.

MWAKYEMBE APOKEA TAARIFA YA SHERIA YA MANUNUZI

Mar 31, 2016

3 Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto) akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma, katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome. 5Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi.
4Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Sifuni Mchome.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amepokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka Tume ya kurekebisha Sheria.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es salaam Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amesema taarifa hiyo ya utafiti itasaidia kurekebisha sheria ya manunuzi ambayo inalenga kukuza uchumi wa nchi.
“Mimi na wataalamu wangu tumeipokea taarifa hii, tutaiangalia na kuhakikisha tunaifikisha Wizara ya Fedha na Mipango na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuendelea na utaratibu unaofuata ili mchakato wa marekebisho uweze kufanyika kwa haraka”alisema Dkt Mwakyembe.
Akifafanua juu ya sheria ya manunuzi ya Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi  amesema kuwa Tume imefanya utafiti wa sheria hiyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
“Tumepata maoni mengi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa manunuzi ya Serikali kwa namna wanavyoiona sheria ya manunuzi ya Umma,na sisi tumeyachambua maoni hayo kwa kutumia vigezo vya sheria”alisema  Jaji Mujulizi.
Aidha,Tume imetoa maoni kwa Serikali kusimamia sheria ili iweze kuendana na ukuaji wa uchumi nchini kwa kurekebisha baadhi ya sheria ili kuepuka muingiliano uliopo kati ya sheria ya manunuzi na sheria nyingine.
Marekebisho ya sheria hii ni moja ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli  lililotolewa Novemba 2015 alipokua akizindua Bunge la 11.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA MASAFA YA USIKIVU YA TBC-KISARAWE.

tib1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe
tib2
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
tib3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
tib4
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
tib5
Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba
Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

UTOAJI MIMBA USIO SALAMA NI JAMBO LA KAWAIDA NCHINI TANZANIA NA NI SABABU KUBWA YA VIFO VYA WAJAWAZITO

0001
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  na Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili wakikata utepe wakati akizindua ripoti ya utafiti wa utoaji wa mimba usiosalama uliofanyika nchi nzima ambao umefanyika kwenye ukumbi wa JNICC leo jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 
001
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  na Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili wakionyesha utafiti huo mara baada ya kuuzindua rasmi.
1
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akisoma hotuba yake kabla ya kuzindua utafiti huo katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam.
03
Profesa PS Muganyizi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili   akiungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi huo  katikati ni Sarah Keogh kutoka taasisi ya Guttmacher ya nchini Marekani  na kulia ni Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili.
3
Baadhi ya wataalamu na waandishi wa habari mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
4
Baadhi ya wataalamu namaofisa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Utafiti mpya Watoa Makadirio ya Kwanza Kitaifa ya Matukio ya Utoaji Mimba Nchini
Katika utafiti wakilishi wa kwanza kitaifa kuhusu matukio ya utoaji mimba na huduma baada ya kuharibika kwa mimba nchini Tanzania, watafiti waligundua kwamba utoaji mimba kwa siri hutokea mara nyingi na huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye vifo na kuumia kwa wajawazito. Utafiti huo, uliofanywa na watafiti kutoka taasisi ya Guttmacher iliyoko Marekani, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili zilizoko hapa Tanzania, waligundua ya kwamba makadirio ya mimba 405,000 zilitolewa nchini ndani ya mwaka 2013, nyingi zikitolewa kwa taratibu ambazo si salama na kuhatarisha maisha ya wanawake. Kutokana na mchanganyiko wa sheria tata na yenye vizuizi vingi ya utoaji mimba ya Tanzania, wanawake hutafuta huduma za utoaji mimba zinazofanyika kisiri na ambazo si salama.
Watafiti hao, ambao walifanya utafiti kwenye vituo vya afya, miongoni mwa wataalamu wa afya na kufanya mapitio ya taarifa za idadi ya watu na uzazi, wamekadiria kwamba wanawake 66,600 walipewa huduma baada ya kuharibika kwa mimba kwenye vituo vya afya kutokana na matatizo yaliyotokana na utoaji mimba usio salama ndani ya mwaka 2013. Hata hivyo, karibu wanawake 100,000 ambao walipata matatizo hawakupata matibabu ambayo waliyahitaji. Watafiti wanatumaini kwamba matokeo yao yatasaidia kutaarifu  juhudi zinazoendelea nchini Tanzania kupunguza uwiano wa vifo vya wajawazito, ambao umebaki kuwa miongoni mwa iliyo juu zaidi duniani.
“Kwa kutambua kuwa utoaji mimba usiokuwa salama ni chanzo kikuu cha vifo vya wajawazito, Serikali ya Tanzania imepanua wigo wa upatikanaji wa huduma baada ya kuharibika kwa mimba katika muongo mmoja uliopita, lakini mapungufu makubwa bado yapo na wanawake wengi hawapati huduma wanazohitaji,” alisema Sarah C. Keogh, mtafiti mwanasayansi mwandamizi wa taasisi ya Guttmacher na mwandishi kiongozi wa utafiti huo. “Utafiti huu unabainisha mapungufu hayo na kusaidia kuunda mikakati kuhakikisha kuwa kila mwanamke wa Kitanzania anayehitaji anaweza kupata huduma baada ya kuharibika kwa mimba inayoweza kuokoa uhai.”
Kiwango cha kitaifa cha utoaji mimba nchini Tanzania—36 kwa kila wanawake 1,000 walio kwenye umri wa uzazi—kinafanana na viwango vya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Hata hivyo, ndani ya Tanzania viwango vya utoaji mimba vinatofautiana kwa ukanda. Viwango vya juu ya utoaji mimba hupatikana katika Kanda ya Ziwa (51 kwa kila wanawake 1,000) na Nyanda za Juu Kusini (47 kwa kila wanawake 1,000), na kiwango cha chini hupatikana Zanzibar (11 kwa kila wanawake 1,000). Viwango hivi tofauti vya utoaji mimba huhusishwa kimsingi na utofauti katika viwango vya matumizi ya njia za uzazi wa mpango na mimba zisizotarajiwa, na uwezekano wa wanawake kuamua kutoa mimba katika tukio la kupata mimba zisizotarajiwa.
“Mbali na huduma baada ya kuharibika kwa mimba, wanawake wa Kitanzania wanahitaji upatikanaji bora na kamilifu wa huduma mbalimbali za njia za uzazi wa mpango na ushauri nasaha kuhusu uzazi wa mpango  ili waweze kufanya maamuzi sahihi,” alisema Godfather Kimaro, mwanasayansi mtafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania, ambaye alifanya kazi kwenye utafiti. “Ndani ya mwaka 2013, wanawake wa Kitanzania walipata mimba zisizotarajiwa zaidi ya milioni moja, ambazo kati yake 39% ziliishia kwenye kutolewa. Kukabiliana na mahitaji yasiyokidhiwa ya uzazi wa mpango kutapunguza kiwango cha mimba zisizotarajiwa na hivyo kupunguza uhitaji wa kutoa mimba na vifo na majeruhi ambayo kwa mara nyingi hutokea baada ya taratibu zisizo salama.”
Watafiti wamependekeza kuimarisha juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa huduma baada ya kuharibika kwa mimba, ambayo kwa sasa inapatikana bila ulinganifu katika maeneo mbalimbali. Wamependekeza uwekezaji katika kufanya huduma baada ya kuharibika kwa mimba inapatikana katika ngazi zote za mfumo wa afya, ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo watoa huduma wa ngazi ya kati na kusambaza kikamilifu dawa na vifaa vyote muhimu kwenye vituo vya afya. Pia, walisisitiza umuhimu wa kujumuisha utoaji wa huduma za uzazi wa mpango  kama sehemu ya huduma baada ya kuharibika kwa mimba na kuhimiza kwamba kila mwanamke anayetibiwa kutokana na matatizo yanayohusiana na kutoka kwa mimba apewe ushauri wa kina na nyenzo za uzazi wa mpango. Hatimaye, walipendekeza kwamba utata katika sheria ya utoaji mimba ya Tanzania ufafanuliwe kuhakikisha kuwa wanawake wanaweza kupata utaratibu salama na wa kisheria  kwa kiasi kamili kinachoruhusiwa. Watafiti wanatumaini kwamba matokeo ya utafiti huu yatasaidia kuleta mwanga kwenye sera na mipango ambayo italeta huduma za kifanisi zaidi na hatimaye kuboresha hali ya afya ya uzazi ya wanawake wote wa Tanzania.
Matukio ya Utoaji Mimba na Huduma Baada ya Kuharibika kwa Mimba Nchini Tanzania” na Sarah C. Keogh wa Taasisi ya Guttmacher et al. inapatikana mtandaoni kupitia PLoSONE.
Utafiti huu uliweza kufanyika kutokana na misaada kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway.

MONUSCO YAONGEZEWA MUDA WA KUENDELEA KULINDA AMANI DRC

Na Mwandishi Maalum . New York
Baraza  la Usalama la Umoja wa Mataifa,   limepitisha  azimio jipya ambalo pamoja na mambo mengine  limeiongezea   kwa mwaka mmoja Misheni ya kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO ).
Sambamba na kuiongezea mwaka MONUSCO,  Baraza la Usalama pia limesitisha zoezi la kupunguza  walinzi wa Amani 1,700 kama ilivyopendekezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Huku Azimio  hilo likitamka  bayana kuwa  MONUSCO inatakiwa kuwa na  walinzi wa Amani wasiopungua 19,815, waangalizi 760,  pamoja na polisi 1,050. 
Ndani ya MONUSCO  kuna Brigedi maalum  ijulikanayo  kama Force Intervention  Brigade (FIB) yenye mamlaka nguvu ya kuyashughulikia makundi ya waasi yenye silaha. Brigedi hii  inaundwa na walinzi wa amani kutoka Tanzania, Afrika ya  Kusini na Malawi.
Kwa mujibu wa Azimio hilo jipya lililopitishwa  na wajumbe 15 wa Baraza  la  Usalama,  uamuzi wa   kuiongezea muda wa mwaka mmoja   MONUSCO  hadi Machi 31,2017, pamoja na kutotoa baraka za kupunguzwa kwa walinzi  wa Amani kunatokana na  taarifa za kuzorota kwa hali ya usalama hususani katika kipindi  hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu.
Jamhuri  ya Kidemokrasia ya  Kongo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Rais mwezi Novemba mwaka huu na tayari kuna taarifa za kuwapo kwa  sintofahamu  miongoni mwa makabila kutokana na tofauti za kisiasa, kuongezeka kwa makundi ya waasi wenye silaha,  kuzorota kwa hali ya kibinadamu  hali inayoitia wasiwasi Jumuiya ya Kimataifa kwamba   kunauwezekano  wa  kutokea machafuko.
 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,  kupitia  Azimio hilo,  limeionya  Serikali ya DRC  kuhusu kuchelewa kwa maandalizi ya  uchaguzi wa rais, huku likitoa wito kwa serikali  wa kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, na makosa ya uhalifu wa kivita  na ukatili dhidi ya  binadamu.
Vile vile  Baraza la Usalama limetoa wito kwa serikali na wadau wengine pamoja na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ( CENI) wa kuhakikisha uwazi   kuhusu mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa kalenda ya uhakika  ya uchaguzi.
Aidha   serikali imetakiwa kutenga bajeti ya kutosha kwaajili ya  uchaguzi na kuweka maadili ya uchaguzi na kuchukua hatua za kuboresha daftari la wapiga kura pasipo kuchelewa.
 Kuhusu makundi  ya waasi wenye silaha,  wajumbe wa Baraza la  Usalama wametoa wito wa kutaka kurejeshwa mapema  iwezekanavyo   operesheni ya  pamoja kati ya MONUSCO na Jeshi la DRC ( FARDC) dhidi  ya makundi  hayo ya waasi hususani kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda ( FDLR).Makundi mengine ya waasi na ambayo yameendeleza matukio ya mauaji  ya raia wasio na hatia na ambayo pia yanatakiwa kushughulikiwa ni  pamoja na kundi la ADF, Mai Mai  na LRA
Azimio hilo lenye kurasa  15 pia limetilia mkazo kuhusu ulinzi wa raia,  ulinzi wa watoto na  linakemea  vikali  kuhusu  vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AANZA ZIARA MKOANI MBEYA LEO

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi, akiwasalimia baadhi ya viongozi wa CCM wa mkoa baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya leo asubuhi. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya, Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo na Katibu msaidizi Mkuu wa mkoa, Adallah Mayomba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwai akiwa na mwenyeji wake, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Mwangwi Kundya (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya.

DONDOO ZA MAGAZETI YA LEO MACH 31, 2016

MAGAZETI YA TANZANIA LEO,MARCH 31, 2016

DKT. SHEIN AMUAPISHA BALOZI SEIF ALI IDDI KUWA MAKAMO WAKE WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

Mar 30, 2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimwapisha Makamo wake wa pili   Ikulu Mjini Zanzibar leo   (Picha na Ikulu, Zanzibar) 
Washauri wa Rais wa Zanzibar wa mambo mbali  mbali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Mjini Unguja
Balozi Seif Ali Iddi  akielekea sehemu ya kula kiapo  kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla   iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi  akipeana mkono  wa hongera na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha kuwa Makamo wa Pili

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi  na  Mama Asha Suleiman Iddi baada ya   kumuapisha  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar   katika hafla   iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akipeana mkono  wa hongera na  Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo leo  Ikulu Mjini Zanzibar

TAASISI YA TIBA YA MIFUPA, UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU (MOI) YAPOKEA MILIONI 20

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk. Othman Kiloloma akizungumza wakati alipokua akipokea msaada kutoka, Taasisi ya GSM ya Dar es Salaam baada ya kumkabidhi hundi ya mfano ya Milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa tiba na matibabu kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ambao unajulikana kama Hydrocephalus & Spinal Bifida. Jijini, Dar es Salaam leo (PICHA NA KHAMISI MUSSA)


NA KHAMISI MUSSA 

Taasisi ya GSM ya Dar es Salaam, imekabidhi msaada wa fedha taslimu shilingi milioni 20, kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kwa ajili ya kununulia vifaa tiba na matibabu kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ambao unajulikana kama Hydrocephalus & Spinal Bifida.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, mwakilishi wa Kampuni ya GSM, Shannon Kiwamba, alisema wameguswa na changamoto zinazowakabili Watanzania ndiyo maana imeamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Shannon alisema, pamoja na msaada wa fedha ambazo GSM imeipa Moi, vilevile watafadhili kambi za upasuaji (Surgical camps) kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi katika mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dkt Othman Kiloloma, alisema anaishukuru GSM kwa kuguswa na hali za Watanzania hususan watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi ambao kimsingi wanahitaji kufarijiwa.
Dkt kiloloma aliongeza, GSM imefanya uamuzi sahihi wa kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya kwa wakati mwafaka.
Alisema, fedha zilizotolewa na GSM zitatumika kama ilivyoelekezwa, vilevile Moi ipo tayari kutoa wataalamu kwenda mikoani kuwafanyia upasuaji watoto katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuwapunguzia wagonjwa adha ya kusafiri kwenda Dar es Salaam.
Taasisi ya Moi imekuwa ikichukuwa jitihada madhubuti za kuhakikisha Watanzania hususan watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanapata huduma bora pale walipo, ambapo imekuwa ikipeleka wataalam mikoani kwa ufadhili wa wadau mbalimbali na kuwafanyia upasuaji.
Takwimu zinaonesha hapa Tanzania watoto zaidi ya 5,000 kwa mwaka wanazaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo watoto 400 mpaka 500 pekee ndiyo wanapokelewa Moi.

TANZANIA NA KUWAIT, WASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   (kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan  (kushoto), wakipongezana Mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya usafiri wa anga baina ya nchi hizo mbili jijini Dar es Salaam leo Machi 29, 2016.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   (kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan  (kushoto) wakielekezwa na wanasheria wao jinsi ya  kusaini  hati za makubaliaono ya Usafiri wa Anga baina ya Kuwait na Tanzania , hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, leo.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   (kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan  (kushoto) wakibadilishana hati za makubaliaono ya Usafiri wa Anga baina ya Kuwait na Tanzania , hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   (kulia)  akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kuwait ,Mhandisi  Yousef Al Fozan  (kushoto)   mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kusaini makubaliaono ya Usafiri wa Anga baina ya Kuwait na Tanzania , hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, leo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   (Kulia) akimsikilza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga nchini Kuwait  Mhandisi  Yousef Al Fozan  (kushoto)    wakati wa hafla ya kusaini  makubaliaono ya Usafiri wa Anga baina ya Kuwait na Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo
Baadhi ya maofisa wa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakimsikiliza kwa makini waziri wa wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa   wapili (kutoka kushoto) wakati wa hafla ya kusaini  makubaliaono ya Usafiri wa Anga baina ya Kuwait na Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo
Baadhi ya wadau wa masuala ya usafiri wa Anga wakiwa katika hafla ya utilianaji saini ya makubariano ya usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Nchi ya Kuwait.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   (wapili kulia) akisisitiza jambo   kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga Kuwait Mhandisi  Yousef Al Fozan , (kushoto)   aliyeongozana na maofisa wake wakati walipowasili ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya  kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.  Wapili kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Idara  ya Mashariki ya kati  wa Wizara hiyo,Balozi Abdallah Kilima na  Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ua Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Kuwait Mhandisi  Yousef Al Fozan , wakipongeza na mara baada ya kutiliana makubakliano ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
ยช