Na.Ahmad Mmow, Lindi-Nachingwea.
Ununuzi
wa gari lenye namba usajili DFPA 1695, Landcruiser mali ya Halmashauri
ya Wilaya ya Nachingwea, mwanzoni mwa wiki iliyopita ilizua
mvutano baina ya madiwani na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,
Mhandisi, Jackson Masaka.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa pili wa baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha
2015/2016 Madiwani hao walisema walikuwa na mashaka katika ununuzi wa
gari hiyo, kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya fedha zilizotumika
kununulia gari hiyo na bila kuwashirikisha.
Diwani
wa kata ya Mkutokuyana, Sada Makota, alisema mchakato wa ununuzi wa
gari hiyo umegubikwa na utata, kwa madai kuwa fedha ambazo awali
zilitengwa kwa ununuzi wa gari hiyo ni shilingi 84 milioni, wakati
zilizoidhinishwa kwenye bajeti ni shilingi milioni 120.00 tu, hata
hivyo ilionekana ilinunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni.
Alisema licha ya ongezeko hilo, lakini pia taarifa haikuonesha fedha za nyongeza zilitoka wapi na kwaidhini ya nani.
Diwani
wa kata ya Lionja, Joachim Mnungu, alisema mkurugenzi alikuwa na kila
sababu ya kuwajulisha madiwani kila hatua iliyohusu mchakato wa ununuzi,
ikiwamo mabadiliko ya mara kwa mara ya bei.
Alisema
fedha zilizokatengwa kwa ajili ya ununuzi ni shilingi 84 milioni. Hata
hivyo kabla ya gari hiyo kuletwa, bei ilipanda na kufikia shilingi 96
milioni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269