.

MWANAHABARI DEOGRATIAS MONGELA ALIVYO UKACHA UKAPERA KWA KUMUOA ELIZABETH SANGA DAR ES SALAAM JANA

May 31, 2015

Kuona picha za Harusi hii, Taadhali> BOFYA HAPA

UMOJA WA MATAIFA WAWAENZI WALINDA AMANI WAKE

Na MwandishiMaalum, New York
Mashujaa Private Ally Salum Jumanne, Private Mohamed John Mbizi, Private Vasco Adrian Msigala na Sajent Hamis Juma Nyange kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ni miongoni mwa mashujaa 126 ambao Ijumaa ya Mei 29, 2015, Umoja wa Mataifa uliwatunuku medali ya Dag Hammarskjold.

 Umoja wa Mataifa umeitenga Mei 29, kuwa siku maalum ya kutambua na kuenzi mchango wa walinda Amani ambao wamepoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani kupitia operesheni za Umoja wa Mataifa.

Katika adhimisho hilo na ambalo lilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki moon, Naibu wake Jan Eliasson, na Wakuu wa Idara za Ulinzi za Umoja wa Mataifa,  jumla ya mashujaa 126 kutokanchi 38 waliopoteza maisha mwaka jana(2014) walienziwa kwa kutunukiwa medali maalum ya DagHammarskjold.

 Adhimisho hilo lilitanguliwa na uwekaji wa shada la maua kwa heshima ya mashujaa hao,  shada liliwekwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon  katika sehemu maalum ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.

 Akizungumza kwa masikitiko makubwa wakati wa hafla hiyo,  Katibu Mkuu, Ban  Ki Moon,  amesema, katika maadhimisho yote ya nayofanyika katika Umoja wa Mataifa,   hakuna adhimisho lenye kutia simanzi na ngumu kama hili la kuwakumbuka na kuwaenzi walinda amani ambao wamepoteza maisha yao wakati wakitoa ulinzi kwa watu wengine.

 “ Ninasikitika kusema kwamba,   hii ni mara ya saba mfululizo ambapo zaidi ya walinda amani 100 wamepote za maisha katika kipindi cha mwaka mmoja. Hatari wanayokumbana nayo walinda amani wetu inazidi kuongezeka kwa kasi kubwa,  kutokana na kushambuliwa na makundi ya wahafidhina na makundi ya wanamgambo wenye silaha mpaka hatari ya magonjwa ambukizi kama Ebola” amesema Katibu Mkuu.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akaendelea kusema. “ Tumekusanyika hapa kuwaenzi mashujaa wetu waume kwa wake ambao wamepoteza maisha yao wakati wakiwalinda wananchi katika maeneo hatari duniani. 

Kujitoa kwao muhanga na namna walivyo yaishi maisha yao,  wanatufanya sisi tujisikie fahari na kututia shime ya kufanyakazi kwabidii zaidi ili kudhihirisha kwamba maisha yao hayakupotea bure.

 Ban Ki Moon, awaeleza wawakilishi kutoka nchi ambazo zimepoteza mashuja wake kwamba,  operesheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa zitaendelea kuwa zenye changamoto na hatari kubwa, na cha kusikitisha ni kwamba adhimisho lililofanyika ijumaa la kuwaenzi mashujaa hao halitakuwa la mwisho.
 
“ Walinda amani wetu wanabeba jukumu zito kwa ajili yetu sote. Natoa heshima zangu kwa mashujaa na salamu zangu za pole kwa familia za mashujaa hawa” akasisitiza KatibuMkuu.

Walinda amani hao 126 na raia 19 wamepoteza maisha wakati wakihudumu  katika misheni zilizopo, Afghanistan,  Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Cyprus,  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Haiti, Mali, Masharikiya Kati, Liberia, Sudan na Sudan yaKusini.

 Pamoja na Tanzania  nchi nyingine ambazo zimepoteza mashujaa wake katika misheni mbalimbali za kulinda amani katika mwaka uliopita ni Senegal, Afrika yaKusini,  Hispania, Togo,  Rwanda, Benin,  Burkina Faso, Bangladesh, na  Burundi.

 Nyingine ni, Cambodia, Chad, El Salvador, Ethiopia, Fiji, Ufaransa, Ghana,  India, Indonesia, Kenya, Malawi, Niger,  Pakistan, Philippines, Tunisia na Zimbabwe.

Pamoja na mashujaa hao ambao ni wanajeshi, wapo pia raia 19 wakiwamo pia polisi, madaktari, watumishi na watoa misaada ya kibinadamu ambao wamepoteza maisha wakati wakitoa misaada kwa binadamu wenzao.

 Wakati Umoja wa Mataifa ukiwaenzi mashujaa hao waliopoteza maisha mwaka jana. Tayari mwaka huuwa 2015 mashujaa wapatao 49 wamekwishapoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya kuleta Amani ,utulivu na ulinzi wa raia wasio na hatia katika nchi zenye migogoro.
Kati yamashujaa 49 hao wapo Watanzania wawili.

 Jumla ya walinzi wa amani 3,300 wamekwisha kupoteza maisha tangu kuanzishwa kwa Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 1948.

HABARI KATIKA PICHA
 Mpiga  Buluji akiimba wimbo maalum wa  maombolezo kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa 126 walinda amani waliopoteza maisha  mwaka jana. shughuli za utoaji wa medali  maalum  zilitanguliwa na uwekaji wa  shada maalum la maua katika eneo ambalo limetengwa katika viunga vya Umoja wa Mataifa.  Pichani anaonekana Katibu Mkuu Ban Ki Moon akitoa salamu za heshima kwa wahanga hao anaonekana pia Naibu Katibu Mkuu  Jan Eliasson
 Katibu Mkuu Ban Ki Moon, akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Jan  Eliasson, na  Viongozi wakuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ( DPKO) muda mfupi kabla ya utoaji wa medali maalum kwa mashujaa 126 walinda amani ambao walipoteza maisha mwaka jana. katika  salamu zake Katibu Mkuu alieleza kwamba katika  maadhimisho yote yanayofanyika katika Umoja wa Mataifa, adhimisho la kuwakumbuka na kuwaenzi walinda amani ni adhimisho lenye  kutia simanzi na gumu.

 Charge d' affaires a.i  Maura Mwingira wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akiandika katika kitabu maalum,  baada ya kupokea  kwa niaba ya  familia  za mashujaa wanne wa JWTZ waliopoteza maisha wakati wakihudumu katika misheni za kulinda amani mwaka jana.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKAMILISHA MAANDALIZI UBORESHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA KWA MIKOA MINNE

Maandalizi ugawaji wa mashine kwa ajili ya kuandikisha wanchi katika daftari la wapiga kura kwa Kanda ya 5 Tano kati ya Sita yamekamilika leo Mei 29, 2015 zaidi ya Biometric Voter Registration (BVR) zipatazo 1492 zinaanza kusambazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kuanzia mapema Alfajiri Kanda ya Tano ni Mikoa ya Mara, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

ARSENAL YATWAA KOMBE LA FA KWA KUICHAPA ASTON VILLA 4-0


Mabingwa mara 12 wa Kombe la FA, Arsenal baada ya ushindi wa jana dhidi ya Aston Villa.

Arsenal wakisherehekea ubingwa wao wa FA.

Theo Walcott akiifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 40.(P.T)
Walcott akishangilia bao hilo.
Alexis Sanchez (kushoto) akipiga shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Arsenal bao la pili.
Per Mertesacker akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la tatu kwa Arsenal.
Olivier Giroud akifanya hitimisho kwa kutupia kambani bao la nne.
ARSENAL imetwaa Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley usiku huu.
Mabao ya ushindi ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya 40, Alexis Sanchez dakika ya 50, Per Mertesacker dakika ya 61 na Olivier Giroud aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao dakika ya 90.
Kwa matokeo ya jana, Arsenal wameweka rekodi ya kulichukua kombe hilo mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote wakiwa wamelitwaa mara 12.

NAIBU MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI BURUNDI ATOROKA NCHI


Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Céni) imekua ikikosolewa kwa kutokua huru. Hapa rais Nkurunziza wakati alipowasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwenye Céni, Mei 8 mwaka 2015.
Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Céni) imekua ikikosolewa kwa kutokua huru. Hapa rais Nkurunziza wakati alipowasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwenye Céni, Mei 8 mwaka 2015
Na RFI

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi unaendelea kukua siku baada ya siku, wakati ambapo maandamano yakiendelea, huku Umoja wa Mataifa ukitangaza kuwa mazungumzo ya kisiasa yamesitishwa.

Wakati huo huo naibu mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (Céni), Spes-Caritas Ndironkeye, ameitoroka nchi tangu Ijumaa jioni wiki hii, huku akiacha ameandika barua ya kujiuzulu kwenye wadhifa huo.

Taarifa ambayo bado haijathibitishwa, inasema kuwa mkurugenzi wa masuala ya utawala na fedha kwenye Tume huru ya Uchaguzi (Céni), Illuminata Ndabahagamye huenda naye pia amejiuzulu kwenye wadhifa huo.(P.T)

Ikiwa ni kweli kuwa wanawake hawa wamejiuzulu itakua pigo jingine kubwa kwa rais Pierre Nkurunziza, utawala wake na tume huru ya Uchaguzi (Céni), siku moja baada ya Kanisa Katoliki kuchukua uamzi wa kuwaondoa wajumbe wake katika mchakato mzima wa uchaguzi nchini Burundi.

Zaidi ya wajumbe 9 wa Kanisa Katoliki wamekua wakisimamia Tume huru ya Uchaguzi katika ngazi ya mkoa, na wengine kadhaa katika ngazi ya wilaya.

Itafahamika kwamba ujumbe wa Umoja wa Ulaya ulitangaza Alhamisi wiki hii kuwa umejionda kusimamia uchaguzi nchini Burundi.

Hata hivyo duru kutoka Tume huru ya Uchaguzi (Céni), zimefahamisha kwamba, kiufundi, kujiuzulu kwa watu hao hakutoathiri shughuli za tume hiyo. Lakini wadadisi wanasema ili tume hiyo iweze kupitisha maamuzi yake kunahitajika kura nne kwa jumla ya kura tano.

Hayo yanajiri wakati zinasalia siku zisiyozidi 6 ili uchaguzi wa wabunge na madiwani uliyopangwa na utawala wa Nkurunziza ukishirikiana na Céni ufanyike.

Jumuiya ya kimataifa iliomba mara kadhaa uchaguzi huo uahirishwe lakini utawala wa Nkurunziza ulikataa katu katu.

Uchaguzi wa wabunge na madiwani unatazamiwa kufanyika Juni 5 mwaka huu.

PESA NYINGI PEFROMANCE NDOGO MSIMU WA 2014/2015

rrr
Sio kila mipango huwa inaenda sawa kwenye biashara mbalimbali, hata kwenye mpira huwa inatokea. Sasa hawa ni wachezaji ambao walinunuliwa kwa pesa nyingi lakini walipofika kwenye timu zao walishindwa kuonyesha uwezo uliotegemewa. Hii listi ina wachezaji kumi  (worst transfer) ambapo list yao imepangwa kutokana na gharama zao za usajili na performance ya uwanjani.
di maria
1.ANGEL DI MARIA | Manchester United | €75 million kutoka Real Madrid
Huyu jamaa alichukuliwa kama mtu ambae anageweza kuja kuisaidia Manchester kufanya vizuri hasa akitokea kwenye timu ambayo imeshinda UEFA champions. Licha mechi chache nzuri, Di Maria ame-struggle sana ndani ya Manchester united na tetesi zinasema anaweza kutimkia PSG.

mangala
2.ELIAQUIM MANGALA | Manchester City | €40 million kutoka Porto
Ilibidi awe partner wa Vicent Kompany lakini mchezaji huyu kutoka Ufaransa ameshindwa kuonyesha uwezo wake ndani ya EPL. Ana mika 24 lakini swali ni kwamba Manchester city wataendelea kuwa na Imani nae kubaki kwenye kikosi chao.(P.T)

JUAN ITURBE
3.JUAN ITURBE | Roma | €30 million kutoka Hellas Verona
Juan Manuel Iturbe atabaki kuwa mmoja kati ya wachezaji wa gharama kubwa kuwai kuamia Roma kwenye historia. Kiasi chote hicho cha pesa lakini amecheza mara 26 na kushinda magoli 2 huku akitoa assists mara mbili tu.
THOMAS VERMAELEN
4. THOMAS VERMAELEN | Barcelona | €20 million kutoka Arsenal
Kutoka Arsenal wakati wa nyakati za mwisho kabla hata dirisha la usajili halijafungwa, lakini akiwa Barca hajaonyesha kile kilichotegemewa. Ameonekana kwenye mechi za mwisho mwisho tu za Barcelona kwenye msimu ulioisha.
falcao
5. RADAMEL FALCAO | Manchester United | Mkopo kutoka Monaco
Kulikua na shangwe baada ya mashabiki wa Manchester united kujua Falcao anasajiliwa na timu yao kwenye nyakati za mwisho za usajili. Lakini hawakujua kwamba atakuja kufunga magoli mara 4 tu kwenye michezo 26 ya EPL. Manchester wametumia zaidi ya €20m kwenye gharama za mkopo pamoja na mshahara wake kwa muda wa mwaka mmoja tu.
twlli
6. MARIO BALOTELLI | Liverpool | €20 million kutoka AC Milan
Lilikua jaribio la kutaka kuziba pengo la Luis Suarez lakini haikua rahisi kama walivyodhania. Baloteli ameshindwa kuonyesha uwezo kwenye EPL kwa msimu huu. Labda tusubili msimu ujao anaweza kuongeza kiwango
CIRO IMMOBILE
7. CIRO IMMOBILE | Borussia Dortmund | €20 million kutoka Torino
Magoli matatu kwenye mechi 24 kwa striker ambae alitegemewa kum-replace Robert Lewandowski, hakuonyesha uwezo wa kutosha kufikia hilo lengo.
DORIA
8. DORIA | Marseille | €7 million from Botafogo
Doria alikua ni mchezaji wa Brazil aliye make headline kubwa sana wakati anaamika Ligue 1 msimu huu. Lakini mambo yake yakawa ndivyo sivyo.
9. ANDRE SCHURRLE
9. ANDRE SCHURRLE | Wolfsburg | €30 million kutoka Chelsea
Zilitumika pesa nyingi sana kwa ajili ya mshindi huyu wa kombe la dunia kutoka Chelsea kwenda Wolfsburg. Tangu asepe Chelsea ameshinda goli moja tu kwenye mechi 14 alizocheza kwenye Bundesliga.
DEJAN LOVREN
10. DEJAN LOVREN | Liverpool | €25 million kutoka Southampton
Raia wa Croatia alipewa jina la Jamie Carragher mpya kwa Liverpool. Kutokana na performance yake kwa season hii iliyoisha ki uhalisia ilibi afananishwe na Djimi Traore mpya na sio Jamie Carragher
Chanzo:shaffihdauda.com

MRATIBU MKAZI WA UN NCHINI NA WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI WATEMBELEA ENEO LA MAPOKEZI YA MUDA KWA WAKIMBIZI MJINI KIGOMA

IMG_0495
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushot0) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma, eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Modewjiblog team
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katikati ya wiki wametembelea eneo la mapokezi ya Wakimbizi kutoka Burundi lililopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Walipofika katika eneo hilo la mapokezi waliojionea huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula duniani (WFP), Shirika la afya duniani (WHO) pamoja na Shirika la UNFPA linaloshughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Wakimbizi wengi waliofika eneo hilo walikuwa na afya dhoofu kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu.
Kutokana na hali hiyo baadhi yao ilibidi wapatiwe huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya makazi yaliyotengwa kwa Wakimbizi ikiwemo kambi ya Nyarugusu iliyopo katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Hata hivyo kambi hiyo ya Nyarugusu ina uwezo wa kuchukua sio zaidi ya Wakimbizi 50,000 lakini sasa ina Wakimbizi zaidi ya 48,000 kutoka Burundi na 60,000 kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo.
Aidha Waziri Chikawe alisema kuwa Serikali imetenga eneo maalum ambalo litajengwa kambi mpya itakayojulikana kama Nyarugusu B ambayo itakuwa ni mahususi kwa Wakimbizi kutoka Burundi.
Mh. Chikawe alisema kuwa kambi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu kutoka hivi sasa, ili kuwatenganisha Wakimbizi kutoka Congo na Burundi.
IMG_0457
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaoandikisha Wakimbizi wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0468
Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto) walipotembelea uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0504
Mmoja wa watoa huduma kwenye kituo cha muda cha Wakimbizi katika viwanja vya Lake Tanganyika akipuliza dawa ya kuua wadudu kwenye mifereji inayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
IMG_0512
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi waliokuwa kwenye foleni ya kupanda mabasi kuelekea kambi ya Nyarugusu kwenye makazi maalum yaliyotengwa na Serikali ya Tanzania yanayohudumiwa na Shirika linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi ya Umoja wa mataifa. Wanne kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
IMG_0440
Foleni ya Wakimbizi kutoka Burundi kuelekea kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la IOM kuwapeleka kwenye eneo maalum la kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0524
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakishuhudia baadhi ya Wakimbizi wakipakia kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM tayari kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
IMG_0525
IMG_0550
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (aliyeipa mgongo kamera kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiagana na baadhi ya Wakimbizi wanaoelekea kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutokea katika kituo cha muda cha mapokezi na huduma za afya kilichopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0475
Baadhi ya wakina mama na watoto zao wakiwa wamejipumzisha ndani ya viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0523
Wahudumu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiwapulizia dawa maalum kwenye mikono na miguu kwa ajili ya kuua bakteria kabla ya kuingia ndani ya mabasi na kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0531
IMG_0536
IMG_0563
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakielekea kutembelea mabanda mbalimbali ya huduma za afya yaliyopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika yanayotoa huduma kwa Wakimbizi wanaowasili kabla ya kupekwa kambini.
IMG_0559
Pichani juu ni baadhi ya watoto wakipatiwa matibabu ndani ya kituo cha muda kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0568
Wazazi na watoto wakiwa kwenye hema maalum, huku nwengine wakiwa kwenye dripu za kuongezewa maji mwilini.
IMG_0558
IMG_0569
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wakisafisha mikono yao na kupuliziwa dawa maalum katika viatu mara baada ya kutembelea mahema yenye wagonjwa mbalimbali Wakimbizi kutoka Burundi wanaopatiwa matibabu kwenye kituo cha muda kilichopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0578
Baadhi ya watoto wakijiliwa na kujifaraji kwa kucheza mpira katika kituo maalum cha kupokelea Wakimbi wanaotafuta hifadhi nchini Tanzania wakitokea nchini Burundi katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0581
Familia za Wakimbi wakiwa wamejipumzisha kwenye kituo cha muda katika viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0500
Sehemu ya eneo la uwanja wa Lake Tanganyika.

FERDINAND ATANGAZA KUSTAFU KUCHEZA SOKA

May 30, 2015

Beki wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Rio Ferdinand ametangaza rasmi kutundiga daluga kusakata kabumbu. Rio aliachwa na QPR baada ya klabu hiyo kuteremka daraja msimu huu.
QPR imewaacha Joey Barton, Rio Ferdinand na Bobby Zamora. Ferdinand ambaye ni nahodha wa zamani wa Uingereza kwa sasa ameamua rasmi kuachana na mchezo wa soka na kuanza maisha mapya uraiani na biashara nyingine. Rio ameiambia amesema hivi “Baada ya miaka 18 ya kusakata kabumbu kama mchezaji wa kulipwa, sasa nimeona ni muda muafaka kwangu kustaafu mchezo huu ninaoupenda zaidi.”
“Nikiwa kama mtoto wa miaka 12, niliweza kupiga mpira kule Friary Estate ambayo ipo Peckham, sikuwahi kuwa na ndoto ya kuichezea timu ya West Ham timu ambayo ndio nilianzia maisha pale. Nimewahi kuwa nahodha wa Leeds United, nimeshinda kombe la klabu bingwa Ulaya nikiwa na Manchester United na kuungana kwa mara nyingine tena na kocha wangu wa kwanza Harry Redknapp hapa Queens Park Rangers.”


“Siku zote nitaheshimu michezo 81 ambayo nimejumuika na timu ya taifa ya Uingereza, nikijivunia sana fahari hiyo. Hizi zote ni kumbukumbu ambazo kamwe hazitosahaulika katika maisha yangu.Ukianza taaluma yoyote ile kila kijana anahitaji mtu wa karibu wa kumshauri. Nilijikuta niko mikononi mwa Dave Goodwin, Meneja wa wilaya huko Blackheath na Tony Carr meneja wa timu ya vijana ya West Ham. Walinipa mafunzo mema ambayo yamedumu kwa takribani kipindi chote nilichokuwa katika mchezo wa soka. Nitaendelea kuwaheshimu daima.”

“Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Chris Ramsey, Harry Redknapp, David O’Leary na David Moyes ambao waliniwezesha katika nyakati tofauti katika maisha yangu ya soka bila ya kusahau wafanyakazi wengine katika timu ambao walionyesha kunijali kwa miaka yote. Pia wachezaji wote ambao nimewahi kucheza nao. Ningependa kutoa shukrani kwa timu iliyonisaidia wakati nikiwa nje ya mchezo huu, Jamie Moralee na kila mtu katika kipindi hiki kipya ninachokianza rasmi.”


“Kushinda makombe kwa kipindi cha miaka 13 nikiwa na klabu ya Manchester United ilinifanya nifanikiwe kila kitu nilichokuwa nikikitamani katika tasnia ya soka. Tangu utotoni mpaka wakati huu, hicho ndicho nilichokuwa nikikiwaza mara zote. Vyote hivyo sidhani kama vingewezekana bila ya kiungo muhimu kabisa ambaye ni, Sir Alex Ferguson. Upeo wake mkubwa katika macho yangu utaendelea kudumu daima. Kwa mtazamo wangu yeye ndiye atabaki kuwa kocha bora kabisa katika historia ya mpira wa Uingereza.”


“Pia ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mke wangu Rebecca na familia yangu, akiwemo mama na baba yangu kwa kujitolea maisha yote juu yangu pia faraja na ushauri wao waliokuwa wakinipa kwa kipindi chote nilichokuwa nikisakata soka”


“Na mwisho kabisa, ningependa kuwashukuru mashabiki wote katika klabu zote kwani bila yao mpira huu uliojaa utaalamu wa hali juu usingekuwepo. Nitamkumbuka kila mmoja wenu kwenye jioni hii ya siku ya Jumamosi.”

MWANAMUZIKI MWANADADA MTANZANIA MWENYE ASILI YA ITALIA KUTUMBUIZA HOTELI YA MEDITERRANEO JUMAMOSI JIJINI DAR ES SALAAMMWANAMUZIKI MWANADADA MTANZANIA MWENYE ASILI YA ITALIA KUTUMBUIZA HOTELI YA MEDITERRANEO JUMAMOSI JIJINI DAR ES SALAAM


Mwanamuziki Chantal Saroldi kutoka Italia.

 Mwanamuziki Chantal Saroldi (kushoto), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Balozi wa Italia nchini, toka Italia.

 Balozi wa Italia nchini, Luigi Sccoto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kuhusu tamasha la muziki litakalofanyika kesho Hoteli ya Mediterraneo iliyopo Kawe ambapo mwanamuziki huyo atatoa burudani.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Mediterraneo waandaaji wa tamasha hilo, Samantar Abdinur Lusuf (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni  mwanamuziki Chantal Saroldi  na Mmoja wa Wakurugenzi wa Hoteli hiyo, Alas Abdinur.
 Balozi wa Italia nchini, Luigi Sccoto (wa pili kulia), akiwa meza kuu na mwanamuziki huyo. Kulia ni mpiga kinanda wa mwanamuziki huyo Gianluca Tagliazucchi na wakurugenzi wa hoteli hiyo waandaaji wa tamasha hilo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Dotto Mwaibale

Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz kutoka  nchini Italia Mwenye asili ya Tanzania Chantal Saroldi anataraji kutumbuiza  katika Hafla maalumu ya kusherehekea Siku ya Taifa la Italia ambapo raia wa Italia waishio nchini  watajumuika pamoja kwenye viunga vya ubalozi wa Italia ili kusherehekea Siku hiyo.

Mwanamuziki  Chantal Saroldi  mwenye asili ya Italia na Tanzania  alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea kabila la Wachaga.

Chanty yupo nchini kwa ajili ya ziara maalumu ya Muziki ambapo  kesho anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya Mediterraneo ya jijini Dar esalaam na Juni 2 anataraji kutumbuiza katika  hafla maalumu inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Taifa hilo.

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto,  alisema kuwa katika kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni mwanamuziki mahiri waratibu wa sherehe hizo wamemchaguliwa kuja kutumbuiza katika hafla hiyo kwa kuwa ni nembo muhimu inayoziunganisha nchi mbili hizi za Tanzania na Italia.

Katika hatua nyingine mwanadada huyo alisema kuwa anajilaumu kwa kutojifunza lugha ya mama yake ambayo ni kiswahili, huku akibainisha kuwa mikakati ni  kujifunza lugha ya Kiswahili.

Mwanamuziki huyo amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya dhahabu katika kipengele cha uhariri na uandishi wa nyimbo ikitolewa na Disc Festival. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
ª