya shule zisizo za serikali zimekuwa zikiongeza ada kila mwaka pasipo kupata kibali cha Kamishna wa Elimu. Utamaduni huu wa kuongeza ada kila ifikapo mwishoni mwa mwaka umekuwa ukisababisha usumbufu mkubwa kwa wazazi/walezi na hata baadhi yao kushindwa kuendelea kusomesha vijana wao katika baadhi ya shule.
Kwa tangazo hili wamiliki wote wa shule zisizo za serikali wanaagizwa kufanya yafuatayo:
1.      Kutokuongeza gharama za uendeshaji wa shule zikiwemo ada kwa mwaka wa masomo unaoanzia mwezi Januari mwaka 2016 mpaka watakapopata maelekezo kutoka kwa Kamishna wa Elimu; wale ambao tayari wameongeza gharama na ada kwa mwaka wa masomo wa 2016 bila kibali cha Kamishna wa Elimu, Wizara haitambui ongezeko hilo kwa kuwa ni batili na hivyo zimefutwa.
2.      Ada zote kwa shule zisizo za serikali zitabaki kama zilivyokuwa zimeidhinishwa na Kamishna wa Elimu.
3.      Kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Shule aliyepo Idara ya Ithibati ya Shule inayoeleza kiasi cha ada na gharama kinachotozwa kwa sasa (kabla ya mwaka wa masomo 2016) na tarehe shule ilipopata kibali kutoka kwa Kamishna wa Elimu kutoza kiwango hicho cha ada.  Taarifa hiyo ifike ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe ya tangazo hili.
Wathibiti ubora wa shule waliopo sehemu mbalimbali nchini wanaagizwa kulifuatilia suala hili kwa karibu ili kila shule itekeleze agizo hili na kutoa taarifa zilizoelekezwa katika tangazo hili. Hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa wamiliki ambao hawatatekeleza maagizo haya.  
Aidha Wizara iko katika hatua za mwisho za utafiti na kuandaa mfumo wa kielektroniki wa kutambua gharama za kumsomesha mwanafunzi katika elimumsingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na hivyo wadau mbalimbali watoe ushirikiano kwa timu za wataalamu wanaofanya kazi hii ili kusaidia katika kuukamilisha mfumo na hatimaye kuwa na ada elekezi katika maeneo mbalimbali.
IMETOLEWA NA KATIBU MKUU

WAZIRI ANGELLA KAIRUKI APIGA MAUFUKU MATUMIZI YA BARUA PEPE ZA KAWAIDA KATIKA MAWASILIANO YA SERIKALI

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri (wapili kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora . Angella Kairuki (watatu kushoto) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho jijini Dares Salaam, leo Desemba 31, 2015. (Picha na Aron Msigwa wa Maelezo)

 Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora . Angella Kairuki (kushoto) akipokelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala  jijini Dar es salaam.
Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi jijini Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Angella Kairuki (kushoto) kuhusu utendaji wa wakati kwa  ziara ya kikazi ya  Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala leo jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao, Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Angella Kairuki (kulia) mara alipotembelea kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini jijini Dar es salaam leo.
Na Aron Msigwa MAELEZO.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali  kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini.

Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua  pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu  Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali.

Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za  umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.

Katika hili ninatoa siku 60 muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa Ameeleza Mhe. Angella.

Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa Wakala hiyo kuweka mpango  wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi waliopo kazini  kwa kujenga utaratibu wa kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na utendaji wa Wakala hiyo.

Mhe. Kairuki amewataka kuwa wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA ili kuimarisha dhana ya Serikali mtandao  ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa kupitia matumizi ya TEHAMA.
Akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya  ya fedha katika kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa bei ya kawaida.

katika hili Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha


Amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata huduma hizo  mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov)  kuwa wabunifu katika kutengeneza programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata huduma.

Aidha, katika hatua nyingine ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma zote  ziweze kupatikana katika eneo moja  na kuondoa urudufu wa mifumo iliyopo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao.

Amesema kuwa Wakala hiyo inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja.

Aidha amesema kuwa Wakala ya Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali vinazingatiwa.

VIDEO: UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SDSEMBA 31, 2015

Star TV:>BOFYA HAPA

CH 10:>BOFYA HAPA
 
Azam TV:>BOFYA HAPA
 
 TBC:>BOFYA HAPA

HARUSI: MWALIMU GODFREY GODWIN KIHENGU NA MISS MARIAM BARAKA BINAGI WAUAGA RASMI UKAPERA

Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akiwafungisha ndoa Bi.Mariam Baraka Binagi (wa pili kulia) wa Rebu Tarime, Mara pamoja na Mwalimu Godfrey Godwin Kihengu (wa pili kushoto) wa Nyansurura Tarime, Mara ikiwa ni katika ibada iliyofanyika jana Desemba 30,2015 katika Kanisa Anglikana Buhemba Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Picha na BMG (Binagi Media Group)
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bwana harusi cheti cha ndoa
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bibi harusi cheti cha ndoa
Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa
Bi.Mariam Baraka Binagi (Kushoto) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu.
Bibi harusi akimlisha keki bwana harusi
Maharusi wakinyweshana Shampeni
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wachungaji
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake akiwemo mama yake mzazi pembeni ya bibi harusi
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake
Maharusi wakiwa pamoja na Wakwe zake
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wadogo zao
Bibi harusi akiingia Ukumbini siku ya Sendoff iliyofanyika juzi Desemba 29,2015
Kushoto ni bi harusi akiwa ukumbini siku ya Sendoff iliyofanyika juzi Desemba 29,2015
Bi.Mariam Baraka Binagi (Kulia) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu (Kushoto)
Kaka wa bibi harusi ambae pia ndie mmiliki wa BMG (Kushoto) akiwa pamoja na Mama Mzazi wa bibi harusi
Kaka wa bibi harusi ambae pia ndie mmiliki wa BMG (Kulia) akiwa pamoja na dada wa bibi harusi
"Tunawatakiwa Maisha Mema na Yenye Fanaka katika ndoa yenu na Mola azidi kuibariki" Zaidi BONYEZA HAPA
ยช