.

MAAFA YA MAFURIKO MOSHI: MBATIA MKURUGENZI WA MAAFA WAJIONEA WENYEWE

Apr 30, 2016


Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava .
Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko.
Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.
Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Hivi ndivyo hali inavyoonekana.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,Mbazi Msuya akizungumza na wananchi katika eneo hilo lililoharibika vibaya.
Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa.
.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
Kwahisani ya
  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

ABIRIA WANUSURIKA AJALI YA NDEGE MJINI BUKOBA LEO

Watu kadhaa wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air (pichani), waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa Bukoba baada ya ndege hiyo kupata pancha tairi ya nyuma ya upande wa kulia ilipokua inatua.
Kwa umahiri wa Rubani amaweza kuicontrol kama inavyo onekana pichani ikiwa pembezoni mwa Uwanja.
Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Jijini Mwanza ,tukio limetokea majira ya saa nne asuhuhi ya leo Jumamosi April 30,2016

 Kwahisani ya
#BUKOBAWADAU MEDIA
 

UVCCM: SUMAYE ACHA KUMBUGHUDHI RAIS DK. MAGUFULI HUNA VIWANGO

Apr 29, 2016

 KaimuKatibu Mkuu UVCCM
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Waziri mstaafu Frederick Sumaye, hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala. 

Sumaye ametakiwa amuache Rais Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri Mkuu lakini hakufikia hata thekuthi ya utendaji unaofanyika sasa.
   
Hayo yamesemwa jana na Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM wa kata mbili za Kwandele na Mbichi jimbo Rombo mkoani Kilimanjaro.

Shaka alisema anachokifajya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau.

Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika  utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye. 

"Amekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu yeyote na kwa bahari mbaya sana ndiye waziri mkuu zero kuliko mwingine yeyote tokea tupate uhuru mwaka 1961 "alisema shaka.

Aidha Kaimu huyo katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka aache kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.

Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi iuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima alisema  kina sumaye na wenzake  wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa. 

"Sumaye aacha kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati mambo yalikushinda wakati ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi Hanang ukalime maharage na karanga "alisema

Pia shaka aliwataka wananchi wa jinbo la Rombo kujitatayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwasabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, selasimi hajui anavhokufanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka 

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagonbea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba. 

Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa. 

"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, haiutuacha tukiwa tumegawahyika  , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni baa au janga katika jamii "alisema Raib. 

Jumla ya wananchi wapya 103 wa ccm na jumiya zake walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya Rombo.

VIONGOZI WA KISIASA WAFANYA BIASHARA, WATAKIWA KUWAJALI WATOTO WENYE ULEMAVU

 Wanafunzi wa shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini ugeni wa kaimu katibu mkuu uvccm taifa Shaka Hamdu Shaka
 wanafunzi na ugeni ukisikiliza Risala iliyo somwa na mmoja wa wanafunzi walemafu katika shule hiyo
 Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akipokea Risala ya Wanafunzi
 Mkuu wa shule ya msingi Mreyai Nuruel Laizer  wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Rahibu Juma akifuatiwa na kaimu  katibu mkuu UVCCM taifa katika makabidhiano ya baadhi  ya msaada ambao ulipelekwa shuleni hapo
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mreyai
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mreyai
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akizungumza na moja ya Wanafunzi wenye ulemavu
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akipanda mti
Wanafunzi wa Shule ya msingi Mreyai wakifurahi pamoja na 
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka  Shaka.

===================

NA FAHADI SIRAJI
Viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto  wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwani wao pia  ni binadamu wanao sitahili kupata haki na mahitajj muhimu ya kibinadamu.

Hayo yamebainishwa na leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro yenye jua huduma watoto wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa akili.

Alisema kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani wakitengenezwa vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu  watakuwa viongozi wazuri wa baadae.

Aidha alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo ya watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa ata sehemu
ambayo aitakiwi siasa.

"napenda kuviambia vyama vingine vya siasa sasa ivi uchaguzi imeisha ni kipindi cha kufanya kazi na kuachana na siasa sasa ivi ni kipindi cha kufanya kazi na kutatua ma tatizo ya wananchi " alisema Shaka.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi ambao ni walemavu wa viungo ambapo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi, ukosefu wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu ,baskeli kwa
ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.

Alisema kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika ma bweni apo shule ni lakini wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro  kwani vitanda ambavyo wana vitu mia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja kuchukuwa.

Aliomba serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia kitu icho ili watoto hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto.

"watoto hawa wanawazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wa me wamewaleta Hapa ili wapate elimu hivyo tu naomba sana serekali na wadau mbalimbali wajitokeze kutusaidia"alisema Laizer

Shule hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi, sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.

DC KINONDONI HAPI AANZA MAPAMBANO NA WATUMISHI HEWA WILAYANI KWAKE, ABAINI 89 WALIOKOMBA SH. ZAIDI YA SH BILIONI 1.331, ASEMA MWISHO WA MACHINGA KESHO KUKAA KATIKA MAENEO YASIYO RASMI

Apr 28, 2016

DC wa Kinondoni Salum Hapi akizungumza leo ofisni kwake
NA BASHIR NKOROMO
Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam,  Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa  imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa.

Amesema, baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo siku saba zilizopita, amesimamia maofisa wake kufanya uchunguzi na kubaini kuwa pamoja na wafanyakazi hao hewa ambao wameisababishia serikali kupoteza sh. 1, 331, 734, 881 pia wapo watumishi vivuli wapatao 8823 ambao wanalipwa mishahara wakati  hawafanyi kazi katika maeneo husika kutokana na sababu mbalimbali.

Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu.

Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kinaa na kuwabinya wasimamizi katika idara mbalimbali za utumishi, na kwamba ameelekeza mwanasheria kuchukua hatua haraka ili wahusika wachukulie hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine, Hapi amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga, kuwa kuanzia kesho ni marufuku kufanya shughuli zao katika maeneo yasiyo mahsusi kwa biashara katika wilaya ya Kinondoni.

Amesema, agizo hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kutaka ifanyike hivyo kwa lengo la kulifanya jiji liwe safi kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuhimiza usafi nchi nzima.

Hapi amesema, machinga wote kama wahanitaji kufanya biashara zao ni lazima waende katika maeneo yaliyopangwa, ambayo alisema, hapo mengi na bado yana nafasi za kutosha kwa ajili ya kutumika kufanyia biashara.

MAGAZETI YA LEO APRIL 28


ยช