Breaking News

Your Ad Spot

Jun 7, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA ACHANGIA MILIONI MOJA KUSAIDIA KUUNDA UMOJA WA MSASANI JOGGING CLUB

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na wana jogging wa Kata ya Msasani Dar es Salaam leo asubuhi kwenye hafla ya kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe Msasani Jogging Club.
 Viongozi mbalimbali meza kuu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Jogging, Asia Mohamed, Katibu Msaidizi wa Msasani Jogging, Alhaji Seif Muhele, DC Makonda, Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti, Mwenyekiti wa Msasani Jogging Club, Mohamed Hassan na Makamu Mwenyekiti, Pili Ndumba.
 Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti (kulia), akihutubia katika hafla hiyo.
  Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti (kushoto), akizungumza na Kiongozi wa Msasani Jogging, Abubakar Simon.
 Wana jogging wa Msasani Club wakimsikiliza DC Makonda.


 Madaktari wa Msasani Jogging wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Swalehe Mohamed Akida na Tatu Hamisi.
 DC Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wanamsasani Jogging Club.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoki Paul Makonda akiondoka baada ya kuhudhuria hafla hiyo na kuhutubia.


Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amewataka vijana waliopo katika shirikisho la umoja wa Jogging wa Kata ya Msasani kuunda umoja ambao utawasaidia kupata fursa mbalimbali.

Makonda alitoa mwito huo wakati akizungumza na wana jogging waliopo kwenye shirikisho hilo kutoka katika kata hiyo wakati wa hafla ya kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe Msasani Jogging.

"Naomba fanyeni mchakato wa kuanzisha Kamati ya Uchumi na Mipango na muuanzishe umoja wenu uliosajiliwa, utawasaidia kupata mikopo na sisi kama serikali tutawapa kazi kama za kukusanya takataka, ulinzi na nyingine nyingi" alisema Makonda.

Alisema Manispaa ya Kinondoni imetenga zaidi ya sh. bilioni 2 kwa ajili ya vijana na wanawake fedha zitakazo tolewa kupitia makundi mbalimbali yaliyosajiliwa.

Alisema fedha hizo zipo kwa ajili ya shughuli mbalimbali na kuwa kwa awamu ya kwanza zitatolewa sh.milioni 100.

Katika kusaidia mchakato wa kuanzisha umoja huo, Makonda alitoa sh. milioni 1 na Diwani wa Kata hiyo, Christina Kirigiti alitoa sh. 300,000 papo hapo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages