Breaking News

Your Ad Spot

Feb 19, 2016

K-VIS MEDIA Na Mashirika ya Habari
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amemvaa mgombea urais wa Marekani Donald Trump, na kumwita sio Mkristo.
Papap Francis ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ndege akirejea Vatican akitoka nchini Mexico baada ya kuongoza ibada kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Trump alinukuliwa kuwa akiwa Rais wa Marekani atajenga ukuta kwenye mpaka wan chi yake na Mexico ili kuzuia wahalifu kuingia Marekani hususan wauza “unga”.
Pia Papa Francis hakufurahishwa na kauli za mgombea huyo tajiri zinazoashiria ubaguzi ambapo Trump amewahi kunukluliwa kisema, endapo atachaguliwa kuwa rais wa Marekani, Waislamu hawataruhusiwa kuinia nchini humo.
Papa alisema “Yeyote anayefikiria kujenga ukuta baina ya Mexico na Marekani huyo sio Mkristo.” Papa alisema.
Akijibu matamshi hayo ya Papa, Trump ambaye alikjuwa akifanya kampeni zake huko South Carolina, aliiita kauli ya Papap kuwa si ya haki na kumwita Papa kuwa ni “mshenga) wa serikali ya Mexico”
“Sibabaishwi na kauli za Papa, ni lazima tuzuie wahamiaji haramu.” Alisema Trump akimjibu Papa. na kuongeza kuwa Papa atatambua Ukristo wa Trump, pale Vatican itakaposhambuliwa na Wanamgambo wa Kiislamu, ISIS

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages