Breaking News

Your Ad Spot

Mar 23, 2016

LIBERIAYAFUNGA MIPAKA YAKE NA GUINEA CONAKRY BAADA YA WATU KADHAA KUFA KWA HOMA YA EBOLA KATIKA NCHI HIYO JIRANI

Liberia yafunga mipaka yake na Guinea Conakry baada ya watu kadhaa kufa kwa homa ya Ebola katika nchi hiyo jirani
Serikali ya Liberia imechukua uamuzi wa kufunga mipaka yake na Guinea Conakry baada ya watu kadhaa kufariki dunia katika nchi hiyo jirani kwa homa ya Ebola.
Liberia imetangaza kuwa, sanjari na kuchukua hatua za kiafya kwa ajili ya kukabiliana na kesi mpya za maambukizi ya Ebola, imechukua uamuzi wa kufunga mipaka yake na jirani yake Guinea Konacry.
Liberia iumechukua uamuzi huo masaa kadhaa tu baada ya kuripotiwa mripuko mpya wa homa hatari ya Ebola nchini Guinea Conakry ambao tayari umesababisha vifo vya watu watano huku mamia ya wengine wakiaminika kuwa wameambukizwa ugonjwa huo.
Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema kuwa, mripuko huo mpya umetokea katika kijiji cha Porokpara, kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Kesi mpya mbili za Ebola zilithibitishwa Ijumaa iliyopita Kusini mwa mkoa wa Nzérékoré nchini Guinea Conakry. Kesi mpya zilithibitishwa siku ambayo Shirika la Afya Duniani WHO lilitangaza kumalizika kwa mripuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani ya Sierra Leone.
Ebola imeua zaidi ya watu 11,300 tangu mwezi Desemba 2013 katika mripuko mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa wa ugonjwa huo uliozikumba zaidi nchi tatu za magharibi mwa Afrika za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Homa hiyo ya Ebola mbali na kusababisha vifo vya watu katika nchi hizo tatu, ilitoa pigo kubwa pia kwa uchumi wa nchi hizo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages