Breaking News

Your Ad Spot

Nov 21, 2015

MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA WAIOMBA SERIKALI YA DK. MAGUFULI

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena (kushoto) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.

MTANDAO wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi umeitaka Serikali ya Awamu ya Tano iliyopo chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ijenge misingi imara itakayoondoa mazingira kandamizi kwa jamii ya chini hasa kwa akinamama. Aidha umeitaka serikali kuhakikisha inasimamia ipasavyo suala zima la uwajibikaji na kupambana na vitendo vya kifisadi ambavyo ndivyo vinavyowakandamiza wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na jopo la viongozi wanaounda mtandao huo likiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Mtandao, Profesa Ruth Meena walipokuwa wakitoa tathmini juu ya mtazamo wa mtandao huo baada ya Uchaguzi Mkuu na suala zima la usawa wa jinsia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi alisema serikali ya awamu ya tano ina kila sababu ya kumjali mwanamke na kutambua kuwa anamchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi.
Alisema Serikali hainabudi kujenga misingi imara ya uwajibikaji wa kweli na kutambua makundi mbalimbali ya jamii kwa jinsia zote. “…Tunataka haki yetu iwe haki kweli kweli na itambulike huku ikiwa nautekelezaji wa vitendo na kwa uhakika,” alisisitiza Bi. Rusimbi.
Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania akisisitiza jambo kwenye mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi na  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.

Alisema kuwa wangependa kushuhudia idadi ya kutosha ya wanawake inaingia katika ngazi mbalimbali za uongozi na vyombo vya maamuzi ili waweze kuingiza changamoto zao na kuzisemea ipasavyo kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake Prof. Meena akizungumzia mtazamo wa mtandao baada ya Uchaguzi Mkuu juu ya ushirikishwaji wa wanawake katika kugombea nafasi anuai za uongozi alisema bado kuna changamoto kubwa kwa kundi hilo kwani kulingana na matokeo ya sasa Tanzania itafikia usawa wa 50/50 mwaka 2055.
Alisema licha ya ongezeko la fursa ya vitimaalum kupandishwa hadi kufikia asilimia 40 bado fursa hizo zinachangamoto kubwa kwani viti hivyo ndani ya vyama hutolewa kwa wanawake kama aina fulani ya zawadi jambo ambalo huwazuia wanawake hao kusimamia ajenda zao za msingi kwa kuhofia kuonekana wasaliti. “…Viti hivi maalum hutolewa na vyama na vyama ndio vyenye ushawishi na misimamo hivyo wanawake hawawezi kusimamia hoja zao ipasavyo…,” alisema Prof. Meena.
Aidha Profesa Meena alivitaka vyombo vya habari kusaidia kubeba ajenda za wanawake na kukemea mfumo dume ili kuibadili jamii ambayo bado inamtazamo hasi juu ya wanawake na uwezo wao. Alisema wanawake walijitokeza kwa wingi katika uchaguzi huu licha ya kwamba ndani ya vyama vyao bado kuna aina fulani ya ugumu katika kuwapa nafasi kundi hilo.
Naye Mjumbe wa Mtandao huo, Dk Ave-Maria Semakafu aliitaka serikali kuendelea kuondoa vikwanzo na changamoto mbalimbali katika jamii ambazo bado zinamtesa mwanamke. Alisema huduma za elimu bado mtoto wa kike anachangamoto jambo ambalo linamnyima kufikia malengo yake huku huduma nyingine za maji na utafutaji wa nishati ya kuni ikiwa ni mzigo kwa mwanamke.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini Dar es Salaam.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages