.

ASKOFU GWAJIMA APATA DHAMANA POLISI OYSTERBAY LEO

Mar 31, 2015

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa kwenye baiskeli ya wagonjwa wakati akitoka katika Hospitali ya TMJ Dar es Salam leo mchana kwenda Kituo cha Polisi cha Oyterbay kupewa dhamana.
Askofu Gwajima akiingia kwenye gari huku 'akiugulia' wakati akielekea kwenye kituo hicho kupewa dhamana
Baadhi ya waandishi wa habari wakitoka kituo cha Polisi Oysterbay kufuatilia 
habari hiyo.
Wachungaji wakibadilishana mawazo wakati wakimsubiri Askofu Gwajima apewe dhamana
Waumini wa kanisa hilo wakijiandaa kumpokea Askofu wao 
baada ya kupatiwa dhamana
waumini hao wakiwa kituoni hapo.
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakiwa wamelizonga gari lililombena Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Josephat Gwajima, huku wakishangilia kwa kusema Yesu, Yesu... baada ya kupewa dhamana  katika Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo mchana.
Waumini hao wakilipungia mkono gari lililomchukua 
Askofu Gwajima. Imeletwa na www.habari za jamii.com)

DK. ALECK CHEMPONDA AFARIKI DUNIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


WAZIRI LUKUVI AZUNGUMZA NA WADAU KUHUSU MPANGO WA UENDELEZAJI WA MJI MPYA KIGAMBONI

Mar 30, 2015

3
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Meck Sadiki. Sehemu ya wadau hao ni pamoja na viongozi wa taasisi za Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), madhehebu mbalimbali ya dini na taasisi za elimu na ulinzi na huduma mbalimbali zilizopo katika eneo hilo la Kigamboni.
2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam.
4
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Sellasie Mayunga akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
6
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi Sophia Mjema akizungumza wakati wa mkutano huo.
5
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi pamoja na Naibu wake Mhe. Angellah Kairuki wakimsikiliza mmoja wa wadau Bw. Nyaronyo Kicheere nje ya ukumbi wa mkutano

JENERALI MWAMUNYANGE: MAMLAKA ZA MISHENI ZA ULINZI WA AMANI ZIWE WAZI

Na Mwandishi Maalum, New York
Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amelishauri   Baraza Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa,   kuweka  bayana    na kwa uwazi mamlaka ( mandate) ambayo misheni ya kulinda Amani itapaswa kutelekeza  kule inakopangiwa kwenda.

Ametoa  ushauri huu   siku ya Alhamisi  wakati alipokuwa akitoa mchango wake kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi  ambao nchi zao zinachangia  katika operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.

Katika  mkutano huo uliokuwa wa siku moja, na kuhudhuriwa na  Wakuu wa Majeshi  na  Maafisa wa Ngazi za Juu ,kutoka nchi 108, Jenerali  Mwamunyage amesema;
“ Wakati wa utoaji wa idhini na mamlaka kwa   misheni ya   kulinda Amani,  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  linatakiwa kumwita mbwa kwa  jina lake kama lilivyo.Mbwa aitwe kwa jina lake. Elezeni bayana na  kwa    uwazi  mamlaka na idhini  za utekelezaji za ya misheni ”

Na kuongeza, “ iwekwe wazi, kama ni misheni ya kulinda Amani, basi ielezwe ni ya kulinda Amani, na kama  ni  ya matumizi ya nguvu  basi na iwe hivyo”. Amesisitiza Mkuu wa Majeshi
Amesema kwamba, kwa kutamka  jina halisi /mamlaka  ya misheni  pale inapoundwa,  Baraza Kuu la Usalama  linakuwa linapeleka ujumbe ulio sahihi kwa pande zote zinazohusika  pamoja na nini wakitarajie.

Jenerali Mwamunyage ameuleza washiriki wa mkutano huo  mkutano wa kwanza wa aina yake  kuwakutanisha Wakuu wa Majeshi zaidi ya mia moja, wakati mmoja na mahali pamoja. Kwamba, uwazi huo pia utasaidia  kuweka bayana hatua za utekelezaji  zinazofanywa  na walinzi wa amani   kwenye eneo la utekelezaji.

Vile vile Mkuu wa Majeshi ya Tanzania ameshauri pia kuwa misheni  ambayo tangu  kuundwa kwake zilikuwa na mamlaka ya kutumia nguvu,   ni vema zisiendelee kutambuliwa hivyo pale mamlaka ya misheni hiyo  yanapobadilika  kutoka matumizi ya nguvu na kuwa misheni ya kulinda Amani au jina lolote lile.

Tanzania  inawanajeshi wake katika Misheni mbalimbali  ikiwa ni pamoja na   UNAMID ( Darfur) UNFIL, ( Lebanon) MONUSCO ( DRC) na katika maeneo mengine. Vile vile Tanzania ina Polisi na  Askari Magereza ambao nao wanahudumu katika misheni mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo ambao ulifunguliwa na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na  Ban Ki Moon na kufungwa na  Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson.  Jenerali Davis Mwamunyange amesema,  mkutano kama huo unapashwa kuitishwa mara kwa mara kwa kuwa unawawezesha  wakuu wa majeshi kubadilishana uzoefu wao katika utekelezaji wa  operesheni za ulinzi wa Amani na hasa kwa kuzingatia kwamba nchi wanachama ndio wanaotoa wanajeshi wao na ndio  haswa wanaokumbana na changamoto mbalimbmali za utekelezaji wa  dhamana hiyo.

Awali akifungua mkutano huo,   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon  pamoja na kuwashukuru  Wakuu hao wa Majeshi kwa mchango wao katika eneo hilo la  ulinzi wa Amani,  amesema   operesheni  ya kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa,  licha kwa kwamba ni  dhamana inayohitajika sana  lakini pia inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Akazitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa  ni  upugufu wa raslimali fedha,  zana,  vifaa na teknolojia za kisasa lakini pia ugumu na hatari wanazokumbana nazo walinzi wa Amani, ambapo  hivi sasa mbinu za kigaidi na uvamizi kwa walinzi wa Amani ni baadhi ya changamoto na hatari wanazokumbana nazo.

Katibu Mkuu, amewataka wakuu hao wa majeshi kuongeza ushirikiano wao kwa  Umoja wa Mataifa na hasa katika kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto za kiulinzi na kiusalama ambazo duni hivi sasa inakabiliana nao.

Akaongeza kuwa   kujitokeza kwa idadi kubwa ya wakuu hao wa majeshi ya  ulinzi kushiriki mkutano  huo, kumeipa faraja kubwa  Umoja wa Mataifa.

Naye  Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson, akihitimisha mkutano huo, amewataka wakuu hao wa majeshi na serikali zao kuendelea na majadiliano  ya mchakaTo wa  kuundwa kwa majeshi ya ulinzi ya kikanda,  majadiliano ambayo  yanatakiwa kuendelea  kuelekea mkutano wa Operesheni ya Ulinzi wa Amani  utakaofanyika mwezi  Septemba mwaka huu.

     Wakuu hao wa Majeshi ya Ulinzi pamoja na kutoa mchango wa mawazo yao, pia walipata fursa ya kupata maelezo kutoka kwa  Viongozi wakuu waandamizi wanaoongoza    Idara zinazozohusu  Operesheni ya Ulinzi wa Amani.

-------------------------------------------------------
HABARI KATIKA PICHA
 " Mnatuwakilisha vema?" ndilo swali ambalo   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,  Jenerali Mwamunyange alilowauliza watanzania hawa wawili,  Afisa wa Usalama wa UN Bw. Jacob Mwashiozya na  Bw.  Joseph Msami, wa Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa walipokuwa  wakisalimiana naye na ujumbe wake  mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi
 Jenerali Davis Mwamunyange (watatu kushoto), akiwa na ujumbe wake mbele ya bendera ya Tanzania, baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Majeshi ya  Ulinzi kutoka nchi 108. Kutoka kushoto ni  Kanali Adolf Mutta, Brigedia Jenerali Luwogo, Brigedia Jenerali Kamunde,  Meja Ngh'abi, na  Luten  Kanal Itang'are
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiingia kwa staii ya aina yake wakati alipokwenda kufungua mkutano wa kwanza wa aina yake  kufanyika  katika Umoja wa Mataifa,  ambapo Wakuu wa Majeshi  ya ulinzi kutoka  nchi zaidi ya 100 walikutana kwa wakati mmoja na mahali pamoja kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu operesheni za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa.

ZITTO KABWE AZINDUA CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARECY(ACT) DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha    Akiwashukuru wanachama wote walioshiriki walio kiunga Mkono chama hicho nawaliotoka vyama vingine wakiwemo viongozi na Taasisi Mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha, akiwasalimia wanachama kwa Salam ya chama hicho 

Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe. akizungumza na wanachama Mbalimbali toka Nje na Ndani ya Dar es Salaa  katika uzinduzi wa chama hicho na kuwaomba wanachama popote walipo waipigie  Kura ya Hapana  Katiba Pendekezwa.
Kikundi cha Ngoma ya Asili ya Kutoka Kigoma kwa jina maarufu kwa Mkoa huo wa kigoma inaitwa Usambere ikitoa burudani katika uzinduzi huo
Wanachama wa chama hicho kwa makundi mbalimbali wakiingia katika ukumbi kwa nyakati tofauti
Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango wakiingia Ukumbini

Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango yenye Ujumbe tofauti wakiingia Ukumbini

Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango yenye Ujumbe tofauti wakiingia Ukumbini
Wanakikundi wa kasimbo Asili, toka Mkoa wa Kigoma Kijiji cha Nyarubanda Kataa ya Mkigo Wilaya ya Kigoma wakitoa salam ya Chama hicho wakiwa wanajiandaa kuingia kwa Nyimbo za Ali ya Mkoa wao katika Mkutano wa Uzinduzi wa Mkutano wa  Alliance for change and Transparecy (ACT)
Baadhi ya Wafuasi wa Chama hicho wakiingia Ukumbini
Msanii Afande Sele akiwa na wanachama wa Alliance for change and Transparecy (ACT) katika Picha ya pamoja kwenye Uzinduzi wa Chama hicho
Baadhi ya wajumbe na Viongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Zitto Kabwe alipo kua akizindua Mkutano wa Chama hicho(wa tatu kushoto) ni Baba wa  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.,

Msanii  wa Makomando Said Christopher akisalimia Viongozi alipopanda juukwaani na mwenzake

 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha akisalimiana na
Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe mara alipo maliza kuzungumza na wafuasi wa chama hicho

 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha akisalimiana na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Kigoma Angilikana Gerald Mpango  baada ya kuzungumza na Wanachama
Afande Sele akiwa Jukwaani akitumbuiza
Wasanii wa Kikundi cha Makomando wakitoa Burudani, kulia ni fred felix na Said Christopher
Wafuasi wa chama hicho wakijiandikisha na kupatakadi ya Uanacha
Wanachama
Mamia wajitokeza Uzinduzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Zitto Kabwe akisoma Fomu ya Chama hicho inayomtaka kila mwanachama Ngazi ya juu atangaze Mali zake
Kasimbo Asilia ikitoa Burudani katika Mkutano wa chama cha Alliance for change and Transparecy (ACT)  katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Sallam leo mara baada ya chama hicho kufanya Uzinduzi 
  Kasimbo Asili ni Kikundi cha Usambere  kutoka Mkoa wa Kigoma katika kijiji cha Nyarubanda Kataa ya Mkigo Wilaya ya Kigoma ikitoa burudani, pichani ukiona wakiruka na kupokezana kwa katika kucheza. 
Wanachama Mbalimbali wakifatilia kwa makini katika Mkutano wa Uzinduzi wa chama hicho Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Alliance for change and Transparecy (ACT)
Vikundi mbalimbali Vikitoa maigizo katika Uzinduzi wa Chama hicho
Wanachama wakijipanga wakati Viongozi wa Chama hicho Kitaifa wakitarajia kuingia katika Ukumbi wa  Diamondi Jubilee
Wanachama wakijipanga mikono wakati Viongozi wa Chama hicho Kitaifa wakitarajia kuingia katika Ukumbi wa  Diamondi Jubilee na baadhi ya wanachama wakipunga mikono kwa kuonyesha alama ya chama chao
 (kulia) akiwapungia mikono wanachama alipokua akiingia katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Sallam leo (kushoto) ni  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.

Ulipoimbwa wimbo wa Mungu Ibariki.
Wanachama wakiimba Wimbo wa Taifa
.Katibu Mkuu ACT Tanzania Samson Mwigamba akizungumza na wanachama alipokua akifafanua jambo  (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
ยช