Mrembo wa Taifa Miss Tanzania
Lilian Deus Kamazima atakabidhiwa Bendera ya Taifa na Mkuu wa Mkoa wa
DSM ikiwa ni ishara ya kumtakia kila la heri katika mashindano ya urembo
ya Dunia yatakayofanyika Sanya China tarehe 19 Desemba 2015.
Mrembo huyo ataondoka nchini
Ijumaa ya tarehe 20 Novemba 2015 na ataungana na waremboe wengine kutoka
nchi zaidi ya 120 duniani na watapiga kambi ya mwezi mmoja katika
Hotel ya Beuaty Crown Sanya China.
Miss Tanzania Lilian amekuwa katika maandalizi ya kutosha tangu achukue Taji hilo mwezi Oktoba 2014
Pamoja na mambo mengine
ameshiriki Onyesho la Mavazi la nchi za Afrika ya Mashariki
lililoandaliwa na Kampuni ya Arapapa Fashion ya mjini Kampala Uganda
mwezi Novemba 2014.
Ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Jamii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na D’salaam.
Kama Balozi wa Hospital ya CCBRT
Miss Tanzania Lilian anaondoka na ujumbe wa kupiga vita na kupambana na
matatizo ya wasichana na akina mama ya Fistula.
Mrembo huyo anatarajia kurejea nchini tarehe 20 Desemba 2015.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269