Breaking News

Your Ad Spot

Mar 21, 2016

Dkt. Ali Mohammed Shein (pichani), ametangazwa leo Machi 21, 2016, kuwa ameshinda uchaguzi wa marudio wa Zanzibar kwa asilimia 91.4, ushindi ambao umeelezwa kuwa ni mkubwa kwa kiongozi wa Zanzibar usinda katika miaka ya hivi karibuni.
Hata hivyo Dkt. Shein amepata ushindi huo katika mazingira ambayo, chama kikuu cha upinzani visiwani humo yaani CUF, kiliususia uchaguzi huo kwa maelezo kuwa uchaguzi wa marudio si wa haki kwa vile uchaguzi ulikwishafanyika Oktoba 25, 2015 ambapo chama hicho kilielekea kushinda. Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), Jecha Slim Jecha, aliufuta uchaguzi huo kwa maelezo kuwa ulijawa na ghiliba na haukuwa huru na wa haki.
Dkt. Shein akisalimiana na Hamad Rashid

Kwa mujibu wa matangazo ya leo ya matokeo ya uchaguzi huo, Dkt. Shein amekusanya jumla ya kura 299,982 huku anayemfuatia, Hamad Rshid Mohammed, amejipatia kura 9,734 sawa na asilimia 3.4, huku Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye chama chake hakikushiriki uchaguzi huo amepata kura 6076 sawa na asilimia 1.9.
Hamad Rashid Mohammed wa ADC
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, chama kinachofuatia kile kilichoshinda, ndicho kitatoa makamu wa kwanza wa rais.
 Dkt. Ali Mohammed Shein, rais mteule wa Zanzibar, akionyesha cheti chake cha ushindi mara baada ya kutangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Sa,im Jecha kwenye ukumbi wa Salama wa Hoteli ya Bwawani mjini Unguja Machi 21, 2016.
 Mwenyekiti Jecha akitangaza matokeo
Aliyeshika nafasi ya pili kwenye matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa hotuba yake

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages