Breaking News

Your Ad Spot

Nov 17, 2015

ASBEA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi, (kushoto), akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wan ne wa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Mabenki ya Akiba Afrika Mashariki, (ASBEA), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulilenga kujenga mkakati wa pampoja katika kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiwekea akiba ili kuongeza kipato binafsi na taifa kwa ujumla wake. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba nchini Kenya, Anne Karanja, (kulia) na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Uganda, Stephene Mukweli.
(Picha na Mpiga Picha wetu)

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania TPB, Sabasaba Moshingi, (katikati), akiwa na Wakurugenzi watendaji wa Benki za Posta Kenya na Uganda, Anne Karanja, (kushoto), na Stephene Mukweli, wakati
akiwaarifu waandishi wa habari yaliyojiri kwenye mkutano wan ne wa Bodi ya Wadhamini ya Umoja wa Chama cha Mabenki ya Akiba Afrika Mashariki, ASBEA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha na Mpiga Picha wetu).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi, (katikati), akizungumza jambo wakati kwenye mkutano wa nne wa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Mabenki ya Akiba Afrika Mashariki, (ASBEA), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kujenga mkakati wa pampoja katika kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiwekea akiba ili kuongeza kipato binafsi na taifa kwa ujumla wake. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba nchini Kenya, Anne Karanja, (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Uganda, Stephene Mukweli. (Picha na Mpiga Picha wetu)

HABARI KAMILI

Na Mwandishi wetu
AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, amewahimiza wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye akaunti zao.

Bw. Moshingi aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kutano wanne wa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Mabenki ya Akiba wa Nchi za Afrika Mashariki, (ASBEA), uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

“Lengo la Umoja huu ni kuhamasishawananchi wan chi wanachama wa ASBEA, kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kama njia ya msingi ya kutokomeza umasikini, kimarisha uchumi na kujenga uwekezaji wenye faida katika
uchumi wa mataifa yetu.” Alisema Afisa Mtendaji huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya
Kenya, (KPOSB), Anne Karanja, na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta nchini Uganda, Stephene Mukweli, pamoja na wajumbe wengine, alisema Nchi za Afrika Mashariki bado zipo nyuma kwenye suala zima la uwekaji akiba na kutolea mfano Tanzania, ambapo alibainisha “Takriban asilimia 14 tu ya wananchi wa Tanzania ndiowanaojiwekea akiba kwenye akaunti zao, kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na asilimia 23 ambayo ndio wastani wan chi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara.” Alisema Bw. Moshingi.

Umoja huo wa ASBEA ulioanzanishwa mnamo mwaka 2001, unakusudia kupanua wigo wa wanachama wake ambapo uko kwenye majadiliano ili kuzishawishi nchi za Rwanda, Burundi na Sudani Kusini kujiunga na umoja huo.
 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya,AnneKaranja alisemaukuaji wa teknolojia umeleta changamoto kubwa katika sekta ya kibenki barani Afrika na hivyo ni wajibu wa wa ASBEA kuangalia namna bora ya kuitumia teknolojia hiyo katika kuzipeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi ili kukuza uchumi wao na nchi wanachama kwa ujumla.

Jumuiyaya ASBEA inajumla ya wateja milioni 3, wanaoweka takriban akiba ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 314 katika amana, wakijivunia utoaji huduma kupitia mawakala, magari ya kutolea huduma, matawi yaBenki na ATMs.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages