Breaking News

Your Ad Spot

Nov 12, 2015

MAWAZIRI WAMTESA DK.MAGUFULI.....AAPA KUFANYA MAAJABU

 *Sura mpya zatajwa kuingia Baraza jipya
122 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZIKIWA zimetimia siku sita tangu Rais Dk. John Magufuli aapishwe kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wingu zito limetanda kuhusu uteuzi wa Baraza la Mawaziri.
Wakati kitendawili cha kwanza kinatarajiwa kuteguliwa Novemba 19 mjini Dodoma, pale Bunge la 11 litakaporidhia uteuzi wa waziri mkuu anayesubiriwa kwa hamu, mtihani mwingine unabaki kwa mawaziri.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili baada ya matokeo ya ubunge kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), umebaini kuwa wabunge wengi wanapungukiwa sifa za kuweza kutumikia nafasi za uwaziri.
Hali hiyo inachagizwa na Bunge la sasa kuingiza vijana wengi zaidi tofauti na vipindi vilivyopita, ambao wengi wao wanatajwa kukosa sifa na uzoefu katika suala zima la  uongozi.
Ibara ya 51 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaeleza wazi kuwa waziri mkuu anapaswa kuwa mbunge wa kuchaguliwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages