Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na katibu Mkuu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Jumanne
Sajini baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya TAMISEMI jijini Dar es
salaam kuzungumza na watumishi Novemba 24, 2015.
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi
baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam kuzungumza na
wafanyakazi Novemba 24, 2015.
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watumishi wa
Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) jijini Dar es salaam Novemba 24, 2015.
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es slaam baada ya kuzungumza nao Novemba 24,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)
WAZIRI
MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu
wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) wapate nakala ya
hansard ya hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la
11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.
“Katibu
Mkuu hakikisha umepata hansard ya hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati
akizindua Bunge na uhakikishe kila mkurugenzi ana nakala na kila mmoja
wenu lazima ahakikishe anafanyia maeneo ambayo Mheshimiwa Rais
ameyaainisha. Ni lazima tuelewane ni nini tunapaswa tufanye,” alisema.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Novemba 24, 2015) wakati akizungumza na
wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI) kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya TAMISEMI, barabara
ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.
“Ninatamani
kuona mabadiliko ya utendaji kazi Serikalini katika kipindi kifupi.
Natamani kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa huku chini. Ni nyote
ni wataalamu, kwa hiyo mnapaswa kudhirisha elimu yenu na ujuzi
mlionao,” aliwasisitizia Wakurugenzi hao.
Alisema
kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na
ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi
matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye
Serikali ya Awamu ya Tano. “Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni
field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie
watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,”
alisisitiza.
“Mambo
ninayotaka mhimize watendaji waliopo chini yenu ni pamoja na haya
yafuatayo: muda wa kuripoti kazini uzingatiwe, muda wa kukaa kazini
uzingatiwe, utokaji kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana
udhibitiwe, na mipango na malengo ya kazi kwa siku ni lazima yafikiwe,”
alisema.
“Tunataka
kujua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia ofisini. Suala siyo kukaa
tu ofisini, kwani kuna mtu anakaa ofisini, hajaenda hata kunywa chai
lakini ukiuliza amefanya nini hupati jibu la kueleweka. Sisi kama
vongozi wao ni lazima tujue wanafanya kazi gani wanapokuwa maofisini,”
alisisitiza.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitisha kikao ofisini kwake kesho
saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi
yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa. “Kesho saa 4 asubuhi
Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka
kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini
yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa
nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.
“Ninataka
kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es salaam,
wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri.
Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,” aliongeza.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa
TAMISEMI, Katibu Mkuu wa OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alimweleza
baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo
katika utendaji wake wa kazi.
Kuhusu
ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji wa
masomo ya sayansi, Bw. Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka kutoka
247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161 mwaka 2014/2015. Pia alisema vyumba
4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.
Kuhusu
utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama wazee na
watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu Mkuu
alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na kufikia
7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269