.

DKT. NDUGULILE ATAKA MABUNGE KUSHIRIKISHWA KWENYE MPANGO WA “AFYA MOJA”

Jun 29, 2016

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile(Mb) ameyataka Mataifa kushirikisha Mabunge katika kufanikisha mpango wa Usalama wa Afya Duniani (Global Health Security Agenda).

Akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia,, Dkt Ndugulile alisema, “Mabunge yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kwenye utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani kwa kusimamia Serikali na kuhakikisha hatua zote muhimu zinatekelezwa; kutunga Sheria zitakazosimamia utekelezaji wa mpango huu pamoja na kuhakikisha mpango huu unapata fedha za kutosha kutoka kwenye Bajeti ya Serikali”.

Dkt Ndugulile alisema kuwa muingiliano wa shughuli za kilimo, mifugo na shughuli nyingine za kibinadamu zimesababisha baadhi ya magonjwa ya wanyama kuleta athari kwa binadamu na pia usugu wa madawa ya aina ya antibiotiki. Hivyo, kuna haja ya wadau wa sekta hizi kuwa na ushirikiano wa karibu chini ya mpango wa “Afya Moja” (One Health). 
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile (Mb) (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia.
Alisema kuwaIli mpango wa “Afya Moja” ufanikiwe in lazima maboresho yafanyike kwenye uratibu wa sekta mbalimbali ndani ya nchi na pia kuandaa mpango wa pamoja wa udhibiti na kushughulikia majanga.

Dkt Ndugulile aliyasema hayo kwenye mkutano wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani unaofanyika mjini Bali, Indonesia. Mkutano huu ulioanza tarehe 27 Juni unatarajia kuisha tarehe 30 Juni.
Dkt Ndugulile mbali ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mabunge Duniani (Inter Parliamentary Union) kuhusiana na masuala ya UKIMWI, Afya ya Wanawake, Vijana na Watoto.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA SADC NCHINI BOTSWANA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma (wapili kulia) kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na serikali wa Jumuiya yaMaendeleo kusini mwa Afrika ( SADC ) kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli Juni 28, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MAKONDA ATEMBELEA BANDA LA UN KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Makonda alifika katika banda hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) alipotembea banda la shirika hilo lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia kila mwananchi alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lillilopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.


Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG's) yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi walivyojipanga katika kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar. Kulia ni Maafisa Habari wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Usia Nkhoma Ledama. RC Makonda amekuwa mgeni kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka zake kwenye maonyesho hayo.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya pamoja huku wakiwa na bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17 ya SDGs na mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo kwenye ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea banda hilo na kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu SDGs na kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.

WATUHUMIWA WALIOUA MSIKITINI MWANZA NA KULE MAPANGO YA AMBONI NAO WAUAWA; WALIJARIBU KUWARUSHIA MABOMU POLISI JIJINI DAR ES SALAAM

Jun 28, 2016

  Kaanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye kituo kikuu cha kati cha Polisi jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017 huku akionyesha bomulakurusha kwa mkono (Hand Grenade) alilokutwa nalo mtuhumiwa wa mauaji ya msikitini jijiniMwanza hivi Karibuni. Kamanda Siro alisema, mtuhumiwa huyo ameuawa wakati polisi walipokuwa wakijaribu kumkamata nyumbani kwake huko Chamazi nje kidogo ya jiji, baada ya kujaribu kuwatupia bomu askari. (PICHA NA RASHID ZUBERI)
 Bomu alilokutwa nalo mtuhumiwa wa mauaji ya msikitini jijini Mwanza. Mtuhumiwa alikutwa huko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi nyumbani kwake Juni 27, 2017
 Bomu, bastola na risasi, zilizokamatwa na polisi wakati wa purukushani ya kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji ya waumini wa dini ya Kiislamu jijini Mwanza hivi karibuni. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, watuhumiwa wawili akiwemo pia aliyesababisha mauaji huko jirani na mapangoya Amboni mkoaniTanga wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi.
 Kaanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye kituo kikuu cha kati cha Polisi jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017
Bomu, bastola na risasi, zilizokamatwa na polisi wakati wa purukushani ya kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji yawaumini wa dini ya Kiislamu jijini Mwanza hivi karibuni. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, watuhumiwa wawili akiwemo pia aliyesababisha mauaji huko

YANGA VS TP MAZEMBE, MABOMU YARINDIMA UWANJA WA TAIFA, POLISI WAFUNGA MAGETI UWANJA WATAPIKA MASHABIKI WAGOMA KUONDOKA

 Gari la polisi likimwaga maji ya kuwasha, kuwatawanya mashabiki wa soka walioamriwa kurudi nyumbani baada ya uwanja wa taifa kujaa "pomoni" majira ya saa sita mchana Juni 28, 2016. Yanga inatarajiwa kumenyana na TP-Mazembe ya DCR kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la CAF hatua ya robo fainali. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID) NA K-VIS MEDIA UONGOZI wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, umelazimika kufunga mageti yote ya kuingilia uwanjani humo baada ya uwanja huo kujaa "pomoni" ilipofika saa 6 mchana. Polisi walifanya kazi ya ziada kuwazuia maelfu ya mashabiki wa soka waliojihimu mapema kufika uwanjani, ili kujionea pambano hilo la soka ambalo Yanga ilitangaza kuwa halitakuwa na kiingilio. Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya mashabiki hao wa soka ambao licha ya kuwaambia uwanja umejaa na warudi nyumbani ili kuona pambano hilo kupitia matangazo ya moja kwa moja ya runinga. Hata hivyo mushawishi huo ulishindikana na hapo ndipo polisi walipoamua kufyatua mabomu na kurusha maji ya kuwasha. Polisi walipata upinzani kidogo baada ya baadhi ya mashabiki kuanza kurusha mawe hata hivyo sio kwa muda mrefu kwani polisi waliongeza jitihada za kuwadhibiti na baada ya masaa mawili jitihada hizo zilizaa matunda
MTANZANIA ALIYEIBUKA MSHINDI WA KWANZA AFRIKA NA WA SITA DUNIANI KATIKA MASHINDANO YA KUSOMA QUR-AN KWA NJIA YA TAJIWEED AWASILISHA TUNZO KWA MZEE MWINYI LEO

Jun 27, 2016

Mwanazuoni kutoka Kondoa, Tanzania, Sheikh Rajay Ayub ambaye ameibuka mshindi wa kwanza Afrika na wa sita Duniani katika mashindano ya 37 ya Kimataifa ya usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed, yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Iran akikabidhi tuzo zake kwa Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika leo, kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania-BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam. Kulia ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakary Bin Zubeir na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa, Alhaj Omary Kariati ambaye aliratibu hafla hiyo. KWA PICHA KEM-KEM ZA HAFLA HIYO>>BOFYA HAPA 

KITUO CHA HUDUMA NA MTOTO EAGT LUMALA MPYA CHA JIJINI MWANZA CHAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO WENYE UHITAJI

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.

Akikabidhi msaada huo hii leo, Askofu wa kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola, amesema watoto 18  waliokabidhiwa msaada huo ni sehemu ya watoto 264 wanaolelewa na kanisa hilo kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto iliyoanzishwa kanisani hapo tangu mwaka 2010.

Askofu Dkt.Kulola amesema hiyo si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa msaada wa vitu hivyo na kueleza kuwa limekuwa likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.

Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel, amesema msaada huo umetolewa baada ya uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.

Wazazi, walezi na watoto walionufanika na msaada huo, wameushukuru uongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.

Msaada huo wa vitanda, magodoro, mashuka, mahindi na mchele umegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa ambazo zilitolewa na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo cha Huduma ya Mtoto ambacho kiko chini ya Kanisa hilo.
Mmoja wa watoto walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya watoto wengine
Mmoja wa wazazi/walezi walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya wazazi/walezi wengine
Mmoja wa wazazi/walezi walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya wazazi/walezi wengine
Watoto baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
Watoto baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
Mtoto katika ubora wake
Msaada wa vyakula kwa watoto wanaolelewa na Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Kila mmoja katika jamii anao wajibu wa kuhakikisha mtoto anapata malezi bora

TAASISI YA NITETEE YAITAKA SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA TAASISI ZINAZOFANYA KAZI VIZURI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.
 Flora Lauwo akitafakari jambo alipokuwa akifuatilia mwenendo wa mijadala ya Bunge mjini Dodoma.
Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula katika viwanja vya Bunge, DodomaSerikali imetakiwa kuziangalia kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuanza  kutoa ruzuku kwa  taasisi za watu binafsi zinazofanya kazi  ya kufuatilia na kubaini matatizo yanayowakumba wananchi kama afanyavyo, Flora Lauwo Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee.

Licha ya serikali kutambua mchango unaotolewa na taasisi hizo,  jamii nayo imeaswa kujitokeza kuwasaidia watu ambao wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo  unyanyasaji wa kijinsia ,maradhi na wale wanaohitaji msaada wa kupata elimu .

Kufatia serikali kutambua mchango huo baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wanajitokeza na kubainisha changamoto zinazowakumba.


Yapo malengo yanayowekwa na wadau hao ili kutimiza ndoto za kuwasaidia watanzania

“Lakini wapo Wajanja ambao wamekuwa wakinufaisha na misaada wanayopewa na wafadhili badala ya kuwasaidia walengwa,” alisema Lauwo.Taasisi ya nitetee inajishughulisha na utatuzi wa matatizo yanayozikumba  familia zinazoishi katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa imeshazifikia kaya 36 pamoja na kuwapeleka watoto 20 shule.

ASILIMIA 87 YA WATANZANIA WANATUMIA POMBE ZA KIENYEJI. MIKOA YA DAR NA MOSHI YADAIWA KUONGOZA

Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa, asilimia 87 ya Watanzania wanakunywa pombe za kienyeji huku miji ya Dar es Salaam na Moshi ikitajwa kwamba, inaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi wa pombe hizo.

Hayo yameelezwa na Dakta Kissah Mwambene Katibu wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Akili Tanzania wakati alipokuwa akitoa mada kwa Wabunge juu ya madhara na athari za matumizi ya pombe na kuongeza kuwa, takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanywa nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2010. Kwa mujibu wa utafiti, miji ya Dar es Salaam na Moshi inaongoza nchini Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaotumia pombe za kienyeji. 

Dakta Mwambene amesema kuwa, utafiti huo unaonyesha juu ya kuweko ongezeko kubwa la utumiaji wa pombe kupita kiasi nchini Tanzania jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii. 

Awali akifungua semina hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dakta Hamisi Kigwangala alisema kuwa, ulevi ni tatizo kubwa katika jamii na kwamba, asilimia 30 ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15 wameanza ulevi, asilimia 80 ya wasomi wanatumia pombe huku asilimia 63 ya watu wanaokaa maeneo ya jirani na vilabu vya pombe wakitumia ulevi.

RAIS KAGAME KUFUNGUA MAONYESHO YA BISHARA YA KIMATAIFA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

 MAONYESHO ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam, yanayoandaliwa na Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania, (TANTRADE), kwa mwaka huu wa 2016, yanatarajiwa kuanza rasmi, Jumanne Juni 28, 2016 kwenye viwanja vya Julius Nyerere, barabara ya Kilwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. K-VIS BLOG imeshuhudia waonyeshaji bidhaa kwenye mabanda mbalimbali wakiendelea na hatua za mwisho za kuandaa mabanda yao kama ambavyo pichahizi zinavyoonesha leo Juni 27, 2017. Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame anatarajiwa kuyazindua maonyesho hayo. (PICHA NA K-VIS MEDIA)ยช