Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Kamishna Mkuu
Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye ameagwa leo Kijeshi Juni 04,
2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam kabla
ya kusafirishwa kwa mazishi kwao Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Mwili wa Marehemu, Kamishna Mkuu
Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa
Jeshi la Magereza tayari kwa zoezi la kuagwa Kijeshi katika Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja akiwa amesimama wakati mwili wa Marehemu
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ulipokuwa ukiwasili
katika Viwanja vya Chuo Cha Maafisa Magereza Ukonga(katikati) ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kulia) ni Inspekta
Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja akisaini katika Kitabu cha Maombolezo kabla
ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu Onel
Malisa.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa
Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini salaam mbalimbali za
rambirambi zilizokuwa zikitolewa katika hafla ya kuuaga mwili wa
Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa.
Kiongozi Mwakilishi wa Wastaafu wa
Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka
akitoa salaam za rambirambi.
Gadi Maalum ya Maafisa wa Jeshi la
Magereza kwa ajili ya paredi la kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu
Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa.
Umati wa ndugu na Jamaa waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269