Breaking News

Your Ad Spot

Mar 23, 2016

BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU LAITISHA KIKAO KUJADILI HALI YA MAMBO NCHINI BURUNDI

Baraza la Haki za Binadamu laitisha kikao kujadili hali ya mambo nchini Burundi
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa jana liliitisha kikao kujadili hali ya mambo nchini Burundi.
Kikao hicho kilichofanyika mjini Geneva Uswisi kilijadili ripoti ya wataalamu watatu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya haki za binadamu nchini Burundi. Asasi zisizo za kiserikali pamoja na nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Burundi ianzishe mwenendo wa mazungumzo na wapinzani kwa shabaha ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Kikao hicho kiliashiria pia kuweko kesi za ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi sambamba na kutathmini utiwaji mbaroni wapinzani pamoja mateso wanayokabiliana nayo kutoka kwa vyombo vya serikali.
Machafuko ya ndani nchini Burundi yalianza baada ya Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kutangaza nia yake ya kuwania tena kiti hicho kwa mara ya tatu mfululizo. Wapinzani wanasema hatua hiyo ilikiuka katiba ya nchi na makubaliano ya amani ya Arusha, Tanzania yaliyohitimisha vita vya ndani katika nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, tangu Aprili mwaka 2015 hadi sasa wakimbizi laki tano na 946 wa Burundi wamekimbilia katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tanzania, Rwanda, Uganda na Zambia.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages