Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2016

AU : YAWATAKA RAIA WA UGANDA KUWA WATULIVU BAADA YA UCHAGUZI

Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika nchini Uganda umetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi na kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wawapendao.
Mkuu wa ujumbe huo wa AU, Sophia Okofor pia amewataka raia wa Uganda kudumisha amani na kuwa watulivu baada ya uchaguzi. Bi. Okofor kutoka Ghana aidha amewataka wanasiasa wanaowania nyadhifa mbalimbali kuheshimu matokeo na kufuata mchakato wa kisheria endapo hawataridhishwa na matokeo ya uchaguzi.
Uchaguzi wa bunge na rais umeanza asubuhi ya leo nchini Uganda na tayari Rais Yoweri Museveni amepiga kura yake katika kituo cha Rwakitura huku wagombea wengine wa nafasi ya urais pia wakipiga kura zao kwenye vituo walikosajiliwa.
Wapigakura waliojiandikisha ni takriban milioni 15.3 na kuna vituAo 28, 010 kote nchini Uganda. Wagombea urais ni wanane na kwa upande wa bunge, viti vinavyowaniwa ni 290.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages