.

MTAA WA GONGO LA MBOTO MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDELEA KUUNGA MKONO KAULI YA RAIS DK.MAGUFULI YA KUFANYA USAFI

Jan 31, 2016

 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Kazi ya usafi ikiendelea.
 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
 Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
 Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
 Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.

Alisema lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi kwa wananchi wa eneo hilo.

Shingo alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi ambapo wamegawa maeneo  na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.

Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika mtaa huo Ali Mwinyimkuu  Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu waliojiwekea.

Alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.


TANROAD YA BOMOA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKA HIFADHI YA BARABARA MAENEO YA BUZA, LUMO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana. Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.
 Wakazi wa Buza Sigara wakiondoa mabaki ya mbao baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), kubomoa nyumba hizo.
 Kijana akipita jirani na nyumba iliyobomolewa.
 Mkazi wa Buza akiondoa mabaki ya mbao baada ya nyumba yake kubomolewa.
 Moja ya nyumba iliyobomolewa.
 Wananchi wakiangalia moja ya Baa iliyobomolewa.
 Tingatinga likiwa kazini.
 Watoto wakiangalia zoezi la ubomoaji lilivyokuwa likiendelea.
 Ofisa wa Tanroad akisimamia ubomoaji huo.
 Wananchi wakiangalia zoezi la ubomoaji.
 Tingatinga likiisambaratisha moja ya nyumba iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara eneo la Buza kwa Lulenge.
 Wananchi wakiangalia  ubomoaji huo.
 Tingatinga likifanya vitu vyake bila huruma.
 Askari wa kutuliza ghasia wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA AISHUKURU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, WANANCHI WA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

DC. Paul Makonda
Mnamo tarehe 23 wilaya yangu iliamua kufanya upimaji wa bure wa magonjwa ya moyo, upimaji ambao niliamini ungebeba faida kubwa nne: moja, kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara miongoni mwa wananchi, pili kubaini watu ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, tatu kuchukua hatua za awali za kuwasaidia wale ambao tayari wameshashambuliwa na magonjwa hayo na mwisho kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yote ya moyo. 
Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa unaoweza kuzalisha magonjwa mengi sana na kama hujafanya vipimo sahihi ni rahisi kushughulika na matokeo ya ugonjwa huku ukiacha chanzo kikizaa magonjwa mengine. Mathalani, unaweza kujikuta unahangaika na kuvimba kwa miguu au kuhangaika na macho ama figo aukisukari na hata kupoteza nguvu za kiume ukifikiri ndio tatizo kumbe tatizo la msingi ni moyo. 
Kimsingi ni kwasababu hizo nilizozianisha nilichukua hatua ya kukiomba taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kinachosimamiwa na Profesa Janabikinisaidie kutoa huduma hiyo bure ndani ya wilaya yangu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana madaktari kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na mwananyamala kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu kulifanya zoezi hilo. zoezi ambalo lilikuwa kubwa na zito kwani kwa makadirio ya awali tulitegemea kupata watu wasiozidi 2000 ila badala yake walijitokeza wananchi zaidi ya 7000 ila kutokana na umahiri wa madaktari hao tuliweza kuhudumia zaidi ya wananchi 5900 ingawa tulilazimika kulifanya zoezi hilo kwa siku ya pili yake ambayo ilikuwa ni tarehe 24. 
Na kwa watu wengine zaidi ya 1200 waliokuwa wamebaki, zoezi lao tulilipanga na kulifanya tarehe 30 ya mwezi huu huu wa kwanza. Ukweli ni kwamba, mambo mengi yalijitokeza kwa siku hizi tatu za upimaji; wapo waliolazimika kukimbizwa kwa ambulance kuelekea hospitali za mwananyamala na muhimbili, wapo waliolazimika kupewa appointments za kuwaona madaktari, wapo waliopewa ushauri wa matumizi ya dawa na wengine kubadilishiwa dawa sambamba na maelekezo ya utumiaji wa chakula na ufanyaji wa mazoeziili kupunguza uzito. 
Nichukue tu fursa hii kuwapongeza wanakinondoni kwa kuitikia wito na kuniamini mkuu wao wa wilaya na serikali yangu kwa ujumla kwamba tuna nia njema na tunawapenda wananchi wetu kwa kuwahakikishia afya zao zinastawi na kuendelea kuwa bora siku zote. 
Kutokama na maelezo niliyoyatoa hapo juu sambamba na sababu zilizonisukuma kufanya zoezi hilo na kutokana na muitikio mkubwa wa wananchi bila kusahau matokeo ya vipimo vilivyofanyika na kupata majibu ya kwamba watu wengi wanahitaji matibabu, kubadilishiwa dawa, maelekezo ya matumizi sahihi ya vyakula pamoja na mazoezi nimefanya uamuzi wa kulifanya zoezi hili la kudumu na tayari nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na nimetafuta njia na utaratibu bora zaidi wa kulifanya zoezi hili kuwa ni zoezi la kudumu.
Sasa basi, natamka rasmi kuwa serikali ya wilaya ya kinondoni inaanza utaratibu wa kupima bure mara tatu kwa mwaka, utaratibu ambao utaanza katikati ya mwezi wa nne. Zoezi hili litafanyika kwa kupima zaidi ya magonjwa kumi ikiwemo yafuatayo: moyo, kisukari, kansa, macho, figo, meno, kifua kikuu (TB), typhoid, magonjwa ya ngozi, presha, animonia, kansa ya kizazi, kansa ya matiti, mabusha na matende. 
Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na kila hospitali itatoa vitengo viwili au vitatu na utaratibu utakuwa hivi. Kwa mfano, utakuta banda limeandikwa Jakaya Kikwete Cardiac Institute ndani ya banda hilo utakuta madaktari waliobobea kwenye upande wa moyo na upimaji wa presha kwahiyo mtu anayetaka kupima moyo ama presha atakwenda moja kwa moja kwenye banda husika. 
Ama unaingia kwenye banda limeandikwa Ocean Road hospital kwahiyo yeyote anayetaka kupima kansa ataingia humo…hivyo hivyo kwa magonjwa mengine yote: kutakuwa na mabanda tofauti yaliyoandikwa ni hospitali gani na wanapima magonjwa gani, lengo ikiwa ni kumpa urahisi mpimaji atakayejitokeza. 
Mwisho ila si kwa umuhimu niwashukuru sana wananchi wote wa wilaya nyingine na wale waliotoka mikoa mbalimbali ikiwemo Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi na Dodomakwa imani yao kubwa juu ya tukio hili iliyowafanya kutoka mbali na kujisogeza mpaka viwanja vya leaders wakiwa na imani ya kupatiwa huduma hata kama zoezi hili lilikuwa limewalenga wakazi wa wilaya ya Kinondoni. 
Sambamba na kuwashukuru wananchi niwashukuru pia waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari mbele kulitangaza tukio na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kwa wakati. 
Imetolewa na:- Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda

WACHINA WAISHIO NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MWAKA MPYA 2016 “NGEDERE”

np1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni mshereheshaji aliyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
np2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
np3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
np4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
np5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere”
np7
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
np8
np9 np11
Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
np12 np14
Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere”
np15 np16
Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akichanganya tiketi za bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere”
np17
Vimulimuli vy fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Jumuiya ya Wachina wanaoishi nchini wamezindua na kuukaribisha kwa shamrashamra mwaka Mpya wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Akizindua shamrashamra hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alisema kuwa Wachina na Watanzania ni ndugu ambao uhusiano wao ni wa kudumishwa milele na milele.
“Uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria ambao ni wa muda mrefu katika mambo mbalimbali ikiwamo kijamii, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni Utamaduni na kimawasiliano kati ya nchi hizi mbili” alisema Waziri Nape.
Kihistoria, uhusiano wa China na Tanzania ni wa kidugu na kirafiki wakati wote iwe wa dhiki au faraja katika maisha ya kila siku kati ya Watanzania na Wachina.
Ni wakati muafaka kuongeza jitihada za kuimarisha uhusiano na ushirikiano wan chi hizo mbili ili kuwaenzi waasisi wa ushirikiano huo ambao ni Rais Mwalimu Julius Nyerere  na Mao Tse Tung.
Kwa upande wake Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei alisema kuwa wanajisikia faraja wakati wote wanapofanya kazi na Watanzania kwa kuwa wanamengi ya kujivunia katika historia ya nchi hizo.
Aidha, shamrashamra za mwaka mpya wa Kichina zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu Salum Ahmed Salum, Mizengo Pinda, viongozi mbalimbali na wenyeji wa sherehe hizo ambao ni raia wa Kichina wanaoishi nchini wakiongozwa na viongozi kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Mwaka huu unajulikana kama “Ngedere” wakati mwaka 2015 ulijuklikana kama “Kondoo” ambapo maadhimisho ya Mwaka Mpya wa “Ngedere” yalipambwa na michezo mblimbali ikiwemo bahatinasibu, sarakasi, nyimbo, muziki wa ala, mazingaombwe na ngoma.

LOWASSA USO KWA USO NA MAJALIWA, WAKUTANA KWENYE IBADA MAALUM YA KUMUWEKA KAZINI ASKOFU WA KKKT, JIMBO LA KILIMANJARO


Waziri MkuuKassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016

Baadhi ya waalikwa  walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu  Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU MKAPA NYUMBANI KWAKE MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akipeana mikono na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Dkt. Magufuli alikwenda kumsalimia. (Picha na Ikulu)

MAJALIWA AHUDHULIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI ASKOFU MKUU WA KKKT MJINI MOSHI, AKUTANA NA LOWASSA

 Waziri MkuuKassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi leo, Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu  Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016
Baadhi ya waalikwa  walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016
ยช