Breaking News

Your Ad Spot

Apr 19, 2015

NJIA 3 MUHIMU KATIKA UJENZI WA UCHUMI WA GESI TANZANIA


Ugunduzi huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012.PICHA|MAKTABA
Na Dk. A. Massawe
YA KWANZA
Mojawapo ya njia zitakazofanikisha matumizi ya gesi yetu asilia hapa chini yawe yenye tija zaidi ni ile ya kuisambaza maeneo yote nchini kwa kuanzia na miji mikuu ya kanda au mikoa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani na kuzalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya pale pale unapozalishwa.
Kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam itakakotumika kuzalishia umeme, majumbani na viwandani ni sahihi tu kama umeme wote utakaozalishwa utatumika ndani ya ukanda wa Dar es Salaam.
Yaani, ni sehemu kidogo tu ya gesi asilia inayowasili Dar es Salaam ingebaki hapo hapo kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi ya majumbani na viwandani ndani ya ukanda wa Dar es Salaam na kitakachosalia kiendelee na safari yake hadi kanda nyingine za Tanzania kuzalisha umeme na kwa ajili ya matumizi mengine ya moja kwa moja majumbani na viwandani kuendana na mahitaji ya kila kanda.
Lengo ni kuondokana upotevu mkubwa wa umeme na gharama kubwa ya kuusafirisha umbali mkubwa kutoka kanda moja ya Tanzania hadi nyingine, pia ikizingatiwa kwamba, zaidi ya umeme, kila kanda hapa Tanzania pia inahitaji gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja majumbani na viwandani kama Dar es Salaam.
Hivyo ni kosa kuzalisha umeme wa megawati 3000 hapa Dar es Salaam kutokana na gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya matumizi ya ukanda wa Dar es Salaam na kanda nyingine zilizoko mbali na Dar es Salaam kwani njia sahihi ni kusambaza uzalishaji wa umeme utokanao na gesi asilia kote nchini kwa kusambaza gesi asilia kote nchini kwa njia ya mabomba na kufunga mitambo midogo midogo ya uzalishaji wa umeme wa gesi asilia kwenye kila kanda kuendana na mahitaji halisi ya kanda.
Hivyo, cha muhimu zaidi kwenye kufanikisha matumizi ya gesi asilia hapa nchini yawe yenye tija tosha ni kujenga miundo mbinu ya mabomba kwa ajili ya usambazaji gesi asilia kikanda kote nchini itakakozalisha umeme na kutumika moja kwa moja majumbani na viwandani kikanda kuendana na mahitaji halisi kikanda ili kukwepa upotevu mkubwa wa umeme na gharama kubwa za kuusafirisha umbali mkubwa kutoka kanda hadi kanda, huku ikizingatiwa kwamba, zaidi ya umeme, kanda zote pia zinahitaji gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja majumbani na viwandani kama Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages