Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2016

ASKARI WA BURUNDI WATUHUMIWA KUFANYA UFISADI CAR

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, askari wa kulinda amani kutoka Burundi wanakabiliwa na tuhuma za kufanya ufisadi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mtandao wa habari wa Africa Times umemnukuu Stéphane Dujarric akisema kuwa, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaodhaniwa kutenda vitendo vilivyo kinyume na maadili dhidi ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kutoka nchini Burundi.
Amesema, Umoja wa Mataifa umeamua kuwarejesha nyumbani askari hao wa Burundi kama adhabu ya vitendo vyao hivyo.
Siku ya Ijumaa, Umoja wa Mataifa ulisema umeanzisha uchunguzi kuhusu tuhuma kuwa askari wa kulinda amani wa umoja huo wanafanya ufisadi wa kimaadili huko CAR.
Amesema tuhuma hizo zilitolewa mwezi Mei mwaka huu na kwamba walalamikaji walisema askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa walifanya vitendo vilivyo kinyume na maadili katika eneo la Kemo la kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Hii si mara ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa kuwarejesha nyumbani maafisa wanaohudumu katika kikosi cha kulinda amani ya umoja huo huko Jamhuri ya Afrika kwa sababu kama hizo za ufisadi wa kimaadili.
Mwaka 2015 kuliripotiwa kesi 69 za vitendo viovu vilivyo kinyume na maadili vilivyofanywa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages