Meneja
wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah
Mbena akitoa maelezo ya baadhi ya vifaa (havipo pichani) wanavyotumia
katika kusafisha manispaa ya Ilala kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi (kushoto) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya
mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Dar, Said Meck Sadiq akimkabidhi cheti na kikombe kwa mmoja wa
wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd iliyopewa zabuni
ya kusafisha manispaa ya Ilala, Hawa Sindo ambao wameibuka mshindi wa
kwanza wa usafi wa mazingira mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe za
kilele cha wiki ya mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya
Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Grace Mushi kutoka
Green Waste Pro ltd.
Bi.Hawa Sindo (kushoto) akiwa na mfanyakazi mwenzake Grace Mushi ambao wote ni wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea tuzo ya mazingira.
Msanii
wa Bongo Movie nchini ambaye pia ni Balozi wa usafi na Mazingira wa
Manispaa ya Ilala 2015/2016, Mohammed Mwikongi (wa tatu kushoto) akipozi
na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd
iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala walioibuka kidedea
mshindi wa kwanza wa usafi wa mazingira mkoa wa Dar es Salaam katika
sherehe za kilele cha wiki ya mazingira duniani zilizofanyika ndani ya
viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tuzo za
mazingira kwa mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe za kilele cha wiki ya
mazingira duniani zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269