TAMWA YASIKITISHWA KESI ZA UBAKAJI/ULAWITI KWA WATOTO KUTOHUKUMIWA
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(katikati) akizungumzia mbele ya waandish wa habari (hawapo pichani) ni kwa jinsi gani wamepata malalamiko kutoka kwa familia zinazofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi za mahakama, polisi na baadhi ya hospitali hapa nchini.
Mratibu
wa Kituo cha Usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza
mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa
wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya
ukatili.
Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia.
Mwanasheria
wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani
wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
leo katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini.
……………………………………………………………………………………………………………………..
Chama
cha Wanahabari wanawake nchini Tanzania(TAMWA) kimelaani vikali
ucheleweshwaji na upotoshwaji ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa
kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi ya mahakama, polisi na
baadhi ya madaktari hospitalini. Hali hiyo imekuja baada ya TAMWA
kubaini kesi sitini na mbili (62) za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu
au uamuzi na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi
cha mwaka 2014 hadi 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga amesema kati ya kesi 63 za ubakaji, ni kesi moja tu mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi arobaini na tatu (43) bado ziko mahakamani, kesi kumi na saba (17) zimeshindwa kufika mahakamani ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosa ushahidi.
Pia aliongezea kwa kusema kuwa uongozi wa TAMWA umesikitishwa kuona kesi hizo zikicheleweshwa na vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo jeshi la polisi na mahakama. Na kuna baadhi ya viongozi wanapokea rushwa ili kuzima kesi za watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia, pia baadhi ya polisi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa mlalamikaji ambapo wanatoa maneno ya vitisho na kupelekea mlalamikaji kukosa ujasiri wa kuhifadhi na kutetea kesi yake na wakati mwingine mama mzazi anaandikwa kama mlalamikaji badala ya mtoto mwenyewe aliyefanyiwa ukatili huo.

Pia wameunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposema wakati wa siku ya sheria
duniani kuwa “Kila Hakimu wa Mahakama anapaswa kuhukumu kesi si chini ya
260 kwa kila mwaka na kwa haki”, Hivyo basi wao kama TAMWA wanaamini
ndani ya mwaka huu Mahakama hapa nchini zitafanya kazi yao kiweledi ili
kuweza kupunguza ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269