.

Feb 29, 2016

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUTAFUTA WAWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR’AN TUKUFU.

bil1
Makamu wa Rais mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Picha na Mafoto Blog
bil2
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar . Picha na Mafoto Blog
bil3
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, Ibrahim Omary, aliyepata pointi 90 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. Picha na Mafoto Blog
bil5
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog
bil6
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog
bil8
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar, wakati wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-had Mussa Salum. Picha na Mafoto Blog
bil9
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu. Picha na Mafoto Blog
bil10
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sl-had Mussa Salum, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, kufunga mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog
bil11
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo,Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA WARSHA YA PILI YA KIMATAIFA YA UNESCO MKOANI TANGA LEO

su1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika Firmin Matoko katikati na mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Zulmira Rodrigues kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Balozi wa Korea kusini Nchini Geum-Young Song kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti kiongozi wa Spice kutoka Zanzibar ambae ni mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.(Picha na OMR)

WAZIRI MKUU AAGIZA DAKTARI ASIMAMISHWE KAZI

MTW1
Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw2
Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw5
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw6
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw7
Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia)  baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw8
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw9
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma  kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka  kurejea Dar es salaam Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 ………………………………………………………………………………………….
1.Ni baada ya kudai rushwa ya sh. 100,000/- kumfanyia upasuaji mgonjwa
2.Mama alilazimika kuuza shamba ili apate fedha za kumtibia baba yake
3.Aagiza maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo yafungwe leo hii
4.Amwagiza RAS aitishe kikao cha watumishi wote leo saa 9 alasiri
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-. Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja. Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa. Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. “Dirisha la wazee lipo?” akajibiwa hakuna. “Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo” nalo pia akajibiwa halipo. “Je wazee wana daktari wao”, hakupata jibu.
“Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee  na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,”  alisema wakati akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa.
Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba “tuna jambo, tuna jambo” wakiashiria kutaka kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.
Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi Waziri Mkuu. “Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje (pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji.” “Tarehe 12 Februari  baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/- na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani”. “Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?” Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza.  Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua. Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo.  Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika. “Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho,” alisema.  Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.
Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.
Sakata la hospitali ya Ligula lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua.
Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni sana.
Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana huu.

MKE WA RAIS MSTAAFU NA MWENYEKITI WA WAMA ASISITIZA UMUHIMU WA CHAMA CHA GIRL GUIDE TANZANIA KUONGEZA WANACHAMA

WAMA1
Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
WAMA2
Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza  katika kusherekea World Thinking Day  ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
WAMA3
Mama Salma Kikwete akiingia katika ukumbi wa Tambaza Sekondari akiwa na viongozi wa Girl Guide kushoto ni Mama Symphorosa Hangi, Kamishna Mkuu  na kulia ni Mama Matilda Balama na Mkuu wa Shule ya Tambaza.
WAMA4
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi  na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa  Girl Guide
WAMA5
Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wakinamama wajasiriamali ambao walifanya maonyesho katika sherehe hizo
PICHA NA YUSUPH BADI
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Philomena Marijani- Meneja Uraghbishi na Mawasiliano, WAMA
Chama cha Girl Guide Tanzania kimetakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha inaongeza wanachama watakaojiunga na chama hicho ili vijana wengi waweze kunufaika
Rai hiyo imetolewa mwishoni wa wiki na Mke wa Rais Mstaafu na  Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete wakati wa maadhimisho  ya kilele cha  siku ya  World Thinking Day yenye kauli mbiu ya Ungana, Shirikiana, Sherekea  iliyoadhimishwa na Tanzania Girl Guides Association. Sherehe hizo zilianza kwa maandamano ya wanafunzi Wanachama kutoka Upanga katika Makao Makuu ya Girl Guide Tanzania na kumalizikia  katika Shule ya Sekondari Tambaza ambapo  sherehe rasmi ilifanyika hapo.
Akiongea katika sherehe hizo Mama Salma Kikwete  alipongeza uongozi wa Girl Guide  kwa kufikia mikoa 19 ambapo  mpaka sasa chama kina  wanachama 97,143 na aliongeza kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni kuongeza Wanachama zaidi kwani Tanzania ina watu wengi sana.
“Wito wangu kwenu ni kuongeza juhudi ya kuwafikia vijana wengi zaidi kwani sote tunajua umuhimu wa TGGA katika kuwasaidia vijana kujiepusha na changamoto mbalimbali katika makuzi yao. Ni lazima tuweke malengo ya muda mfupi, kati na mrefu ndani ya miaka mitatu ili ifikapo  mwaka 2018 tuwe tumeingiza wanachama zaidi ya 100,000/= Tumieni vizuri shule za msingi na sekondari , nina hakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. ” Alisema Mama Kikwete
Mama Kikwete pia alishauri uongozi wa Girl Guide Tanzania kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto kwa kutumia rasilimali walizonazo.
“Kwa kuwa TGGA ni chama kikongwe, chenye rasilimali kama ardhi ambazo ziko sehemu nzuri kibiashara  naamini kwamba ikitayarishwa mipango mizuri  mnaweza kupata wabia wenye tija au mkawekeza kama chama kwa kushirikiana na mabenki. Mtakusanya kodi ambazo zitasaidia uendeshaji na kuongeza uwekezaji. ”Alisema Mama Kikwete.
Akielezea maana ya World Thinking Day Mkufunzi wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association, Mama Magreth Olumbe alisema kuwa sherehe hii ilianza rasmi mwaka 1926 ambayo ni siku ya; kuwakumbuka Girl Guide wote duniani na hasa wale walio kwenye mazingira magumu;kuongelea mambo yanayowagusa wasichana kwa mfano mimba za utotoni, kuolewa katika umri mdogo; na kukumbuka mwanzilishi wa Chama Lord Baden Powell na mke wake Olave Baden Powell.  
Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa  Tanzania Girl Guides Association, Mama Symphorosa Hangi alisema kuwa katika kuadhimisha  World  Thinking Day walikuwa na wiki mbili za kutoa huduma kwa jamii ikiwemo kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road na kutoa chakula, mavazi   na nauli za kuwarudishwa makwao wale waliokuwa wameruhusiwa baada ya matibabu. Aliongeza pia walitumia muda huo kuhamasisha wasichana wengine kujiunga na chama cha Tanzania Girl Guides ili nao waweze kupata fursa ya kujikwamua kifikra kwa kupitia mafunzo yanayotolewa na chama.
Chama cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kilianzishwa hapa nchini mwaka 1928. TGGA ni chama kisicho cha serikali na ni cha kujitolea chenye lengo la kuwaendeleza watoto wa kike na wanawake kwa ujumla kushiriki katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kupitia elimu na mafunzo yanayotolewa kwa kuzingatia kanuni za Girl Guides pamoja na kuwajenga kimaadili.

BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO

Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya
Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna  
 
Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. .
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.
Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya  Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .
Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
 
Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa  nje kusbiri utaratibu mara baada  waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto.Picha na David Nyembe 

TAS NA UTSS WAMTAFUTA MWENZAO ALIYEPOTEA.

2 (1) 
Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Dar es Salaam.
Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) wameiomba Serikali kuwasaidia kumtafuta Bw. Said Abdalah Ismail (47) mkazi wa Kijiji cha Mbezi Mlungwana Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa (TAS) Josephat Torner alipokua akiongea na waandishi wa habari juu ya  taarifa hii ya kupotelewa na mwenzao.
“TAS kwa kushirikiana na Shirika la Under The Same Sun (UTSS) tunaendelea kufanya juhudi ya kumtafuta na juhidi zetu tunaomba Serikali ituunge mkono” alisema Torner
Torner aliongeza kuwa, Said alionekana kwa mara ya mwisho  Januari 31 mwaka huu katika Kijiji cha Mtipule alikokwenda kuuza mboga za majani na baadae alionekana katika kilabu cha pombe ya kienyeji ambapo inasemekana aligombana na wenzie waliokua wakinywa pamoja kabla hajaondoka kilabuni hapo.
“Tunalitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lile la Afrika Mashariki kujadili kwa kina tatizo hili  na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu pia vyombo vya dola kuhakikisha wakatili hao wanatafutwa, wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria  ili sisi wenye ualbino tuweze kuishi kwa amani.” Alisema Torner.
Amesema kuwa pamoja na juhudi za kumtafuta Said kuendelea taarifa ya kupotea kwake ilipelekwa kituo cha Polisi Wilaya ya Mkuranga na kupewa RB namba MKU/PE/05/2016 pia kituo kidogo cha polisi Kimanzichana kwa RB namba KIM/RB/50/2016.
 Aidha, Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo ambapo jina la muuza pombe pamoja na majina ya wale aliogombana nao tayari yamewasilishwa polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Albino wilayani Mkuranga mkoani Pwani Hassan Kambangwa akizungumzia tukio amesema amelipokea kwa masikitiko makubwa na kuiomba Serikali kuwachukua hatua kali za kisheria wote waliohusika katika tukio hilo.
Kambangwa ametoa wito kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji kutafuta mbinu za kuzuia ukatili huo.
Ikumbukwe kuwa tukio hilo kwa Bw.Said Abdalah Ismail ni la pili kwa kuwa  aliwahi kupatwa na mkasa wa kukatwa kiganja cha mkono akiwa mkoani Morogoro miaka michache iliyopita.

SPIKA WA BUNGE MH. JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI LEO

J1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai akizungumza na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) hawapo pichani kutoka Tanzania wakati walipomtembelea katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es salaam na kumpa salaam maalum za kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake na watanzania na kuwa Rais wa Tanzania awamu ya Tano ikiwa ni pamoja na kupongeza utendaji kazi wake kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
J2
Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kutoka kulia ni Mh. Adam Kimbisa, Mh. Shy Rose Banjhi na Mh. Abdallah Mwinyi wakizungumza na Spika wa Bunge.
J3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai kulia akizungumza na wabunge hao.
J5
Mkurugenzi wa Mhusiano ya Kimataifa ofisi ya Bunge Bw. Josey Mwakasyuka akijitambulisha katika mkutano huo.
J7
Mh. Shy Rose Banjhi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kushoto ni Afisa habari wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya

POLISI WAZIMA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KILICHOKUWA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU JOSEPH TAWI LA SONGEA

01
Mmoja wa vijana ambaye anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa na serikali  akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo.
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
1
Baadhi ya askari wakijiandaa kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na Mipango Posta  jijini Dar es salaam.
2
Wanafunzi hao wakifurumushwa na polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana bila kibali kwenda kumuona  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
3
Wanafunzi hao wakitoka mbio baada ya kuamriwa na polisi kuondoka eneo hilo na kutawanyika.
4
Askari polisi wakizunguka maeneo mbalimbali kuangalia hali ya usalama.
5
Polisi wakiwazuia wanafunzi hao na kuwaamuru kutawanyika kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.
6
Mmoja wa polisi akiwaamuru wanafunzi hao kutawanyika eneo hilo.
ยช