Breaking News

Your Ad Spot

Apr 11, 2016

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AZINDUA TAASISI YA (BASILA MWANUKUZI EMPOWERMENT FOUNDATION)


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy
Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation)
yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili
kujiinua kiuchumi  hasa Mama Lishe kwa kushirikiana na wadau mbali
mbali. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni
Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Basila Mwanukuzi (kulia), Kaimu Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja pamoja na Mwakilishi wa Mama
Lishe, Bi. Grace Foya.

2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika  jijini Dar es salaam.

3
Basila Mwanukuzi Mkurugenzi wa Taasisi ya  (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation) akimkaribisha Waziri Ummy Mwalimu ili kuzungumza na wageni waalikwa na kisha kuzindua rasmi taasisi hiyo.
4
Baadhi ya ndugu na wanafamilia wa Basila Mwanukizi wakiwa katika hafla hiyo
5
Mrisho Mpoto kushoto na Miriam Ikoa mmoja wa waliowahi kuwa Miss Tanzania wakiwa pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo.
7
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy
Mwalimu akisalimiana na Basila Mwanukuzi mara baada ya kuwasili katika uzinduzi huo Katikati ni Kaimu Mkurugenzi  wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja

8
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy
Mwalimu akisalimiana na baadhi ya akina mama Lishe waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi.

9
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
10
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy
Mwalimu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.

11
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy
Mwalimu na Basila Mwanukuzi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages