Breaking News

Your Ad Spot

Apr 22, 2015

MAKAMU WA RAIS DR. BILAL AKABIDHI TUZO YA MCHANGIAJI BORA KWA JAMII 2014

Azindua Ripoti ya Hali ya Mazingira 2014 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi Tunzo ya ushindi kwa mchangiaji bora katika maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2014, Makamu wa Rais wa kampuni ya North Mara Gold Mine, Bw. Deo Mwanyika wakati wa ghafla fupi iliyofanyika jana usiku April 21, 2015 katika Hoteli ya Hyyat Regence Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Tunzo ya zawadi ya picha kutoka kwa waandaaji wa mashindano ya Tunzo ya mchangiaji bora katika maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2014, wakati wa ghafla fupi iliyofanyika jana usiku April 21, 2015 katika Hoteli ya Hyyat Regence Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano ya Tunzo ya mchangiaji bora katika maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2014 kutoka katika makampuni mbalimbali ya uchimbaji, wakati wa ghafla fupi iliyofanyika jana usiku April 21, 2015 katika Hoteli ya Hyyatt Regence Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na msanii wa nyimbo za injili Mbasha alipokutana nae kwenye mashindano ya Tunzo ya mchangiaji bora katika maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2014, yaliyofanyika jana usiku April 21, 2015 katika Hoteli ya Hyyat Regence Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya viongozi wa makampuni ya uchimbaji madini ambao ni washiriki wa mashindano ya Tunzo ya mchangiaji bora katika maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2014, yaliyofanyika jana usiku April 21, 2015 katika Hoteli ya Hyyat Regence Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Steven Masele alipowasili katika Ukumbi wa Jengo la Mwalim Nyerere leo April 22,2015, kwa ajili ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa waka 2014. Kushoto Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa uzindua wa Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa mwaka 2014. Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo April 22, 2015.
Viongozi na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akiwahutubia wakati wa uzindua wa Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa mwaka 2014. Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo April 22, 2015. 
 Viongozi na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akiwahutubia wakati wa uzindua wa Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa mwaka 2014. Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo April 22, 2015. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa mwaka 2014. Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo April 22, 2015. Kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushoto waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dkt. Binilith Mahenge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kopi ya kitabu cha Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa mwaka 2014. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalando mara baada ya kuzindua Ripoti hiyo leo April 22, 2015 Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, baada ya kuzindua rasmi Ripoti ya Hali ya Mazingira kwa mwaka 2014, leo April 22, 2015 Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha zote na OMR)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages