Breaking News

Your Ad Spot

Jun 7, 2015

KINANA AFUNGA KAZI MULEBA, AZURU VISIWA, MKUTANO WAKE WA HADHARA WAFURIKA MAELFU YA WANANCHI LEO

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya yeye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika kijiji cha Katunguru, wilayani Muleba leo
 Wananchi wa kijiji cha Katungulu wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowahutubia akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kukagua uhai wa CCM, mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Kijiji hicho cha Katunguru. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi katika kijiji hicho cha Katunguru
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akiwasili katika Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini, kuhutubia mkutano wa hadhara leo mchana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akiwasili katika Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini, kuhutubia mkutano wa hadhara leo mchana
 Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka  akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
  KTIBU  NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
 Uwanja wa mpira wa Muleba mjini, ukiwa umefurika wananchi wakati Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja huo
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,  akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
 Katibu Mkuu wa CCM, akikabidhi cheti kwa mmoja wa maderefa wa bodaboda ambao wameshiriki mafunzo ya kuendesha bodaboda ambayo yaliratibiwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Kinana alikabidhi vyeti hiyo katika mkutano huo wa hadhara
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini mkazi mmoja wa Muleba mjini, ambaye alikuwa na kero ambayo alitaka Chama Cha Mapinduzi kimsaidie kulitatua
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Profesa Anna Tibaijuka wakiwa na vijana wa bodaboda waliopewa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages