Breaking News

Your Ad Spot

Apr 16, 2015

MTANZANIA, BRIGEDIA JENERALI SARA RWAMBALI ATEULIWA KUUWAKILISHA UMOJA WA AFRIKA SUDANI YA KUSINI

Na MwandishiMaalum, New York 
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dr.Nkosanzana Dlamini Zuma, amemteua,  Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali kutoka Jeshi la Wananchiwa wa Tanzania ( JWTZ), kuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika Sudan yaKusini .
   
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewana AU na nakala yake kutumwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, makakazi ya Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali yatakuwa Juba.
   
Pamoja na uteuzi wa Brigedia Jenerali Sara Rwambali, Dr. Nkosazana Dlamini Zuma pia amewateua Madame Josephine- Charlotte Mayuma Kala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika huko Cote d’Ivoire na makazi yake yatakuwa Abidjan.
   
Wengine walioteuliwani  Madame Nyiramatama kutoka  Rwanda, anayekuwa Mkuuwa Ofisiya  AU huko Chad, makazi yake yakiwa Ndjamena  na Dr. Arvin Boolelkutoka Mauritius anayekuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya AU  katika Maziwa Makuu Burundi na makazi yake yakiwa Bujumbura.
   
Taarifa kwa vyombo vya Habari kutoka AU inaeleza zaidi kwamba uteuzi huo nisehemu ya AU ya kuhakikisha uwepo wake katika kila eneo na vile vile kuunga mkono juhudi zinazolenga katika kukuza Amani na Usalama Barani Afrika.

 “Ninatoa pongezi za dhati kwa wateuliwa ambao ni viongozi wa ngazi za juu na wenye sifa za kutukuka katika utumishi wa umma wakiwa na uzoefu mkubwa katika eneo la amani na usalama.Si jambo la ajabu kwamba wateule watatu kati ya wanne ni wanawake” anasema Dr. Zuma

Na kuongeza, “katika mwaka huu wa 2015, ambao Umoja wa Afrika umejikita katika uwezeshwaji wa wanawake.Ninayo matumaini makubwa kwamba AU na Afrika kwa ujumla itanufaika na utaalamu na uzoefu mkubwa na uwezo wa kiuongozi kutoka kwa wateuliwa hawa”.

Mwenyekiti wa Kamishna ya AU pia ametoa mwito kwa wadau wote kuwapatia ushirikiano wateuliwa hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu kwa maslahi ya Bara la Afrika, huku akitoa shukrani kwa wawakilishi ambao wanamaliza muda wao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages