.

MGODI WA BUZWAGI WAKABIDHI MADAWATI 4494 KWA AJILI YA SHULE ZA MKOA WA SHINYANGA

Jul 31, 2016

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi umekabidhi madawati 4494 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 548 kwa ajili ya shule za sekondari na msingi za mkoa wa Shinyanga.Mwandishi wetu Kadama Malunde,anaripoti.

BOHARI LATEKETEA KWA MOTO SINZA LEGO JIJINI DAR JIONI HII

Bohari likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea
Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto ,  hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua. Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
BOHARI   ya  kuhifadhi mataili  na vifaa vyengine vya magari lililopo eneo la  Sinza Lego limeteketea  kwa moto na kusababisha  hasara ya mamilioni ya shilingi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka  eneo  hilo  kilidokeza kuwa moto  umeteketeza  mataili, huku chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika.
Chanzo hicho   pia  kilisema kuwa mmiliki wa ghala hilo hajakufahamika kwa jina, hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea ili kuzungumzia  hasara ya mali iliyoteketea kwa moto.
Alisema jirani ya bohari kulikuwa  Gereji ambayo haikuathirika na moto, mpaka jioni kikosi cha zimamoto  kiliendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika.

Hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni zinaendelea kuelezea.

WAZIRI NAPE AONGOZA KUAGA MWILI WA MPIGAPICHA MKONGWE JOSEPH SENGA, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO, AKUTANA NA LOWASSA, MBOWE

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ameongoza kuuaga mwili wa Mpigapicha Mkuu wa Tanzania Daina, Joseph Senga (pichani), ambaye ni mpigapicha mkongwe, aliyefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu. Mwili wa Josefu Senga uliwasili nchini jana, na kuagwa leo, Sinza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitoa heshima kwenye mwili wa marehemu Joseph Senga, Sinza jijini Dar es Salaam, leo
 Naibu Wazri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia wambura akitoa heshima kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga leo Sinza Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania taima alilokuwa akifanyia kazi Joseph Senga, akitoa heshima mwa mwili wa marahemu Joseph Senga. Wafuatao ni waombolezaji wengine wakitoa heshima kwa mwili wa marehemu Joseph Senga


 Mjane wa Marehemu Joseph Senga akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mumeweJeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga likibebwa kuingizwa kwenye gari tayari kwa safari, waliobeba jeneza hilo wengi wao ni wapigapicha za habari
KABLA YA KUAGA MWILI
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, akiteta jambo na Waziri Mkuu wa zamani, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kabla ya hatua ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga. Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema Joseph Senga Freeman Mbowe,  kabla ya hatua ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, akisalimiana na Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kipentekoste William Mwamalanga, wakati wa shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga. KWA PICHA ZAIDI ZA MSIBA HUU>>>BOFYA HAPA
ยช