Breaking News

Your Ad Spot

Jun 5, 2015

MWENYEKITI BAVICHA AWATAKA LUDEWA KUTOMPOTEZA FILIKUNJOMBE


mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  akizungumza na   baadhi ya  wananchi  wa kijiji  cha Luana waliojitokeza kuungana nae katika maendeleo ya  kuchimba mifereji ya kutolea maji katika barabara yenye urefu wa km 2  aliyowachongea

mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe  akielekea  kujumuika na  wananchi wake wa  kijiji  cha Luana  kuchimba mifereji ya kutolea maji katika barabara ya kijiji  cha Luana ambayo ameshirikiana na  wananchi hao kuichonga

Wananchi  wa Luana  wakielekea kazini pamoja na mbunge  wao.(P.T)
Wananchi  wa Luana  wazee na vijana  wakishiriki maendeleo na mbunge  wao
Wananchi  wa Luana  wakiwajibika kuchimba barabara
Na MatukiodaimaBLOG 
MWENYEKITI wa baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kijiji cha Luana  wilaya ya  Ludewa mkoani Njombe Bw Kalolo Nkwera  amempongeza mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa jitihada  zake  za uboreshaji  wa barabara za wilaya ya Ludewa  ikiwemo barabara ya  kijiji hicho yenye urefu wa kilomita 2 aliyoichonga mbunge  huyo kwa kushirikiana na  wanakijiji kwa gharama  ya  zaidi ya Tsh milioni 54.
Bw  Nkwera  alisema  kuwa  jitihada zilizofanywa na  mbunge Filikunjombe katika  wilaya ya Ludewa ni  kubwa na kila mwananchi  wa Ludewa na wasio  wa Ludewa ambao  wanafika  wilayani  humo ni mashahidi wa maendeleo ya  sasa  ya  wilaya hiyo na  wao kama  wapinzani wanatambua mchango mkubwa wa mbunge  huyo katika maendeleo hivyo hawana  sababu ya kutafuta mbunge zaidi nje ya Filikunjombe.
Mwenyekiti  huyo  wa BAVICHA alisema toa kauli  hiyo leo   wakati  akizungumza na  wanahabari  baada ya kushirikiana  na mbunge  huyo na wananchi  wengine katika shughuli  ya  kimaendeleo ya kuchimba mifereji  ya kupitisha  maji kweye barabara   hiyo mpya .
" mimi hapa  na  baadhi ya  wananchi  hapo  ambao  wamekuja  kushirikiana na mbunge Filikunjombe katika uchimbaji wa mifereji  ya  kupitisha maji katika barabara  hii ni watu  wa  upinzani kama  mimi ni mwenyekiti wa BAVICHA katika  kijiji hiki ila katika masuala ya  kimaendeleo mambo ya itikadi  za  vyama tunaweka kando na  kufanya maendeleo .......hii barabara tunapita  wote hivyo  hatuwezi kuwa  wapinzani wa maendeleo yetu"
Bw Nkwera alisema kwa kazi  iliyofanywa na mbunge  huyo katika  jimbo la Ludewa  kwa  kipindi cha  miaka 5 ni  kubwa zaidi na inaweza imezidi hata ile ya  wabunge waliokaa madarakani zaidi ya miaka 40 bila kufanya  kazi kubwa kama  hiyo ya mbunge wa Ludewa.
Hata   hivyo  alisema ili Ludewa  izidi kusonga mbele  zaidi hakuna  sababu ya wana Ludewa kufanya  siasa za maeneo mengine za kuvutana kwenye mambo ya maendeleo kwani  kufanya   hivyo  ni kujikwamisha zaidi katika maendeleo kama  ilivyo kwenye majimbo mengine ambayo wabunge  wanafanya kazi katika mazingira magumu na wafuasi  wa chama cha  upinzani hawatakiwi katika shughuli za CCM na wale wa CCM hivyo hivyo  japo kwa Ludewa kwenye mambo ya  kimaendeleo  ni wananchi  wote  na  vyama  vinawekwa kando.
Mwenyekiti   wa  serikali  ya  kijiji  cha Luana Bw David  Luoga alisema kuwa wananchi  hao kamwe hawatamsahau  mbunge  huyo kwani ameweza  kuwaharakishia maendeleo ya  kijiji hicho  kwa  kufikisha umeme na kuwatengenezea barabara   hiyo ya  Malatu - Itungi  ambayo ilikuwa haipitiki japo  inaelekea katika taasisi mbali mbali kama nyumba  za ibada, soko, Zahanati  na shule  ila serikali ya wilaya haikuona sababu  ya  kuitengeneza hadi wananchi  hao  walivyoomba  kwa  mbunge  huyo katika mkutano wao wa hadhara  uliofanyika miezi mitatu  iliyopita .
Bw Luoga  alisema  toka  nchi  ipate  uhuru wake  mwaka 1961 kijiji  hicho hawajapata barabara nzuri kama  hiyo ambayo ni barabara muhimu ambayo haikupewa umuhimu  wowote na  serikali ya wilaya ya  Ludewa.
Hivyo alisea ahsante  yao kwa  mbunge wao kwa  kuwaletea maendeleo ni  kuona wanamchagua kwa  kura  nyingi zaidi  ili kuendelea kuwa mbunge kwa vipindi vingine 15 ama  zaidi   na  kuwa kipimo chake   kilikuwa ni miaka  mitano  hii ambayo ameonyeha ufaulu  wa  zaidi ya asilimia 100 hivyo kama kijiji wananchi wameweza  kuchangishana  na  kupata kiasi cha Tsh 100,000 kwa  ajili ya kwenda  kuchukulia fomu muda  wa  kufanya  hivyo utakapofika.
Kwa upande  wake  mbunge Filkunjombe pamoja na  kuwapongeza  wananchi hao wakiwemo wale  wa Chadema ambao  walijitolea  kushirikiana  nae katika ujenzi  wa barabara   hiyo bado alimpongeza mkurugenzi  wa kampuni ya barabara  ya Boimanda chini ya mkurugenzi  wake Nicholaus Mgaya kwa  kuendelea   kuwa mzalendo na wilaya ya Ludewa kwa kujitolea  mitambo ya kuchonga barabara hiyo  bila malipo.
Alisema ni wakandarasi  wachache  sana  wazalendo ambao wanajitolea kwa wananchi kama   hivyo na  kuwa kampuni  hiyo si  tu imekuwa ikijitolea katika jamii bali ni  moja kati ya kampuni za kizalendo ambazo zinafanya kazi ya  ujenzi wa barabara kwa uaminifu mkubwa bila  kulipua kama zilizokampuni nyingine za ukandarasi ambazo hugeuza wilaya   hiyo  ya Ludewa ni shamba la bibi kwa kujenga barabara kwa kiwango  cha chini ili mradi  wachume pesa.
Mbunge Filikunjombe aliwataka  wananchi hao  wa Luana kutunza barabara   hiyo badala ya kuiharibu kwa kupitisha mifugo na  kuwa kutengenezwa kwa barabara  hiyo  kutapunguza maswali ya  wananchi katika mikutano ya hadhara kwa  wananchi hao kila mkutano kutoa  kilio cha barabara  hiyo huku akisisitisha  kuwa  kero  zipo  nyingi haziwezi  kumalizika zote kwa  wakati mmoja japo kwa kuchagua moja  moja ipo siku zitamalizika  zote .
"Leo  kikao  cha  bunge kinaendelea bungeni ila nimeona  ni vizuri kukimbia mara moja kuja  kutatua kero  hiyo ya barabara ambayo ilikuwa ikiwatesa  wananchi  wangu kwanza .....kwani  ubunge huu  ni wa  wananchi hivyo  lazima  pale ninapoweza kuwasaidia kero  zao"
Wakati   huo  huo  mbunge Filikunjombe amewapongeza wananchi  wa Luana  kwa kumchangia kiasi hicho cha pesa za  kuchukulia fomu pia kumpongeza mwenyekiti  wa  BAVICHA  kwa kujitoa kwake katika  shughuli  za maendeleo pasipo kutanguliza itikadi  za chama chake na  kuwataka  wana Ludewa kushikamana katika mambo ya kimaendeleo badala ya  kujikita katika siasa za kupinga maendeleo kama ilivyobaadhi ya majimbo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages