Breaking News

Your Ad Spot

Feb 24, 2016

TUME YA MIPANGO YATEMEBELEA SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO (SIDO)


Bibi. Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, alipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha TEMSO Engineering kinachozalisha vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile mashine za kufyatulia matofali na matoroli (wheelbarrows).



Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).


Omar Jumanne Bakari (wa tatu kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es Saalam na mikoa ya jirani.


Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile.



Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO (aliyesimama), akitoa maelezo kwa viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango (waliokaa kushoto) kuhusu SIDO inavyofanya kazi katika kuwasaidia wazawa ili kukuza uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo. Waliokaa kulia ni wamiliki wa viwanda vidogovidogo wanaofanya shughuli zao chini ya SIDO.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages