Na
Mwandishi Maalum, New York
Zaidi
ya nchi 162 zinatarajiwa kutia saini leo
( Ijumaa) Makubaliano kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi
ambayo yalifikiwa jijini Paris -Ufaransa mwezi Desemba Mwaka jana.
Miongoni
mwa nchi ambao zimethibitisha kushiriki hatua
hiyo muhimu na ambayo ni hatua ya mwanzo kuelekeza utekelezaji wa makubaliano hayo maarufu kama Paris Agreement
ni pamoja na
Mataifa makubwa kiuchumi duniani na
ambayo yanachangia kwa asilimia kubwa katika utoaji wa hewa ya ukaa.
Baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo katika mkutano ambao umeandaliwa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,
nchi wanachama wa Paris Agreement
watatakiwa ama kupitisha
makubaliano hayo au kuridhia ( ratification).
Ili hatua ya utekelezaji ianze Nchi 55
zinatakiwa kuridhia makubaliano
hayo ndani ya siku
thelathini, na nchi hizo 55
zinatakiwa ziwe ni zile ambazo kwa
ujumla wake zinachangia asilimia 55 ya hewa ukaa.
Taarifa
kutoka Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa zimeeleza kuwa mataifa makubwa kama Marekani na
China yameonyesha nia ya kutia saini
makubaliano hayo huku nchi ndogo na zinazoendelea zipatazo 13 zinatarajiwa
kusaini na kuridhia makubaliano hayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269