Breaking News

Your Ad Spot

Feb 24, 2016

UTAFITI : MWANYA KATI YA MATAJIRI NA MASIKINI KUPANUKA MAREKANI

Utafiti: Mwanya kati ya matajiri na masikini unazidi kupanuka Marekani
Utafiti mpya unaonyesha kuwa mwanya kati ya matajiri na masikini unazidi kupanuka nchini Marekani.
Gazeti la Wall-Street Journal limechapisha ripoti inayoonyesha kuwa mlingano wa kijamii unazidi kutokomea miongoni mwa Wamarekani ambapo Masikini wanazidi kulemewa na uchochole nao matajiri wanazidi kujilimbikizia mali kila uchao. Utafiti huo mpya umefichua kuwa, jamii ya Wamarekani weusi imezidi kutengwa na kunyimwa nafasi sawa na wenzao weupe jambo linalozidi kupanua pengo kati ya matajiri na masikini. Utafiti huo umetumia vigezo vya afya, ajira na umri wa kuishi watu ili kuandaa ripoti hiyo mpya. Kwa mujibu wa watafiti ni kwamba Marekani inaongoza kwa kuwa na ukosefu wa usawa katika jamii.
Ripoti hiyo imewanyooshea kidole cha lawama wanasiasa wa Marekani ambapo wanatuhumiwa kuharibu mazingira ya uwekezaji na hivyo kuongeza kiwango cha ukosefu wa ajira. Matokeo yake ni kupanuka mwanya kati ya watu masikini na wale matajiri katika nchi hiyo inayohesabiwa kuwa na uchumi mkubwa zaidi duniani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages