Kocha Mkuu wa timuya Taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, Charles Boniface Mkwasa amewashukuru watanzania kwa kuwapa sapoti
katika michezo miwili ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2018
nchini Urusi.
Akiongea na waandishi wa habari
leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema
pamoja na kupoteza nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya makundi
kuwania kufuzu kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018, anawashukuru
watanzania wote kwa ujumla kwa sapoti waliyowapatia.
“Tumepotezea mchezo wa mwisho
dhidi ya Algeria, wenzetu walituzidi kiufundi, uwezo wa wachezaji
binafsi ulikua chachu ya kuweza kuibuka na ushindi nyumbani kwzo, lakini
bado watanzania waishio Algeria na washabiki waliokuja uwanjani
walitusapoti katika mchezo huo” alisema Mkwasa.
“Tupo katika kipindi cha kujenga
timu, tuna vijana wengi wanaochipukia, hivyo wanahitaji muda wa kucheza
zaidi na kupata uzoefu, tuendelee kuwapa sapoti vijana hawa kwa ajili ya
kujenga kikosi bora cha baadae” ameongeza Mkwasa.
Mkwasa amewaomba watanzania
kuendelea kuwasapoti vijana, pamoja na matokeo mabaya dhidi ya Algeria,
bado kuna nafasi ya kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya kuwania
kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017.
Naye nahodha msaidizi wa Taifa
Stars, John Bocco ameishukuru TFF kwa kuwapatia huduma bora za
maandalizi na wakati wa michezo yao yote, amewashukru watanzania na
vyombo vya habari kwa kuwapa sapoti na kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono
pindi wanapokua na majukumu ya kuiwakilisha nchi katika michuano
mbalimbali.
“Matokeo ya juzi (dhidi ya
Algeria) sisi wachezaji yametusikitisha, tulikua na malengo na mtazamo
tofauti wa kupata ushindi, lakini katika mpira kuna matokeo matatu,
tumepoteza mchezo huo kikubwa ni kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo na
watanzania muendelea kutusapoti timu ya Taifa kama ambavyo mmekua
mkifanya kwa sasa” alisema Bocco.
Stars imerejea leo alfajiri
ikitokea nchini Algeria ilipokua na mchezo wa marudiano dhidi ya
Algeria, Jumanne katika uwanja wa Mustapher Tchaker mjin Bilda ambapo
ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 7 -0.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269