Breaking News

Your Ad Spot

Apr 12, 2016

RAIS MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI WAKATI WA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIEWAHI KUWA MBUNGE WA VITI MAALUMWA CHADEMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Rais Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, wakati walipowasili kwenye viwanja vya Karimjee, wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye aliwahikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli
 Rais  Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
 Rais  Magufuli, na Mkewe Mama Jannet Magufuli, wakisalimiana na baadhi ya waheshimiwa wabunge waliokuwepo kwenye shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye aliwahikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam.
 Rais  Magufuli, akimpa pole Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,  Freeman Mbowe, kufuatia msiba wa aliewahikuwa  Mbunge wa Chama chake, Marehemu Christina Lissu Mughwai.
 Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, aliewahikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukuwasili kwenye ukumbi wa Karimjee leo, Jijini Dar es salaam.
 Rais  Magufuli, akimfariji, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu  ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, akimfariji  Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, akifuatiwa na Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai,  Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
 Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Veronica Mallya akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.





Rais , akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai,  aliewahikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
Rais  Magufuli, akiagana  Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambae ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages