NA
K-VIS MEDIA/Na Mashirika ya Habari
KINANARA
wa upinzani nchini Uganda, Kanali Dkt. Kizza Besigye amekamatwa na polisi leo
Ijumaa Februari 19, 2016, huku Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni akiongoza
kwenye matokeo ya awali ya kura ambazo zimehesabiwa hadi sasa.
Polisi
wa kutuliza ghasia walifyatua mabomu ya kutoa machozi jijini Kampala, eneo
ambalo kiongozi huyo wa upinzania kutoka chama cha Forum for Democratic Change,
(FDC), ana wafuasi wengi. Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo ulifanyika Alhamisi
Februari 18, 2016 na umeelezwa kuwa ulikuwa mtulivu na wa amani licha ya kasoro
chache zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo ambapo vifaa vya kupigia kura
vilichelewa kufika.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Nchini Uganda, Injinia Badru Kigundu, amewaambia waandishi
wa habari kuwa kwa wale waliofanya fujo na kuharibu vifaa vya kupigia kura,
wasitegemee uchaguzi kufanyika kwenye eneo hilo na badala yake wasubiri
uchaguzi mwingine mwaka 2021.
Hii
ni mara ya pili chini ya masaa 245 Dkt. Besigye anakamatwa na polisi. Alhamisi
jioni majira ya saa 12, Dkt. Besigye alizuiwa na polisi, ambapo walisema
wanamzuia kwa usalama wake ili asidhuriwe na wafuasi wake, ingawa baadaye
walimuachia.
Dkt.
Besigye ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Museveni kabla ya
kuhitilafiana, amedai uchaguzi huu sio huru na wa haki na kusema kuwa “Madikteta
Duniani kuondolewa kwa mapinduzi kama sio kifo.”.
Matokeo
rasmi yanatarajiwa kutangazwa Jumamosi Februari 20, 2015
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269