Breaking News

Your Ad Spot

Nov 20, 2015

MTANGAZAJI PRINCE KAMKURU AFARIKI DUNIA

kamkuru new
Prince Baina Kamkuru enzi za uhai wake.
Mtangazaji wa zamani wa Radio Free Afria (RFA), Clouds FM na Star TV, Prince Baina Kamkuru amefariki dunia ghafla jana usiku akiwa jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu kifo cha marehemu Kamkuru zinaeleza kuwa alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya viungo na alipokuwa akiwahishwa hospitali kwa matibabu alifariki dunia.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda mkoani Kagera kwa mazishi siku ya Jumapili na kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages