.

GARI CHUPUCHUPU KUZAMA BAHARI YA HINDI

May 31, 2016

 Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi baada ya kutofuata sheria za vivuko, gari hilo likiwa limesheheni barafu ambapo haikufahamika mara moja ilikuwa ikipelekwa wapi.  Inakadiriwa mnamo  majira ya saa 11: 25 alfajiri, gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami mapema leo hii lilinasa kwenye mlango wa kivuko  hicho kwa kile kinachodaiwa ni kuzidisha mzigo mkubwa na kusababisha kunasa katika mlango huo na kusababisha MV Lami kusukumwa na gari hilo na ikabidi barafu hiyo kupakuliwa kisha gari hilo kuvutwa na na gari lingine lenye namba za usajili T 661 AXB na kupelekwa   Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini  Dar es Salaam   (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF WAENDELEA NA KAMPENI YA KUELIMISHA MADAKTARI KUHUSU FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAPATAPO MADHARA KATIKA KAZI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.  Emmanuel Humba, (kulia),  akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi Mhe. Anthony Mavunde alipowasilili kufungua mafunzo kwa Madaktari yanayohusu ajali na maginjwa yanayosababishwa na kazi Jijini Arusha jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na kampeni yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya  ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana na kazi safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Anthony Mavunde, huko jijini Arusha, ni muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria.
WCF imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.MADAKTARI WAPATA MAFUNZO YA KUREKEBISHA MIGUU ILIYOPINDA

 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa Dk.Richald Gellman  kutoka Califonia - San Fransisco Marekani (kushoto), akiwaonesha kifaa Chuma, maalumu kinacho tumika kufanya marekebisho ya mifupa iliyo pinda baada ya kuunga vibaya au kutounga kabisa,   madaktari  mbalimbali kutoka nchi mbalimbali , Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia, DRC Congo, Nigeri, Zimbabwe na wenyeji wao Madaktari wa Taasisi hiyo  wamehudhuria Mkutano huo utakaomalizika Juni 3, 2016 , unaendelea katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mifupa ya Fahamu Muhimbili (MOI) 
Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Pichani ni baadhi ni vifaa
 Madaktari Bingwa wakiwa katika chumba cha mikutano katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Moi

Mmoja wa Maktari Bingwa wa Taasisi hiyo mwenye miwani mbele Dk. Moonlight Mnyenye akiandika jambo wakati wa mkutano huo

SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

MS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda  PMAYA The President’s Manufacure of the Year  pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU / HASSAN SILAYO-MAELEZO
MS2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
MS3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
MS4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
WAF1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.(P.T)
WAF3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF4
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.
WAF5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.
WAF6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda.
WAF7
Wadau wa Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

RAIS KENYATTA AKUTANA NA RAILA ODINGA

Raila Odinga
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anafanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ili kuondoa wasiwasi wakati ambapo taifa hlo linajiandaa kwa uchaguzi mwaka mkuu ujao.
Bw Odinga alikatiza ziara yake ya kushiriki katika mazishi kusini magharibi mwa eneo la Natol ili kuhudhuria mkutano huo wa Uhuru Kenyatta katika mji mkuu wa Nairobi.
''Nilipokea simu kutoka ikulu ya mkutano na rais Uhuru Kenyatta.Naomba ruhusa yenu watu wa Narok nielekee kuzungumza naye,alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akiwaambia waombolezaji.Nitatangaza kwa Wakenya iwapo tumekubaliana na iwapo hatujakubaliana pia nitawaelezea'', aliongezea bw Odinga.
Uhuru Kenyatta
Muungano wa upinzani nchini Kenya Cord umeapa kuhudhuria mkutano jijni Nairobi hapo kesho,licha ya kwamba serikali ilitangaza kupigwa marufuku.
Watu kadhaa wameuawa katika ghasia kati ya polisi na wafuasi wa upinzani wanaopigania mabadiliko ya sheria ya kupiga kura. BBC

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA JUMUIYA YA ULAYA

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Waangalizi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana (2015), kutoka Umoja wa Ulaya. Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo  . Roeland Van De Geer (katikati) waliofika Ofisini kwake Dodoma leo Mei 31, 2016.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwasikiliza waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliofika Ofisini kwake kuwasilisha Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.
Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) ofisini kwake Dodoma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson Taarifa  ya miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi wa Uchaguzi  kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma. (PICHA NA ARON MSIGWA NA FATMA SALUM-MAELEZO).

TANZANIA ELECTED CHAIR OF THE AFRICAN GEOLOGICAL BODY

Tanzania President, Dr. John Pombe Magufuli
From Freddy Maro
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia.
TANZANIA has been elected a Chair of the Governing Council of African Minerals and Geosciences Center (AMGC) during its 36th annual meeting held at United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) conference Centre in Addis Ababa, Ethiopia over the weekend.
Tanzania was represented by The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz who read the Member country’s statement on behalf of Minister for Minerals and Energy Prof. Sospeter Muhongo.
In her speech, ambassador Naimi urged Member States to consider the development of other strategic minerals such as graphite; lithium and Rare Earth Elements (REEs) which she said were not only economically viable but also important.
“The mining sector is seriously affected by the drop of mineral prices in the global market especially for precious and base metals which are mostly mined by our countries. The decline of mineral price has resulted to low exploration activities to Member States especially my country, which has led to the decline of income to the centre (AMGC),” she said.
The Tanzania Permanent Rep. further advised the African Minerals and Geo-Sciences Center(AMGC) to be more creative and diversify its economic activities for its future and sustainability.
In order for Member States to catch up with fast growing technologies, the Ambassador said it was high time for AMGC to invest in Research and Development (R&D), in which the findings would be shared with Member States for optimal utilization of mineral rich resources found in the continent.
 She said that Member States should endeavor to make AMGC a truly Pan African Center of Excellence and to achieve this more needs be done in terms of marketing, which would increase the center’s visibility and capability and promote the tremendous work it does.
“It is therefore crucial that Member States pay their respective annual contributions to the center, in order to allow it to operate more efficiently and effectively and successfully implement its programs and activities,” She emphasized.
Ambassador Naimi said Tanzania was very proud to host the AMGC and stands committed to continue to honor and fulfill its obligation which aims inter alia, to facilitate and ensure that the center fulfills its mission and mandate to serve all African countries.     

In his opening speech the outgoing AMGC chairman who is also The Ethiopian Minister of Mines, Petroleum and Natural Gas H.E. Tolesa Shagi said Ethiopia and many African countries were adopting effective mineral management policies and strategies for the exploitation of mineral resources which were vital in boosting economic growth.
“The Mining sector in Ethiopia is providing support for the development of small and medium scale and artisanal mining enterprises and encourage greater participation of women in mining activities as a strategy for enhancing the development impact of mineral resources,” he said.
The Minister highlighted challenges facing mining industry in Ethiopia and Africa in general including shortage of capacity in negotiating, administering and monitoring the mining contracts as well as lack of sufficient geo-science information.
He said for African countries to overcome the challenges facing the mining industry they should opt for coordinated efforts as envisaged in the Africa Mining Vision (AMV) that was adopted by African Heads of States in February 2009, the long term goal of the vision is to create a Transparent Equitable and optimal exploitation of mineral resources to underpin broad-based sustainable growth and socio-economic development.
Speaking during the same occasion, the Deputy Executive Secretary and Chief Economist of ECA said that the Economic Commission for Africa(ECA) was acutely aware of the strategic importance of the AMGC as a partner to African Countries to collectively implement a transformative agenda for mineral resources development which would be instrumental for sustainable development.
African Minerals and Geosciences Centre (AMGC) formerly known as the Southern and Eastern African Mineral Centre (SEAMIC) started as a sub-regional development Centre for Eastern and Southern African nations namely, Angola, Comoros, Ethiopia, Mozambique, Tanzania and Uganda.
The Centre is located in Kunduchi Dar es Salaam Region, Tanzania.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATUA ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA "AFRICA WORLD HERITAGE"

May 30, 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix  Ntibenda Kijiko (katikati)  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha May 30, 2016 ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa  Kimataifa wa 'Africa  World Heritage' kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha -AICC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS MAGUFULI AMTEUA JAJI KIONGOZI SHAABAN LILA KUWA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI, MAKINDA NAYE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA NHIF

 Jaji Kiongozi Shaaban Lila, sasa ateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini
Bi. Anna Semamba Makinda, Mwenyekiti mpya wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF

RAIS DK JOHN MAGUFULI AFANYA UTEUZI LEO


ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA, RAJAB LUHWAVI MKOANI MANYARA, AKUTANA NA MKUU WA MKOA HUO NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM NGAZI ZA WILAYA

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, Luccas Ole Mukusu, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo Ndegesu Ndekobali. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na baadhi ya watumishi wa CCM mkoa wa Manyara, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo Ndegesu Ndekobali. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati  leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati  leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Afisa Tawala wa mkoa huo, Eliakim Maswi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. 
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara Ndekobali akishukuru baada ya mazungumzo hayo
wakiagana baada ya mazungumzo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiagana na Afisa Tawala wa mkoa wa Manyara Eliakim Maswi baada ya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Joel Bendera (Katikati), alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016.

AKAGUA JENGO LA OFISI YA CCM LILILOUNGUA MWEZI MACHI MWAKA HUU
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) apata maelezo kutoka kwa Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndegesu Ndekobali, alipokagua athari za kuungua jengo la CCM mkoa huo, lililopo mjini Babati. Jengo hilo liliungua Machi 7 mwaka huu.
Luhwavi akimaliza kukagua jengo hilo
Baadhi ya viongozi wa CCM wakimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi kuzungumza nao leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara mjini Babati
Luhwavi akiingia ukumbini
Luhwavi akiwa tayari ukumbini
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara, Ndekobali akitoa neno la utangulizi
Baadhi ya watunishi wa CCM kutoka wilaya za mkoa wa Manyara wakimsikiliza Luhwavi
Masoud Mbengua kutoka Kitengo cha Usalama na  Maadili, Makao Makuu ya CCM akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara akimkaribisha Luhwavi kuzungumza
Baadhi ya wafanyakazi wakichukua dondoo, wakati Luhwavi akizungumza nao. (Picha zote na Bashir Nkoromo
ยช