.

MBUNGE KAPTEN JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA JIONI HII

Feb 28, 2015

Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.
Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini 
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.


Eatv imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya Bunge ndugu Owen Mwandumbya, Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Elimu kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila bila mafanikio kwa kuwa hawakupokea simu
“mwenyezimungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

MAOFISA WA OFISI YA RAIS - UTUMISI WAKIWA KATIKA KIKAO KAZI KWA NJIA YA VIDEO (VIDEO CONFERENCE) KATI YA UTUMISHI NA MIKOA YA MTWARA, LINDI, KILIMANJARO NA DODOMA

Baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kwa kuunganisha mikoa ya Mtwara, Lindi, Kilimanjaro  na Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto), akiongoza kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara, Lindi, Kilimanjaro na Dodoma.  
Maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara, Lindi, Kilimanjaro na Dodoma. Uendeshaji wa vikao kwa njia ya mtandao umepunguza gharama na muda uliokuwa unatumika kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CCM, LEO

SIMBA SI SIFA HIYO KUICHAPA TANZANIA PRISONSMABAO 5-0 LIGI KUU VODA COM UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

Wachezaji wa timu ya Simba wakitoka kushangilia moja ya bao lao waliloifungia timu yao hiyo dhidi ya Tanzania Prison ya Mbeya, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba imeshinda mabao 5-0. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 
Wachezaji wakishangilia moja ya bao lao, waliloifungia timu yao hiyo dhidi ya Tanzania Prison ya Mbeya, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Ibrahim Ajib (kulia) wa Simba akipambana na wachezaji wa timu ya Prison wakati wa mchezo huo.
Ibrahim Ajib (kulia) wa Simba akipambana na Nurdin Chona wa timu ya Prison wakati wa mchezo huo.
Ibrahim Ajib (kulia) wa Simba, mfungaji wa mabao 3 ya Simba (Hat Trick), akiwania mpira na Nurdin Chona wa timu ya Prison wakati wa mchezo huo.
Nurdin Chona wa timu ya Prison, akimtoka Ibrahim Ajib wa Simba. 
Nurdin Chona wa timu ya Prison (kushoto), akiwania mpira na Ibrahim Ajib wa Simba.
Dan Sserunkuma wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Nurdin Chona wa Prison.
Dan Sserunkuma wa Simba, akimtoka Nurdin Chona wa Prison. 
Emmanuel Okwi wa Simba, akimtoka James Mwasote wa Prison. 
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo. 
Wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya mabao yao, waliyoifunga timu hiyo, ya Prison.
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kupata bao katika mchezo huo.  
Mashabiki wa Tanzania Prison wakizozana baada ya timu yao kufungwa mabao 5-0 na Simba katika mchezo huo. 
Emmanuel Okwi wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Nahodha wa timu ya Prison. 
Emmanuel Okwi wa Simba, Nahodha wa timu ya Prison, wakikimbilia mpira.  
Emmanuel Okwi (kushoto), akimpongeza Ramadhan Singano 'Messi' baada ya kuifungia timu yake bao la nne katika mchezo huo. 
Ramadhan Singano 'Messi' (akisujudu), baada ya kuifungia timu yake bao la nne katika mchezo huo, huku wenzake wakimuangalia. 
Ramadhani Singano, akisherehekea bao lake, aliloifungia timu yake hiyo kwa kusujudi huku mwenzake Mohamed Hussein akimnyanyua kwa ajili ya kwenda kuendelea na mchezo dhidi ya Prisons.
Ibrahim Ajib, akiwa na mpira wake aliokabidhiwa baada ya kuifungia timu yake mabao 3 (Hat Trick), katika mchezo huo. 

BLOGGERS KUKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO KATIKA PATI YA KIHISTORIA

Feb 27, 2015

 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  Mkala Fundikira,Shafia Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na Khadija Kalili.
 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
 Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

KIPINDI CHA “JICHO LETU MKURANGA” CHA REDIO UPENDO CHASAIDIA JAMII YA WENYE MAHITAJI MUHIMU MKURANGA


DSC_2663Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani akikabidhi madawati kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaam pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo sare za shule, madaftari na viatu kutokana na msaada mkubwa wa kipindi cha “Jicho letu Mkuranga” kinachorushwa kila siku na kituo cha Redio cha Upendo Media cha jijini Dar es salaam kwa kuibua changamoto hizo na kuhamasisha taasisi na wananchi mbalimbali wenye uwezo kusaidia jamii masikini na zenye mahitaji muhimu, katika picha wa pili kutoka kulia ni Frank Mbando Mkurugenzi wa Kampuni ya FIFA Flow na katikati ni Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo PLCDSC_2664Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la KKKT akikabidhi sare za shule  kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye zililzotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaamDSC_2667 
Picha ya pamoja viongozi hao wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyokabidhiwa kwa wilaya ya Mkuranga.

MWANAMKE AUAWA NA MUMEWE KWA KIPIGO NA KISHA MWILI WAKE KUFUKIWA KATIKA ZIZI LA NG'OMBE


Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.

Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.
 
Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Jenipher Peter (45). Alisema alikuwa akiishi na mume wake, Peter Mrosso (43) pamoja na watoto wao watatu. Alisema mwili wake ulifukiwa ndani ya boma la ng'ombe.
 
Kamanda alisema taarifa za mauaji ya mwanamke huyo ilitolewa baada ya jirani yake kupigiwa simu na mume wa marehemu, akimtaarifu kuwa amemuua mkewe na maiti ameifukia ndani ya boma la mifugo.

PROFESA. ANNA TIBAIJUKA AHOJIWA NA BARAZA LA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA .....MASHITAKA YANAYOMKABILI


BARAZA la Maadili ya Viongozi wa Umma, limemsomea rasmi mashitaka aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (pichani), na kubainisha kuwa kiongozi huyo anastahili kujibu mashitaka kwa kosa la kuomba na kujipatia fedha kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
Hata hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa hakukiuka maadili hayo ya viongozi wa umma, kwa kuwa fedha hizo hakuziomba kwa maslahi yake binafsi, bali kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha taasisi yake inayotoa huduma ya elimu kwa watoto wa kike wasio na uwezo lakini wenye vipaji.
 
Akimsomea mashitaka hayo mbele ya baraza hilo, Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Wemaeli Mtei alisema Profesa Tibaijuka ambaye ni kiongozi wa umma, alishawishi na kuomba fedha na baadaye kupokea Sh bilioni 1.6 kutoka kwa James Rugemalira na mkewe.
 
Aidha, Sekretarieti hiyo kupitia shahidi wake ambaye ni Katibu Msaidizi wa Idara ya Viongozi wa Siasa kutoka Sekretarieti hiyo, Waziri Kipacha, alisema kupitia Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na sekretarieti kufuatilia sakata hilo, ilibaini kiongozi huyo aliomba na kupokea fedha hizo kupitia barua aliyoandika Februari 4, mwaka 2012.
 
“Tulibaini kuwa fedha alizoomba mlalamikiwa zilitumwa kwake kupitia akaunti yake namba 00120102640201 ya Benki ya Mkombozi iliyopo St Joseph jijini Dar es Salaam,” alisema huku akikabidhi baraza hilo barua hiyo ya Tibaijuka ya kuomba fedha na taarifa za kibenki kama ushahidi.
  
Alisema pamoja na hayo, kamati hiyo pia katika uchunguzi wake ilibaini mlalamikiwa ni mmoja wa wadhamini katika Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Barbro Johansson Girls Education Trust, ambapo barua kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ilithibitisha suala hilo. Na kwamba wamiliki wa shule hiyo ndiyo wadhamini.
 
“Tumebaini kuwa mlalamikiwa alipokea kiasi hicho cha fedha na wadhifa aliokuwa nao kama Waziri, jambo lililomwingiza katika mgongano wa kimaslahi,” alisema.
 
Alisema kitendo cha mlalamikiwa kupokea fedha hizo na kuingizwa katika akaunti yake binafsi, ni kosa kwa mujibu wa masharti ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuwa viongozi wa umma hawaruhusiwi kuomba fedha au msaada au kujipatia maslahi ya kiuchumi au kumpatia mtu mwingine maslahi hayo ya kiuchumi.
 
Wakili wa Tibaijuka, Dk Rugemeleza Nshara, alidai mbele ya Baraza mteja wake hakuna kosa alilofanya, bali alitumia wadhifa alionao kama viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuomba na kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na si binafsi.
  
“Nataka kuuliza Baraza hili, ina maana juzi Waziri Mkuu, alivyoongoza uchangishaji fedha kwa ajili ya maendeleo alikwenda kinyume na maadili ya uongozi?,” alihoji.

Profesa Tibaijuka, alikiri kuomba fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo yenye lengo la kujenga shule za mfano za wasichana wenyewe vipaji kila kanda ili kukuza na kuimarisha elimu ya mtoto wa kike nchini.
 
“Huu si msaada wa kwanza, tumekuwa tukifadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia msaada tuliopatiwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye alitambua juhudi zetu na kutuunga mkono, tumechangiwa na taasisi za ndani na nje na watu binafsi, kiasi kinachohitajika kuboresha shule hizi ni dola za Marekani milioni 14 sawa na takribani Shilingi bilioni 25.2,” alisema.
 
Alisema pamoja na Rugemalira aliyetoa Sh bilioni 1.6, pia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi alichangia taasisi hiyo Sh milioni 278, ikiwemo Serikali ya Sweden iliyomaliza mkataba wake iliyochangia Sh bilioni 8.1.
 
“Sisi tuliopo kwenye taasisi hii, tunaaminiana na ni waadilifu ndiyo maana fedha nilizoomba ziliingizwa kweli kwenye akaunti yangu lakini niliziwasilisha, zilizobaki ni deni nililokuwa naidai taasisi, lakini pia nimekopa Benki M Sh bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha taasisi hii na kuweka dhamana nyumba yangu iliyopo Oysterbay. Mbona hili hamlioni?,” alihoji.
 
Wakati akijitetea, Tibaijuka aliomba akabidhi andiko lake mbele ya baraza hilo. “Nina andiko langu na naomba nilikabidhi, kabla hujafa hujaumbika, nasimama hapa leo kwa sababu tayari nimeshahukumiwa bila kusikilizwa, niliomba hata bungeni nipewe nafasi lakini nilihukumiwa kama Waziri nikavuliwa madaraka, nashangaa leo nimesimamishwa hapa kama mbunge,” alisema.
 
Alisema “mimi mpaka sasa nasema sijakiuka maadili labda wanasheria wanieleweshe kwa sababu nilisimama kama mimi wakati wa kuomba fedha na si kama waziri au mbunge, hivyo sasa naona lengo ni kunivunja moyo, kunidhalilisha, kunifanya kama mwanamke mhuni na tapeli.” Aliendelea kujitetea

"Nimekuja kujieleza ila.. Mimi siyo mwanasheria ila ukweli sina kosa na ndiyo maana nyaraka zote ambazo zipo hapa, mimi ndo nimewapa, nimekuja hapa kwa nia njema na naamini kwamba Baraza hili litanisikiliza kwa sababu ukweli ndiyo mwanzo wa maadili, lazima tupiganie haki na tupiganie ukweli.
 
“Kama mimi nimefanya kosa kusimama kuwasaidia watoto wenye vipaji ni kosa, naomba mwanasheria anieleweshe na naomba ukweli usimame maana tukienda na fitina peke yake, hatutafika. Mimi ni profesa na mchumi na ni mstaafu wa muda mrefu na nina pensheni, sina makuu, maisha yangu ni ‘simple’ (ya kawaida) huwezi kunikuta Dubai... Ila nipo tunafanya maendeleo na wananchi wangu,” alisema.
 
Hata hivyo alisema fedha anazodaiwa kuhamisha baada ya kupokea na kukatwa za kulipa deni la Benki M, zilizobaki zilikuwa ni halali yake kwa kuwa alikuwa akidai shule hivyo fedha hizo zilizobaki ni kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

“Mimi ni mchakarikaji, mtafuta fedha na kiongozi anayeshindwa kutafuta fedha kwa ajili ya watu wake hafai.
 
"Hivyo nilipolipwa milioni 117 (Shilingi), nilitoa milioni mbili nikachangia Kanisa la Makongo na nikatoa laki nne nikapeleka kanisani na milioni 10 niliitoa kwa ajili ya matumizi yangu ya kununulia mboga, “ alisema.
 
 Shahidi wa Profesa Tibaijuka ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi Paul Rupia katika ushahidi wake mbele ya Baraza, alisema fedha hizo zimetafutwa na Profesa Tibaijuka.
 
Alisema aliitaarifu bodi kwamba zipo fedha zimeingia katika akaunti yake na zinatakiwa kulipa madeni wanayodaiwa. Alisema katika kikao hicho cha kutoa uamuzi wa kugawanywa kwa fedha hizo kilichofanyika Luguruni , hakuhudhuria, ingawa alikuwa na taarifa zote za kinachoendelea.
 
Rupia alisema bodi hiyo haikumpa masharti yoyote Profesa Tibaijuka ya kumaliza kulipa madeni hayo kwa sababu hawakuona sababu ya kumfuatilia kwa kuwa walimwamini, kutokana na juhudi zake binafsi za kupata fedha hizo. Shauri hilo lilianza saa 3 na baadaye kuahirishwa kwa muda hadi saa 6.30 mchana, lilipoanza kusikilizwa tena na kumalizika saa 11.45 jioni.
 
Katika shauri hilo, Profesa Tibaijuka alitoa ushahidi kwa zaidi ya saa tatu, akilalamika kuonewa na kuhukumiwa bila kusikilizwa. Shauri hilo liliahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, kutokana na muda kutotosha. Wakili aliomba udhuru wa kwenda Marekani kwa siku 10 na Jaji Msumi alikubali.
 
Jaji Msumi alisema wajumbe watapitia shauri hilo na siku hiyo itaamuliwa, endapo hukumu itatolewa wazi au kwa uamuzi wa ndani.

ZITTO KABWE KUTANGAZA MAAMUZI MAGUMU YA KUJITOWA CHADEMA MWEZI WA TATU

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema hatma yake kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) itajulikana katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa.
Raia Mwema linafahamu kwamba tangazo hilo la kisiasa linahusu mustakabali wake wa kisiasa ndani ya Chadema, chama ambacho amekitumikia katika maisha yake yote ya kisiasa tangu akiwa mtoto wa umri wa miaka 16.
Katika mahojiano aliyofanya kwa njia ya mtandao na gazeti maarufu la Guardian la Uingereza wiki iliyopita, Zitto alisema kuna kitu kikubwa atakifanya mwishoni mwa mwezi Machi huu.
“Sijawahi kufanya kampeni yoyote kubwa ya kisiasa kupitia mtandao wa twitter katika maisha yangu ya kisiasa, lakini nataraji kuwa nitafanya hivyo katika muda wa mwezi mmoja kutoka sasa. Fuatilieni tu twitter na mtaona,” alisema Zitto pasipo kwenda kwa undani.

Gazeti hilo la Uingereza limeanzisha utaratibu mpya wa kuhoji watu maarufu kwa kutumia mtandao wa twitter (twit interview) na Zitto alikuwa mwanasiasa wa kwanza kuhojiwa baada ya kubainika kuwa ndiye anayeongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo hapa nchini.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu nini hasa anataraji kukifanya mwishoni mwa mwezi Machi kama alivyozungumza na gazeti hilo, Zitto alisema ni mapema kwa sasa kuweka kila kitu hadharani lakini wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
“Niseme kwamba kwenye mahojiano yale nilisema hivyo kweli na nakuhakikishia kuwa kuna tukio litatokea mwishoni mwa mwezi Machi. Ni tukio gani na linahusu nini bado mapema kusema.
“Ila naomba kuahidi Watanzania kuwa watafahamu kila kitu kuhusu tukio hilo wakati ukifika. Hiyo kampeni ambayo itaendeshwa kupitia mtandao wa twitter na mingineyo, itakuwa ya kisasa na ya uhakika kuliko yoyote ambayo imewahi kuendeshwa katika historia ya Tanzania, “ alisema.
Zitto alikataa kusema lolote kama tangazo hilo litahusiana moja kwa moja na kuhama kwake kutoka Chadema kwenda ACT au chama chochote kingine cha siasa hapa nchini zaidi ya kusema; “subirini”.
Kwa sasa, Zitto ni Mbunge na mwanachama wa Chadema kwa sababu tu ya zuio ambalo Mahakama Kuu kupitia Jaji John Utamwa liliweka katikati ya mwaka jana la kufukuzwa kwake ndani ya chama hicho kutokana na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.
Zitto na wenzake, Profesa Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, walifukuzwa na Chadema kwa madai ya kupanga mapinduzi ya kumng’oa madarakani Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Mwigamba na Kitila wamehamia katika chama kipya cha siasa cha ACT; Mwigamba akiwa Katibu Mkuu wa muda na mwenzake mshauri na Zitto mwenyewe amekuwa akihusishwa na chama hicho.
Akizungumzia mahojiano hayo ya Zitto na Guardian, Dk. Kitila Mkumbo alisema aliyasoma mahojiano hayo lakini akasema anayejua nini kitatokea mwishoni mwa Machi ni Zitto mwenyewe.
“Mimi kama mshauri wa ACT nasema Zitto kama mwanasiasa makini ana mawazo yake na mipango yake. Mimi nasisitiza tu kwamba kama ataamua kuja ACT basi tunamkaribisha kwa mikono yote miwili.
“Tunaamini kwamba yeye ni muumini wa dhana ya Unyerere (Nyerereism) ambayo ndiyo msingi mkuu wa sera za ACT. Kama ataamua vinginevyo, sisi pia tutamuunga mkono kwa sababu tunajua itakuwa kwa nia njema,” alisema.
Katika mahojiano hayo na Guardian, Zitto aliulizwa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu siasa na Tanzania, ikiwamo changamoto za kisiasa, hifadhi za jamii na nguvu ya mitandao ya kijamii katika siasa za hapa nchini.
Zitto alisema silaha kubwa ya maendeleo ambayo Tanzania inayo kwa sasa ni wingi wa vijana ambao alisema kama watawekewa mipango mizuri na kuwezeshwa kutumika kwa kadri ya uwezo wao, Taifa litapiga hatua kubwa.
Alisema fursa hiyo ina hatari yake nyingine kwamba chini ya asilimia 20 ya Watanzania hawana ulinzi wowote wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii, jambo alilosema ni hatari kwa mustakabali wa Taifa.
Alisema pia kwamba kwa sasa Watanzania wengi wana ufahamu wa masuala ya mitandao ya kijamii, lakini akasema idadi ya wanaoitumia ni ndogo; huku akibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa serikali hawako hata kwenye mitandao kama twitter.
Zitto ana wafuasi zaidi ya 200,000 katika mtandao wa twitter akiwa anaongoza kwa wafuasi; huku katika nchi nyingine barani Afrika wanaoongoza wakiwa marais, wanamichezo na wanamuziki maarufu kama Didier Drogba wa Ivory Coast na Wiz Kid wa Nigeria.

NDEGE YA JESHI YAANGUKA NA KUWAKA MOTO JIJINI MWANZA ......RUBANI ANUSURIKA.

 

Ndege ya kijeshi imeanguka leo uwanja wa ndege wa Mwanza na kuwaka moto wakati inatoka kaskazini mwa uwanja huo kuelekea kusini ambapo rubani wake, Peter Augustino Lyamunda, amevunjika mguu.
 
Chanzo cha ajali hiyo ni ndege (mnyama) aliyeingia kwenye moja ya  injini za ndege hiyo ilipotaka kuruka,  ikashindwa na kuanguka.

MASHINDANO YA GOFU NIC CORPORATE LUGALO CHALLENGE 2015 YAFANYIKA KESHO VIWANJA VYA TPDF LUGALO


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC  Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu  vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa na shirika la bima la taifa NIC na  linafanyika kila mwaka kuanzia tangu lilipoanzishwa  mwaka 2013 na linashirikisha wachezaji wa rika zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi mbalimbali kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la umeme. Pia wshindi wengine watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao ambazo ni meza kubwa ya ofisini, mikoba  ya akina mama, mabegi ya wanafunzi, Feni , Friji, Microwave na zawadi nyingine nyingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 5 

ALEX MSAMA ALIPIA ADA ZA WATOTO YATIMA KATIKA VITUO MBALIMBALI NCHINI

1Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuhusu malipo mbalimbali yaliyotolewa kwa vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kulipia karo za wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali nchini, Msama ameyasema hayo wakati akizunguzia maandalizi ya sherehe zakutimiza miaka 15 kwa Tamasha la Pasaka zinazotarajiwa kufanyika Aprili 7 mwaka huu jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali Kusini mwa Afrika, Ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja  na Ulaya kutoka kule nchini Uingereza wanaotarajiwa kutoa burudani katika tamasha hilo litakaloshirikisha michezo mbalimbali pia, Kushoto ni Bw. Khamis Pembe mmoja wa waratibu wa tamasha hilo. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitia jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo. 3 
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifa na taswira za picha  wakati wa mkutano huo.

AL SHAIMAR KWEIGYIR AMTEMBELEA MAJERUHI WA TUKIO LA UPORWAJI WA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI ALBINO (ALBINISM) YOHANA BAHATI


Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir,
amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi
albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.
 
Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini
Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa
wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport
Financial Services mkoani Mwanza.
Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana
nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther
ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha
yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.
 
Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi
limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau,
hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa
kuwapatia ulinzi wa kutosha.
 
Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya
Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba
kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili
kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
ยช