Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya.
Suala la kupambana
na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa
Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa
Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa Ziwa Victoria
ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.
Mara kadhaa huduma
za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani
Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda
katika eneo la ferry la kivuko.
Usumbufu kama huo unahofiwa huenda
ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu
Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.
Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa
kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza
kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri
(Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.
Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo
zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya
Kusimamia Rasilimali za Uvuvi katika Ziwa Victoria (Beach Management
Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya
shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.
Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo
zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa
majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na
matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine,
ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa
ziwa Victoria.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269