Na Jacquiline Mrisho- Maelezo
Wachimbaji wadogo wadogo waliofukiwa katika mgodi wa Nyangalata ulioko wilayani Kahama wamepatikana wakiwa hai.
Hayo yamesemwa na msemaji wa Wizara ya
Nishati na Madini, Bi. Badra Masoud alipokua akiongea na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam kuwa wachimbaji hao walikaa kwa muda wa
siku 41 kuanzia tarehe 5, oktoba hadi tarehe 15, novemba 2015.
Msemaji huyo amewataja wachimbaji hao
waliookolewa wakiwa hai ni Muhangwa Amosi, Joseph Bulule, Chacha
Wambura, Msafiri Gerald na Onyiwa Aindo ambao mpaka sasa wako katika
Hospital ya wilaya ya Kahama wakiendelea na matibabu kwakua hali zao
hazikuwa nzuri.
Aliongeza kuwa mmoja kati ya wachimbaji hao
Bw. Musa Supana alifariki dunia siku 15 zilizopita na mwili wake bado
haujaonekana hivyo uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na wachimbaji
wadogowadogo wanaendelea kuutafuta mwili huo.
Aidha, Bi. Badra aliongeza kuwa wachimbaji
hao waliishi maisha ya shida kwa kula magome ya miti na kugawana maji
kidogo yaliyokua yakidondoka.
Hata hivyo Wizara inatoa ruzuku na mikopo
ili uchimbaji uwe wa kisasa na kutoa wito kwa wachimbaji wachimbe kwa
kutumia nyenzo za kisasa na kuwa makini katika shughuli za uchimbaji.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269