Breaking News

Your Ad Spot

Jun 7, 2015

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN - NCHINI UJERUMANI ATEMBELEA HOSPITALI WURZBURG

???????????????????????????????????? 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) na ujumbe wake wakipewa maelezo na Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati  alipotembelea katika Chuo cha Afya  cha Wurzburg Nchini Ujerumani katika ziara ya kikazi .
[Picha zote na Ramadhan Othman,]
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiuliza swali wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya  cha Wurzburg Nchini Ujerumani ambacho hutoa matibabu na kufanya tafiti mbali zinazohusu maradhi ya Binadamu baada ya kupata maelezo kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipoelezea  mambo mbali mbali (kulia) Balozi Philip Marmon na (kushoto)Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya kinachotoa huduma ya matibabu  kujishuhulisha na tafiti mbali mbali za maradhi ya Binadamu akikwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani Chuo hicho  kimetoa mchango mkubwa katika kupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea katika Nchi za Magharibi.
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake wakipewa maelezo na Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati walipokuwa wakiwaangalia madaktari waliovalia vazi rasmi la kujikinga na maradhi ya Ebola  wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya  cha Wurzburg Nchini Ujerumani
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya kinachotoa huduma ya matibabu  kujishuhulisha na tafiti mbali mbali za maradhi ya Binadamu akikwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani Chuo hicho  kimetoa mchango mkubwa katika kupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea katika Nchi za Magharibi.
????????????????????????????????????
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiwa katika chakula maalum kwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati ujumbe huo ukiwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg uliposhiriki katikaTamasha la Maonesho ya Muziki na Utamaduni liliofanyika na kujumuisha Wasanii na Wanamuziki mbali mbali Afrika na Nchi nyengine Duniani ikiwemo Zanzibar,
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine akiwepo mwenyeji wake Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg  Mhe,Christian Schuehadt (kulia) katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshma yake akiwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani alipohudhuria katika Tamasha la 27 la Muziki na Utamaduni lililoshirikisha Wasanii mbali mbali na Wanamuziki wakiwemo wa Nchi za Afrika na Duniani kwa ujumla,
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa (kushoto) na Msaidizi Naibu Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg Dr.Adolf Bauer wakati wa chakula maalum cha jioni kilichoandaliwa kwa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara ya kikazi  nchini Ujerumani katika Mji wa Wurzburg alipohudhuria katika Tamasha la 27 la Muziki.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages