Breaking News

Your Ad Spot

Apr 24, 2016

MWANAMUZIKI NGULI WA CONGO PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA

58b9d6b2-71c3-4333-900c-2aae3762ad8a 

Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia.
a6748ea4-c121-499b-babb-f4ba4544d416 
Papa Wemba aanguka na kupoteza fahamu katikati ya onesho.
8586346b-436b-48a7-8a9c-960611915e52 
Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wamepanda jukwaani. Hali ilizidi kuwa mbaya wakamkibiza hospitali ambako alikata roho.
Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.
Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.picha kwa hisani ya michuzi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages